Kiasi cha mafuta kwa bar moja

Kiasi cha mafuta kwa bar moja

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Wanajamvi naomba mnisaidie. Hizi gauge za mafuta za kielektroniki, bar moja inawakilisha lita ngapi? Inanipa shida kufanya makadirio ya kiasi cha lita ninachokuwa nacho. Wataalamu nisaidieni.
 
Inategemea na ukubwa wa tank, fuel gauges zinapima ujazo kwa kuzingatia eneo la tank , kuna robo, nusu , robotatu na full.
Si rahisi kupata idadi ya lita kwa kuangalia gauge , ila kama unajua full tank linaingia lita ngapi , utaweza kujua nusu na robo ni wastani wa lita ngapi pia
 
Wanajamvi naomba mnisaidie. Hizi gauge za mafuta za kielektroniki, bar moja inawakilisha lita ngapi? Inanipa shida kufanya makadirio ya kiasi cha lita ninachokuwa nacho. Wataalamu nisaidieni.
unatakiwa kujua tank la gari yako lina ujazo wa lita ngapi, kisha uhesabu hizo bar na ugawanye, roughly utajua kila bar ni approx lita ngapi
 
Succeed boss wangu. Tank ni lita 50. Tank likiwa full bar huwa ziko 8. Ukigawa 50 kwa 8 inakuja kama 6.25. Uhalisia siyo. Bar ilibaki moja, alarm ikablink. Nilipoweka lita 5 ikaongezeka bar moja. Kwa kukadiria, tank lilikuwa na lita kama 6 na hivi. Lakini bar zikawa mbili. Kwa hiyo, kanuni ya ujazo wa tank kugawa kwa idadi ya bar, ni kama inagoma.
 
kwa kawaida gari ikiwasha taa kuashiria mafuta kuisha huwa zimebaki angalau lita tano za kukuwezesha kusafiri hata 20km na zaidi. hili lisikusumbue ni kawaida kabisa
 
Succeed boss wangu. Tank ni lita 50. Tank likiwa full bar huwa ziko 8. Ukigawa 50 kwa 8 inakuja kama 6.25. Uhalisia siyo. Bar ilibaki moja, alarm ikablink. Nilipoweka lita 5 ikaongezeka bar moja. Kwa kukadiria, tank lilikuwa na lita kama 6 na hivi. Lakini bar zikawa mbili. Kwa hiyo, kanuni ya ujazo wa tank kugawa kwa idadi ya bar, ni kama inagoma.
Lakini ikumbukwe kuwa kuna reserve ya mafuta baada ya gauge kuonyesha yameisha kabisa na red imewaka

Baada ya red light kuwaka hapo ujue kuna Lita 10 zimo kwenye tank

Hivyo usiogope kuendesha ila kwa sababu ya kulinda uchafu usinyonywe tunashauriwa wese liwemo juu kila wakati

Ni bora kujifunza ikifika robo tank unajaza au unajaziliza kwa mfuko wako ulivyo
 
Ahsante kwa uelimishaji mzuri.
 
Back
Top Bottom