Kuna watu hawataniani bali huumizwa na mafanikio ya hawa wanamuziki...
sababu ni ndogo tuu tabiri za kushindwa kwao...kuna waliotabiri Diamond atafeli akifanikiwa huumia na kuibua yasiyohusika, pia wapo waliotabiri Ally kufeli anapofanikiwa kama hivi huumia na kutafuta pa kujifichia......
Hii ni ishara tosha hata kwenye haya maisha yetu ya kila siku huwa tunatabiriana hivyo yakiwa kinyume ndo hayoo ya kutafuta kichaka,, wahanga ni wengi sana mtu anaweza mchukia na kumtabiria mabaya mwenzake kisa tuu kapita njia asiyoiamini...
kuna watu bila aibu walitumia nguvu nyingi kuikosoa videoza Ally za Mwana na Aje pia wimbo walioshirikiana Saut sol na Ally wakidai Ally kaharibu hajui na mengine mengi wimbo ulipoanza kutamba kwenye chati mbalimbali wakabadili maneno mara kabebwa wengine wakajitia wazimu na kudai ni wimbo wa Saut sol na si wa pamoja, pia wapo waliokosoa wimbo kama wa Nana wa Diamond na Mr.Flavour ama wa Make me sing lakini zilipokuja kubeba tunzo wakaanza hoo kabebwa mara si nyimbo zake na upuuzi kibao.....
hatukatai kuna baadhi ya nyimbo huwa si kali sana kama Lupela ya Ally na Wangu ya Diamond na Dolnard na ni kawaida siku zote huwezi patia mahutaji ya wengi lakini si kila siku maneno mbovumbovu