Kibaha: Watu wawili waliotoka jela kwa msamaha wauawa

Kibaha: Watu wawili waliotoka jela kwa msamaha wauawa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.

Watu hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 na walipata msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa amesema leo Mei 10, 2021 kuwa watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.

"Hawa watu wametambuliwa ni Ramadhani Mohamed maarufu kwa jina la Seven au Ali (28) mkazi wa kwa Mathiasi na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) mkazi wa mtaa Jamaika, wote walikuwa wamerudi uraiani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais," amesema Nyigesa.

Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameshauri wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna jamaa alikaa jela miaka mitano kwa kesi ya wizi wa kutumia bunduki. Baada ya hio miaka alitoka lakini kesi ikawa haijaisha, ikabaki ile ya bunduki.

Basi jamaa akawa anaenda kusikiliza kesi yake kule mahakama ya mwanzo Ilemela na mimi nikawa namuona pale (nilikuwa sitaki hata mazoea nae).

Jamaa msala wa kwanza ulikuwa umeisha kiaina maana hakuna aliekuwa anafuatilia, msala wa pili ikawa bunduki, nao ulikuwa unaelekea kuisha.

Cha ajabu huyu mwamba alirudi tena mzigoni, akaanza tena kuiba!

Wana nzengo walimkamata mchana kweupe wakapiga sana, alipoulizwa ni wa wapi akasema Igoma (alikamatiwa kisesa), hapo wakaona wampe nafasi awajulishe nduguze kwamba anakufa!

Na ikawa hivyo walimuua mchana kweupe.

Nadhan hawa vijana wanaotoka jela wanapaswa kuwekwa special quarantine kwa ajili ya life skills mpya na kuwekwa sawa kisaikolojia.

Matukio ya kutoka jela na kuuwawa yamekuwa mengi mno.
 
Kuna jamaa alikaa jela miaka mitano kwa kesi ya wizi wa kutumia bunduki. Baada ya hio miaka alitoka lakini kesi ikawa haijaisha, ikabaki ile ya bunduki.

Basi jamaa akawa anaenda kusikiliza kesi yake kule mahakama ya mwanzo Ilemela na mimi nikawa namuona pale (nilikuwa sitaki hata mazoea nae).

Jamaa msala wa kwanza ulikuwa umeisha kiaina maana hakuna aliekuwa anafuatilia, msala wa pili ikawa bunduki, nao ulikuwa unaelekea kuisha.

Cha ajabu huyu mwamba alirudi tena mzigoni, akaanza tena kuiba!

Wana nzengo walimkamata mchana kweupe wakapiga sana, alipoulizwa ni wa wapi akasema Igoma (alikamatiwa kisesa), hapo wakaona wampe nafasi awajulishe nduguze kwamba anakufa!

Na ikawa hivyo walimuua mchana kweupe

Nadhan hawa vijana wanaotoka jela wanapaswa kuwekwa special quarantine kwa ajili ya life skills mpya na kuwekwa sawa kisaikolojia.

Matukio ya kutoka jela na kuuwawa yamekuwa mengi mno
 
Sahihi Bro. Hawa sio watu naona wanakuwa na pepo mchafu. Kuna wengine hata huko gerezani huwa hawataki kutoka yaani wanaona kuwa ni sehemu ya burudani fulani hivi. Jirani yangu alifungwa miezi 6 kwa kosa la udokozi aliporudi uraiani alikuwa kanawiri sana ukilinganisha wakati anapelekwa mahabusu. Wengine wakiachiwa wanaona kama kurudi uraiani kwao ni shida hivyo wanafanya kurudia hayo makosa kusudi warudi gerezani. Counselling nadhani hata kabla ya kuachiwa huwa wanapewa somo kuwa wakirudi uraiani wawe raia wema ila sema tu hawataki kubadilika.Kama zingetumika sheria za uarabuni kosa moja la wizi linaenda na kidole, la pili kiganja.......n.k. Kwao hiyo huwa ni identity kuwa fulani ni mwizi. Katika hali hiyo jamii ikimnyanyapaa lazima ajirekebishe.
 
Back
Top Bottom