Kibabage ananikumbusha timu yetu ya darasa Chuo.

Kibabage ananikumbusha timu yetu ya darasa Chuo.

Kibabage anapatwa na kigugumizi akiwa na mpira yaani anakuwa kama kapokea moto mguuni
Anaweka tu kati ana analenga miguu ya mabeki
Hawezi kupiga Cross za juu kabisa .

Nadhani anapaswa atulie mbona zamani alikuwa anacheza vizuri?
Yaani inashangaza, kama Boka mgonjwa Bora acheze Kibwana, kwa sababu hata kama hapandi kushambulia atakupa uhakika wa kukaba, au Faridi Musa, ambaye hata kama hakabi lakini atakupa uhakika wa kushambulia. Huyu dogo hakabi, hachezi, na wala hashambulii. Kwa ufupi akiwa uwanjani ni kama yanga wako 10. Pasi pekee anayopiga kwa uhakika ni ya kuurudisha mpira nyuma
 
Yani wewe ni layman kabisa kwenye mpira alafu uwa mna matusi sana kwa wachezaji. Baka anavuja sana kwa sababu mbili fitness yake imepungua sana na Yanga imekosa link player katikati ndio unaona jana alianzishwa Muda kujaribu kusaidia mipira isipotee hovyo bahati mbaya nae akawa anacheza kama namba 8.
Kosa la Muda nililiona kuanzia dk ya 8 nikamwambia jamaa karibu yangu kuwa hawa jamaa watashika sana kiungo na pembeni kwa sababu mipira hapo kati haikai na Mazembe wanategemea mbio na krosi tu ili wapige vichwa..
 
Benchi la ufundi nalo tatizo kipa aliumia na aliomba sub baadae akata kulazimisha kucheza akiwa mgonjwa wakati benchi yupo kipa mzuri tu niliwashangaa sana wanafanya kazi kwa uoga na si utaalamu..mudhathir alipotea sana alikua anamchosha Aucho na zile sub zilikua sawa ila Musonda angetolewa mapema nae..
Muda aliwekwa attacking mido kwa sababu kocha alikuwa anajaribu kuzuia ugonjwa wa kupoteza mipira hovyo ambao ni ugonjwa unaosumbua pia timu sana kwa sasa. Aziz chama pacome wanapoteza sana mipira wanaipa kazi safu ya uzuiaji timu inaenda inafika katikati mnapoteza mipira kizembe wakati mshazifungua beki zote za pembeni counter paaa goli
 
Sijui walimchelewesha mtu anaonekana hawezi kuendelea na mechi wanalazimisha!

Walituumiza sana ingewezekana hata lile goli wasingefunga, diara hakuwa sawa kabisa yule sijui anaumwa
Diara anacheza huku akiwa mgonjwa na mchezaji alie fit yupo benchi inashangaza sana hata alivyokua anaanzisha mipira kwa miguu ilikua ni hatari hatari tu..
 
Mechi alizocheza yule mkongo si watu walifikia kusema yule mkongo zaidi ya mbio hana jipya. Unajua sababu ni nini? Timu sasa hivi haina kiungo mchezeshaji na kiungo mkabaji wa uhakika. Aziz na Aucho wakiwa kwenye ubora wao kila mchezaji utamuona anawaka.
Kila kitu kinaanzia na defence kwanza na mengine ndiyo yanafuatia.

Angalau hapo kwenye DM ndiyo uongozi unafaa kufanya jambo
Aucho kachoka sana hivi kwanini hata mkude asipangwe? Ana uzoefu mkubwa na uwezo wake pia mzuri tu

Mechi na mamelodi alipewa time zote akazima licha ya kuwa hakucheza muda mrefu naye wamjaribu pia.

Halafu yule Duke hafai kucheza namba 6 bora namba 8 kama jana angalau kidogo ila anajisahau sana back pass nyingi sana .

Tuingie sokoni tu kuchukua DM mkali kweli kweli na Aziz naye ameridhika atafutiwe mwenzake apewe changamoto
 
Muda aliwekwa attacking mido kwa sababu kocha alikuwa anajaribu kuzuia ugonjwa wa kupoteza mipira hovyo ambao ni ugonjwa unaosumbua pia timu sana kwa sasa. Aziz chama pacome wanapoteza sana mipira wanaipa kazi safu ya uzuiaji timu inaenda inafika katikati mnapoteza mipira kizembe wakati mshazifungua beki zote za pembeni counter paaa goli
Kweli na hilo nililiona
Muda kucheza namba 10 ili kuweka mzani sawa yaani muda atakaba na kushambulia poa kucreate nafasi kwa wakati mmoja ..

Aziz hana msaada kabisa team ikiwa inakaba yaani bure kabisa yule
Na ndio maana mazembe wakawa wanapita pembeni kati palikuwa hapapitiki kabisa
 
Diara anacheza huku akiwa mgonjwa na mchezaji alie fit yupo benchi inashangaza sana hata alivyokua anaanzisha mipira kwa miguu ilikua ni hatari hatari tu..
Lakini nadhani sababu ya footwork yake tu ndiyo inawafanya wampange
Ila khomeini alitakiwa kudaka mechi ile sasa kwanini wanalazimisha kumpanga mgonjwa?

