Kiasi gani Wazungu wametuacha kiteknolojia

Kiasi gani Wazungu wametuacha kiteknolojia

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Habari wanamember,

Kwanza kabisa nataka niweke bayana wazungu ambao nawazungumzia, hawa ni wazungu ambao walikuja huku kwetu Afrika na kututawala, kwa kesi yetu ya Tanzania nitawaongelea Wajerumani na Waingereza.

Kipimo nitakachokitumia kupima uwiano ni miaka, kwamba itatuchukua miaka mingapi kufika umahiri walionao wenzetu katika teknologia. Teknologia inatafrisiwa kama kutumia ujuzi wa kisayansi katika kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii.

Kutokana na kufanyika mradi mkubwa wa reli SGR hapa tanzania nitatumia reli kama uwanja wa kutupima sisi watanzania na wazungu, haya ndo majibu yanayopatikana

WAMETUZIDI MIAKA >200+
Treni na reli kwa wazungu sio kitu kigeni kwani wanacho tokea miaka ya 1800, hivyo basi kutokana na sisi mpaka sasa kutokuwa na uwezo wa kutengeneza treni na reli yetu hivyo inatuonyesha ya kwamba ni miaka zaidi ya mia mbili wapo mbele.

Hii inamaanisha kama ni umri basi wao wapo mbele miaka mia mbili na zaidi hali hii inawafanya kuwa na uzoefu mkubwa sana kulinganisha na sisi, chukulia mfano mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi alivyo kuwa mjuzi itakuwa vipi kwa mtu mwenye uzoefu miaka mia mbili na zaidi.

Kutokana na kuwa na jibu ambalo sio number kamili ( miaka mia mbili na Zzidi) nataka kutumia baathi ya nadharia ili kufanikisha adhimio langu la kupata miaka kamili ya kiasi ambacho tumepitwaa na wazungu hivyo natumia kigezo cha utambuzi wa majengo ya kihistoria ambapo kwa Tanzania jingo la utambuzi unaanzia miaka 1868 na kushuka chini, na ukiangalia Wajerumani nyumba zao za kihistoria zinanza miaka ya 1300 sasa kwa kufanya hesabu za kutoa. Tupapata tukitafutacho.

1868 – 1300 = 568

Hivyo basi napenda kuhitimisha mjadala wangu kwa kusema ya kwamba tumepitwa miaka mia tano na sitini nane.

Najua ya kwamba njia yangu ina mapungufu kaza wa kaza kwani jengo la zamani tanzania lilijengwa na sultani OLD BOMA na sio na wazawa. Hii miaaka ambayo inaonyesha tumepitwa inaweza kutasfiri katika Nyanja mbalimbali.

Tunakuwa vichekesho ambako tunasema wasituingilie mambo yetu ya ndani, ni kama umekuwa kaka unatoa ushauri kwa dogo asije akapotea kwa sababu umeona mengi na unawajibika kutoa ushauri.
 
Hawajatuzidi kitu, sio washindani wetu.... walifanikiwa kutupumbaza na kutuondolea ufahamu wa asili yetu sasa tunahangaika tu.
 
Hawajatuzidi kitu, sio washindani wetu.... walifanikiwa kutupumbaza na kutuondolea ufahamu wa asili yetu sasa tunahangaika tu.
Katika technology wametuzidi, tujifunze kukubali baathi ya mambo, kuna mambo mengine tumewazidi
 
Habari wanamember,

Kwanza kabisa nataka niweke bayana wazungu ambao nawazungumzia, hawa ni wazungu ambao walikuja huku kwetu Afrika na kututawala, kwa kesi yetu ya Tanzania nitawaongelea Wajerumani na Waingereza.

Kipimo nitakachokitumia kupima uwiano ni miaka, kwamba itatuchukua miaka mingapi kufika umahiri walionao wenzetu katika teknologia. Teknologia inatafrisiwa kama kutumia ujuzi wa kisayansi katika kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii.
Jioneee wewe mwenyewe hapa kwamba itachukua miaka mingapi kuwafikia kitechnolojia unaowazungumzia..
 
Wazungu wameturudisha nyuma kwa kutupatia chama Cha mazuzu, pamoja na rasilimali zetu tulizonazo bado hazijatufaidisha
Mwafrika ni mwafrika tu....hata ungepewa chama gani....maendeleo ni haya haya tena inawezekana tungekuwa nyuma sana kama kingekuwa chama kingine....nchi zote za Africa mulemule tu labda zile wazungu walizowekeza sana kama Africa kusini.... Hivyo wacha kujidanganya
 
Wametuacha milele

Mpaka sasa eti tunahangaika na maji safi na salama alafu unawaza teknolojia na wazungu
Hili ni jibu tosha. Mpaka leo hatuoni umuhimu wa lifti katika majengo yetu, nafikiri wala hatusongi mbele kujaribu kuwafikia, bali tunatokomea kusikojulikana, tunapoteza mwelekeo.
 
Wazungu wameturudisha nyuma kwa kutupatia chama Cha mazuzu, pamoja na rasilimali zetu tulizonazo bado hazijatufaidisha
Nyerere ndo katurudisha nyuma miaka 1800 kwa kudai uhuru hewa.
 
Back
Top Bottom