Kiasi gani Wazungu wametuacha kiteknolojia

Kosa kubwa walilofanya hawa wapigania uhuru mimi nawaita wapigaji ( kumfukuza mkoloni na kula wao) wangedai usawa yaani haki sawa ya kushiriki shughuli za uchumi wakawaacha tukashirikiana nao tungekuwa mbali sana
 
Katika technology wametuzidi, tujifunze kukubali baathi ya mambo, kuna mambo mengine tumewazidi

Hoja mezani ni teknolojia, kama unataka mambo mengine sijui utayapima kwa order ipi.... mfano useme tumewazidi uvivu wa kufikiri..!!
 
Cha ajabu Hadi Leo hii tunafundishwa namna ya kunawa mikono ili kujiepusha na kipindupindu....
Sisi waafrica tumeachwa zaidi ya miaka 1000

Mamamae unapishana na njemba inatoka chooni halafu inalipita sinki la kunawia kama haioni vile, hapo akitoka ni salamu za kushikana mikono smdh.... unajiuliza unaacha tu au mtu atanawa kwa mkumbo tu ila akiwa pekee yake hana muda kabisa.
 
Yani tunachokifanya kwenye huu uzi ndio kinazidi kutuweka mbali kuwakuta na kweli hatutowakuta milele
 
Kwenye mambo ya kugegedana, style mbalimbali, kukata viuno, umbea, uvivu, maneno mengi, nk huko tumewaacha mbali sana..

Jielekeze kwenye hoja, teknolojia.... ambayo hata hizo kugegedana mnashinda pornhub kujifua.
 
Tukipita njia walizopita wao tutahitaji miaka 500 kufika walipo leo.Tukiwaiga wao walivyofanya kamwe hatuta wafikia,kwani tutakuwa kuwa tunawafuata kwa nyuma.

Solution ni kutafuta njia yetu ya kufuata angalia nchi kama china na nchi za falme za kiarabu.
 
Yale mambo ambayo bibi yako wa Namtumbo au mjomba wako wa Shinyanga angekatwa katwa mapanga kuitwa mchawi wenzio wameyafanya na wanafikiria pakubwa zaidi!.
Hujanielewa!?.
Namaanisha wazungu wana TRENI ZINAZOELEA!...yani wameweza fanya treni ikatembea kwa kutumia SUMAKU sio haya matakataka ya SGR!.. Sikufuru katafute/kagugo hii kitu MAGLEV TRAINS!!!..

(Bill Gate alijaribu kutuboost afrika labda tuwasogelee wao kiteknolojia kupitia mradi wake wa "LeapFrog" akaishia kugundua kusafisha maji ya choo yanyweke upya kizembezembe!, but seriously leo hii tutamfikia mjerumani ambaye anafunga smartphone traffic light ili kusaidia wale smartphone addict wasigongwe na magari!.
Nimekuacha tena!?.
Munich kuna hizi traffic light sasa badala ya kufungwa kwenye mataa kama Tazara wao wanafunga barabara za watembea kwa miguu, huitaji kuinua macho we tembea umeinamia simu yako bado utaziona taa kwa chini.
)

Tumeachwa MBINGU NA ARDHI jombaaa!!.
 
China na waarabu wapo mbele tangia enzi, cheki great wall of china, angalia arab numeral or name of stars utaelewa
 
Nakubaliana na wewe 100/% Huwa nikiiangalia hii meli kwenye picha ndio huwa naamini jinsi gani tulivyoachwa nyuma. Hii meli, MV Liemba, ililetwa na Mjerumani in 1915 (zaidi ya miaka 100). Yaani miaka miwili kabla ya kushindwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia.

Mpaka leo hii tumeshindwa kupata replacement ya hii meli. Cha ajabu zaidi, MV Liemba bado inatoa huduma mpaka leo. Itatuchukua miaka mingine 500 kabla ya kuwafikia hawa watu.
 
Hakuna mtu duniani anaeweza kukupa teknolojia.

Mzungu kakuweka kwenye dema. Unapowaona wanatangaza "scholarships" mbio mbio mnakimbulia kupeleka "vichwa" vyenu huko, vile vya uhakika wanahakikisha havirudi huku kabisa, labda vije kutembelea ndugu jamaa na marafiki, wiki mbili tu.

Mnafikiri "scholarships" ni msaada ule? Ile ni "investment" inayolipa sana.
 
Huku kwetu ndio kwanza tunawahimuza mjenge vyoo,maana hata vyoo tu hamna.
 
Kumbe mda mwingine unaandika point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…