Kwanza kabisa nataka niweke bayana wazungu ambao nawazungumzia, hawa ni wazungu ambao walikuja huku kwetu Afrika na kututawala, kwa kesi yetu ya Tanzania nitawaongelea Wajerumani na Waingereza.
Kutokana na kufanyika mradi mkubwa wa reli SGR hapa tanzania nitatumia reli kama uwanja wa kutupima sisi watanzania na wazungu, haya ndo majibu yanayopatikana
WAMETUZIDI MIAKA >200+
Treni na reli kwa wazungu sio kitu kigeni kwani wanacho tokea miaka ya 1800, hivyo basi kutokana na sisi mpaka sasa kutokuwa na uwezo wa kutengeneza treni na reli yetu hivyo inatuonyesha ya kwamba ni miaka zaidi ya mia mbili wapo mbele.
Hii inamaanisha kama ni umri basi wao wapo mbele miaka mia mbili na zaidi hali hii inawafanya kuwa na uzoefu mkubwa sana kulinganisha na sisi, chukulia mfano mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi alivyo kuwa mjuzi itakuwa vipi kwa mtu mwenye uzoefu miaka mia mbili na zaidi.
Kutokana na kuwa na jibu ambalo sio number kamili ( miaka mia mbili na Zzidi) nataka kutumia baathi ya nadharia ili kufanikisha adhimio langu la kupata miaka kamili ya kiasi ambacho tumepitwaa na wazungu hivyo natumia kigezo cha utambuzi wa majengo ya kihistoria ambapo kwa Tanzania jingo la utambuzi unaanzia miaka 1868 na kushuka chini, na ukiangalia Wajerumani nyumba zao za kihistoria zinanza miaka ya 1300 sasa kwa kufanya hesabu za kutoa. Tupapata tukitafutacho.
1868 – 1300 = 568
Hivyo basi napenda kuhitimisha mjadala wangu kwa kusema ya kwamba tumepitwa miaka mia tano na sitini nane.