Khomeini footwork yake mbona anafundshika tu afunzwe ni kipa mzuri
 
Yaani inashangaza, kama Boka mgonjwa Bora acheze Kibwana, kwa sababu hata kama hapandi kushambulia atakupa uhakika wa kukaba, au Faridi Musa, ambaye hata kama jamani lakini atakupa uhakika wa kushambulia. Huyu dogo hakabi, hachezi, na wala hashambulii. Kwa ufupi akiwa uwanjani ni kama yanga wako 10. Pasi pekee anayopiga kwa uhakika ni ya kuurudisha mpira nyuma
Kibwana ni mzima, sawa Gamondi alikuwa hampendi. Na kocha wa sasa hivi nae anamchukia?

Mfumo wa Yanga unamfanya kibwana asipate namba. Gamondi kuna wakati aliomba aletewe winga wa asilia ili kuziba mapungufu kama anacheza beki aina ya kibwana au timu ikibadili mfumo akaletwa Okra winga anakaa kwenye kibendera kama yule dogo wa simba aliyetoka mtibwa 😂😂

Tatizo la Yanga hamtaki kulipoint kwa sababu ya mahaba
 
Yaani inashangaza, kama Boka mgonjwa Bora acheze Kibwana, kwa sababu hata kama hapandi kushambulia atakupa uhakika wa kukaba, au Faridi Musa, ambaye hata kama hakabi lakini atakupa uhakika wa kushambulia. Huyu dogo hakabi, hachezi, na wala hashambulii. Kwa ufupi akiwa uwanjani ni kama yanga wako 10. Pasi pekee anayopiga kwa uhakika ni ya kuurudisha mpira nyuma
Kama lengo lilikuwa ni kuzuia kibwana alifaa zaidi yeye yupo vizuri kukaba kuliko kushambulia

Sasa strength ya kibabage ni nini? Kushambulia au kudefence? Kote mweupe

Kocha naye bado mgeni hajawajua wachezaji vizuri pia halafu inaonekana kama kina farid na kibwana hawana fitness na hawa waliopo wamechoka yaani yanga tunaelekea pabaya
 
Kibwana ni mzima, sawa Gamondi alikuwa hampendi. Na kocha wa sasa hivi nae anamchukia?

Mfumo wa Yanga unamfanya kibwana asipate namba. Gamondi kuna wakati aliomba aletewe winga wa asilia ili kuziba mapungufu kama anacheza beki aina ya kibwana au timu ikibadili mfumo akaletwa Okra winga anakaa kwenye kibendera kama yule dogo wa simba aliyetoka mtibwa 😂😂

Tatizo la Yanga hamtaki kulipoint kwa sababu ya mahaba
Uongozi wote ulifeli kwenye usajili msimu huu
Low quality player walioleta kama andambwile hana faida yoyote sijui wale kina okrah tukaishia kupata hasara na kina konkoni wale
Huyo boka naye anashinda hospital kuliko uwanjani

At least tushukuru uwepo wa kibabage yupo fit anapohitajika wengine ndiyo hivyo pancha kama huyo mbuni bora lamolisa alikuwa anapatikana game chache lakini sio kama huyu mbuni
 
Yeah Yanga ilifeli kwenye usajili. Kuna wachezaji wametumia energy kubwa sana miwili iliyopita iliitajika refresh ya kikosi kupata wachezaji wenye energy kuliko waliopo hata kama wawili au watatu lakini wawe wana nishati haswa. Ni Duke tu katika wachezaji wapya unaweza kuipata ile energy waliokuwa nayo misimu miwili iliyopita. Wengine wamekuwa abiria.

Mbaya zaidi pia wana madeni mengi huwezi vunja mikataba hovyo so inabidi utafute kina Mwenda waje wajitafute yani unabet.
 
Sisi hatuna wa kumlaumu acha tujipange tu upya
Tuliongelea sana swala la Gamondi kutumia first eleven moja kumbe tulimlaumu bure

Hakuletewa wachezaji sahihi Duke pekee ndiye walipatia kwengine utumbo mtupu
Sasa yanga ni ya kumchukua mwenda kweli? Tena kwa mkopo? Hatuna namna
 
Bacca anacheza namba mbili
Yanga wamtoe kibabage, ni njia ile
Kila upenyo ni kwake
 
Yanga inabidi iongeze morali ya timu na rotation, hasa mechi za ndani

Dube kafunga, ni jambo jema na dube ni mtu sahihi Kwa mfumo wa yanga

Yanga imtoe musonda na baleke, walete winga Moja ya kiwango na kiungo

Kibabage auzwe, watafute LB wa ndani mwingine hasa yule LB wa tabora united

Walete winga wa ndani

Walete CB wa ndani

Yanga tuna nafasi ya ubingwa wa ligi na Bado kimataifa tuna nafasi

Lkn Kwa muda huu tunapaswa tuwe timu sio club
 
Nadhani Leo mumeona upande wa kushoto unavyo oparate angalieni namna Kibwana anacheza halafu fananisheni na kale kajamaa. Yanga Leo wapo 11 timu Ina balance nzuri
 
Back
Top Bottom