Kiapo laana hatari zaidi

Kiapo laana hatari zaidi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ni kiapo cha damu na maji, hii ni kwasababu vyote viwili vina uhai na katika kukutanika kwao huumba roho isiyokufa na yenye madhara makubwa kutokana na kiapo au manuizi husika.

Kuna hivi viapo vya kuchoma moto maandishi ya damu, hivi humtesa mtu kwa muda tuu lakini baadae hufa na kupoteza nguvu kabisa lakini pia vikiwa vimeshaacha madhara makubwa tuu, chukulia mfano moto unavyoteketeza mali au uhai.

Kiapo kingine cha manuizi ni kile cha njiapanda, cha kuandika manuizi yako na kwenda kuyatupa au kuyazika njiapanda, hapa yatakanyagwa na kila aina ya watu kutoka pande zote, hiki hufanya Kazi mbaya sana kipindi cha uhai wake, mlaaniwa huteseka hasa na hafanyi lolote atafanikiwa mpaka ile katarasi na vitu vyake vioze vyote na kuharibika kabisa.

Lakini kiapo laana cha maji ni kitu kinachoishi milele, na husambaa mbali kwakuwa robotatu ya dunia ni maji na robotatu ya mwili wa binadamu ni. Maji pia na vyote vina uhai.

cc:blogmaster
 
Mkuu mshana jr vipi kile kiapo cha maji tulichopatiwa tukiwa wadogo huku wazazi wakiamini tunabatizwa, kinaleta laana ukiamua kuachana na ubepari wa kanisa.
 
Ubatizo ni agano la milele ndio maana hakuna Ubatizo mara mbili, umebatizwa kwa jina fulani ukakua nalo ukasoma nalo, baadae ukaja ukapata maarifa mengine ya kidunia na kuona hakuna Mungu, huo ni mtazamo wa ukubwani, lakini tayari una utambulisho au hauwezi kufa
 
Mkuu Mshana ahsante ila sio kwamba naona hakuna Mungu hapana, natambua kwamba kuna Mungu muumba wa mbingu na nchi muweza wa yote. ila sio kwa jinsi tunavyo hubiriwa kanisani.
 
Vipi kile kiapo cha wanasiasa kama mawaziri,mabalozi,wakuu wa mikoa wanaapa tena wanashika misaafu halafu wanakwenda kinyume na maapizo inakuaje ?.

Zile ni taratibu tu za kidunia zisizo na chembe ya ukweli, ni njia ya mwanadamu kujifariji na kuleta imani kwa wale atakaowaongoza lakini pia kujijengea hofu mwenyewe kutokana na kile anachokisema
 
Mkuu Mshana ahsante ila sio kwamba naona hakuna Mungu hapana, natambua kwamba kuna Mungu muumba wa mbingu na nchi muweza wa yote. ila sio kwa jinsi tunavyo hubiriwa kanisani.

Yeah nimekuelewa Gamaha ila ilibidi nitoe jibu la jumla kwa faida ya wengi... Infact dini ni njia ya mwanadamu kumtafuta Mungu ambayo ina mapungufu mengi sana
Ni kupitia dini hiyohiyo watu kwa maelfu wameangamia Kukosana na hata kuwa na mambo ya ajabu ajabu
Dini badala ya kuwa sehemu ya faraja na kimbilio kwa mwanadamu imekuwa kitu cha kuogofya chenye sura nyingi.... Kwahiyo tunapoingia kwenye nyumba za ibada tujiongeze
 
Last edited by a moderator:
Dini ndio njia imetumika na wanadamu wachache kutawala wengine na kujipatia pesa. Ili kufanya hivyo huko kwenye madhhebu yao wanaweka sheria ambazo ukienda kinyume chake unaambiwa ukifa utaenda motoni. Vitisho.

Sasa kama roho ni kitu kisicho na mwili, ukikiweka motoni kitaungua aje? Au maumivu itasikiaje? Mshana Jr hebu comment hapa. Dhana ya motoni. What is it all about?
 
