Ile statement ya lift ndio ilinifanya nielewe kwa nini tunarushiwaga ndizi.Hili ni jibu tosha. Mpaka leo hatuoni umuhimu wa lifti katika majengo yetu, nafikiri wala hatusongi mbele kujaribu kuwafikia, bali tunatokomea kusikojulikana, tunapoteza mwelekeo.
Katika technology wametuzidi, tujifunze kukubali baathi ya mambo, kuna mambo mengine tumewazidi
Kosa kubwa walilofanya hawa wapigania uhuru mimi nawaita wapigaji ( kumfukuza mkoloni na kula wao) wangedai usawa yaani haki sawa ya kushiriki shughuli za uchumi wakawaacha tukashirikiana nao tungekuwa mbali sana
Tukipita njia walizopita wao tutahitaji miaka 500 kufika walipo leo.Tukiwaiga wao walivyofanya kamwe hatuta wafikia,kwani tutakuwa kuwa tunawafuata kwa nyuma.
Solution ni kutafuta njia yetu ya kufuata angalia nchi kama china na nchi za falme za kiarabu.
True wengi wao baada ya uhuru wakawa mabilionea wakiishi kikufuru kifalme ndani ya dhiki ya wengi kwa kuwaibia waafrika kuwafanya wawe masikini kuwauwa waafrika,kuwatendea maovu waafrika wenzao zaidi ya waliovowatendea wakoloni.Hata vita na ufukara Africa ni baada ya uhuru kabla ilikuwa nadra vita vya wenyewe kwa wenyeweHao walikuwa wahuni tu.. Waliona wakoloni wanafaidi wakaona na wao wale!
Kwanini mnapenda kuitolea mfano CHINA? Hivi huwa mnadhana maendeleo ya uchina yamekuja juzi eeh?
China na waarabu wapo mbele tangia enzi, cheki great wall of china, angalia arab numeral or name of stars utaelewa
Nitakufundisha kwan ukitaja teknolojia unataja maendeleo na maendeleo huwa hayachagui halal wala haram kuwa na akili japo kdg