Uchaguzi 2020 Kiapo cha Halima Mdee na wenzake: Mnawaonea kuwaita wasaliti bila kujua kilicho nyuma ya pazia


Mambo gani waseme utamaduni wa unafiki ni mbaya sana kama kuna makubaliano yasemwe watu waelewe kula gani la kuficha!
 
Acheni utopolo bana! Error in thinking.
 
Tatizo kubwa la wabongo hatujui siasa ni nini. Pamoja na yote yaliyotokea ktk uchaguzi CDM wangesusia hizi nafasi 19 za wabunge viti maalum ningewashangaa sana. Katika mapambano ya kisiasa eneo bunge ni muhimu sana katika kupaza sauti.
Nakuunga mkono mkuu.
 
CCM ndio mnaowatetea kina Halima Mdee. Huyu Ni kigeugeu jina lake tu utata mtupu, hajulikani hata dini gani Halima James
Sina chama lakini nawaunga mkono akina mdee, kwasababu wanahitaji hela ili chama.kiendelee kuendesha shughuli zake.
Bila hela mtakisahau hicho chama chenu, ma hamtachukua mwaka kujiona mmefutika tz.
Halafu bado mtaendelea kuwa live pale bungeni jambo ambalo naona ni la msingi pia.
Au unategemea kesi alizofungua Lissu. Hata kwa mfano tukawekewa vikwazo, umeona Zimbabwe yaliyotokea? Mwisho wa siku wanakabidhiana wao kwa wao.

watz hamko tayari kuchukua hatua, basi waache akina halima wakale mshahara wa bunge mpaka mtakapokuwa tayari kuchukua hatua.
 
Usaliti ni usaliti tu hata kama umeelekezewa bunduki kichwani. Hivyo hata hayo yaliyopo nyuma ya pazia ni usaliti tu.
 
Zamani kabisa ilikuwa tunasema NI YEYE. Siku hizi tunasema NI WAO.
 
Kigogo alishasema kitambo tu kuwa kuna watu watakiketa chama bila ganzi....
Tuache kumuamin mzee kigogo tuje kwako...
Endelean kuwatetea... hii ishu ilikuwa inafahamika
 
Madada poa hao. Wakikunwa wanachekelea. Hata nyoka alienda kumkuna kwanza Hawa ndipo akafanikiwa kumlaza Adam. Tunaambiwa na maandiko kuwa ishini na wanawake kwa akili.
 
Hongera Na Pongezi kwa Kambi Rasmi.Mh Halima.Bulaya.kwa Kula Kiapo.sasa Ni wakati wa Kwenda kutumikia Wananchi wenu.na kuleta maendeleo na sasa ni wakati wa kinamama kushine.kina mamam oyeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo gani waseme utamaduni wa unafiki ni mbaya sana kama kuna makubaliano yasemwe watu waelewe kula gani la kuficha!
Kwa mfano wewe ukitekwa alafu watekaji wakakulawiti, ukifika hadharani utasema kuwa miongoni mwa mateso niliyopata ni kulawitiwa?
 
Usaliti ni usaliti tu hata kama umeelekezewa bunduki kichwani. Hivyo hata hayo yaliyopo nyuma ya pazia ni usaliti tu.
Apoteze maisha yake kisa wewe usimuone msaliti? Zile kesi mahakamani utamdhamini wewe?
 
CCM ndio mnaowatetea kina Halima Mdee. Huyu Ni kigeugeu jina lake tu utata mtupu, hajulikani hata dini gani Halima James
Kwani ulishasikia mwanamke ana dini? Kama mume wake alimweleza abadili jina la ukoo akaitwa James kuna tatizo gani? Mama wa Taifa anaitwa Maria Nyerere?? sasa kwa Halima lipi geni? Bujibuji una msongo wa mawazo pole usije ukajitundika, wenzako ndiyo wanavuta mkwanja tangu bunge lilipozinduliwa
 
Tuwe wakweli tu, ni nani kati yetu angechagua kisu kikali au sahani yenye dhahabu? Hao waheshimiwa sidhani kama wana kazi nyingine nje ya siasa, wanaweza kuwa wameharibu future yao ya kisiasa lakini angalau wanaweza kuwa na miaka mitano ya kujipanga na kutengeneza future yao nje ya siasa kama itabidi kuwa hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…