Mfamaji kwanza ni muhimu kukubaliana kwamba pamoja na mapungufu yote ya dini lakini imesaidia Sana kuifanya dunia sehemu salama kama hivi tunavyoiona Leo na hii ni ile hofu itokanayo na maisha baada ya kifo na moto wa milele
Pili dhana ya motoni ipo katika uhalisia wake tena hata kabla ya kifo, ukitembelea hospital zetu Jela zetu na zile nchi zenye migogoro mikubwa ya kivita utaiona jehanam katika uhalisia wake, watu wanateseka, wako kwenye maumivu ya kutisha lakini wako hai hawa wako jehanam, wako motoni, motoni ni mateso na Hakuna raha yoyote
Roho ndio kila kitu kwenye mwili, furaha zako, tabu zako, fadhaa zako, raha zako, maumivu yako Mapenzi na hisia zozote zile ni kwasababu una roho, nje ya roho ni jumbamwili tu lisilo na uhai, yani kama sanamu lisilo na hisia zozote ndio maana dhana ya kwenda kuchomwa motoni ni ya kiroho zaidi kuliko kimwili
 
Last edited by a moderator:
Ubatizo ni agano la milele ndio maana hakuna Ubatizo mara mbili, umebatizwa kwa jina fulani ukakua nalo ukasoma nalo, baadae ukaja ukapata maarifa mengine ya kidunia na kuona hakuna Mungu, huo ni mtazamo wa ukubwani, lakini tayari una utambulisho au hauwezi kufa

Acha fiksi bro, kwanza ubatizo sio ishu ya jina, ndio maana hakuna ubatizo wa biblia uliombadili mtu jina, na kama upo basi hayakuwa malengo.

Hawa wanaowabatiza na kuwapa majina wanataka muwe watumwa wao, na ndio maana wanafanya mambo fulani yasiyoeleweka ili kukufunga na ushetani wao, ushajiuliza kwanini ni vigumu sana kumshawishi Mkatoliki kwa hoja, kwa kuwa kuna nguvu imemshika asiyoiona.

Kwanza dini sio maarifa, ndio maana hayana logik, hayasubiri uwe na akili, unaanza kupewa utotoni ukiwa hujijui na huwezi kutafakari, kifupi ni kutekwa...
 
Dini ndio njia imetumika na wanadamu wachache kutawala wengine na kujipatia pesa. Ili kufanya hivyo huko kwenye madhhebu yao wanaweka sheria ambazo ukienda kinyume chake unaambiwa ukifa utaenda motoni. Vitisho.

Sasa kama roho ni kitu kisicho na mwili, ukikiweka motoni kitaungua aje? Au maumivu itasikiaje? Mshana Jr hebu comment hapa. Dhana ya motoni. What is it all about?
Mfamaji, shkamoo bro. Mtaji wa dini ni hofu, hofu ya moto wa milele na maisha ya mbinguni, huku wao wakikusanya vyote vinono vya kimwili...
 
Last edited by a moderator:
Acha fiksi bro, kwanza ubatizo sio ishu ya jina, ndio maana hakuna ubatizo wa biblia uliombadili mtu jina, na kama upo basi hayakuwa malengo.

Hawa wanaowabatiza na kuwapa majina wanataka muwe watumwa wao, na ndio maana wanafanya mambo fulani yasiyoeleweka ili kukufunga na ushetani wao, ushajiuliza kwanini ni vigumu sana kumshawishi Mkatoliki kwa hoja, kwa kuwa kuna nguvu imemshika asiyoiona.

Kwanza dini sio maarifa, ndio maana hayana logik, hayasubiri uwe na akili, unaanza kupewa utotoni ukiwa hujijui na huwezi kutafakari, kifupi ni kutekwa...

Unaziita fix Halafu unaungana nazo bila kujijua, ungesimama kwenye hoja hiyohiyo ya fix, Ubatizo ni agano la milele, na mtu hawezi kubatizwa bila jina... Pembua kwa uangavu na si kwa kutaja sehemu ndogo tu ya kile Usichokijua
 
Sikuja kubisha wala kusaka ushindi, Yesu alibatizwa kwenye Mto Yordani, alipewa jina gani?
 
Kuna mahali nimemtaja?

Mtaje ambaye alibatizwa kwenye biblia akapewa jina... Na mbatizaji wa kwanza anajulikana, na hakuwa Padri wala Mchungaji.

Mbona hoja zingine umeziruka, umeona hiyo tu..
 
Siziruki soma mwanzo wa post hii utaelewa....haya mengine umeyaleta wewe kwahiyo yaweke wazi, tusitegane ila sijawahi kuona ubatizo wa kibubububu popote pale kama una ithibati zozote ziweke hapa kwa manufaa ya wote
 
Back
Top Bottom