Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Kuondoa uhai wa mtu sio jambo jema ila wezi nina hasira nao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Mshana Jr naona Kibaha hawacheki na kimaWatu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.
Watu hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 na walipata msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa amesema leo Mei 10, 2021 kuwa watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.
"Hawa watu wametambuliwa ni Ramadhani Mohamed maarufu kwa jina la Seven au Ali (28) mkazi wa kwa Mathiasi na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) mkazi wa mtaa Jamaika, wote walikuwa wamerudi uraiani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais," amesema Nyigesa.
Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameshauri wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Chanzo: Mwananchi
lulimudanda_jambo lipo kwenye damunafahamu kihehe kidogo wahehe husema LULUMUDANDA ,bila kifo/kuuawa hawaachagi ikishakua lulumudanda
Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Umuhisi si munofu nda,mulakwamila avanu ivoPede uyoo si munu ndaa!! na pewikalibisaa mkaye siwivasaa, ugona miho!!
"A witch will always be a witch" hawajui namna nyingine ya kujipatia riziki mbali na uhalifu. Nadhani jela ndio mahali salama zaidi kwaoWatu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.
Watu hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 na walipata msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa amesema leo Mei 10, 2021 kuwa watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.
"Hawa watu wametambuliwa ni Ramadhani Mohamed maarufu kwa jina la Seven au Ali (28) mkazi wa kwa Mathiasi na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) mkazi wa mtaa Jamaika, wote walikuwa wamerudi uraiani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais," amesema Nyigesa.
Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameshauri wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Chanzo: Mwananchi
Huko jela wanatakiwa watoke na life skills za kuja ku survive mtaani! Ndio maana wanafunzw kufanya productive activitiesKuna jamaa alikaa jela miaka mitano kwa kesi ya wizi wa kutumia bunduki. Baada ya hio miaka alitoka lakini kesi ikawa haijaisha, ikabaki ile ya bunduki.
Basi jamaa akawa anaenda kusikiliza kesi yake kule mahakama ya mwanzo Ilemela na mimi nikawa namuona pale (nilikuwa sitaki hata mazoea nae).
Jamaa msala wa kwanza ulikuwa umeisha kiaina maana hakuna aliekuwa anafuatilia, msala wa pili ikawa bunduki, nao ulikuwa unaelekea kuisha.
Cha ajabu huyu mwamba alirudi tena mzigoni, akaanza tena kuiba!
Wana nzengo walimkamata mchana kweupe wakapiga sana, alipoulizwa ni wa wapi akasema Igoma (alikamatiwa kisesa), hapo wakaona wampe nafasi awajulishe nduguze kwamba anakufa!
Na ikawa hivyo walimuua mchana kweupe.
Nadhan hawa vijana wanaotoka jela wanapaswa kuwekwa special quarantine kwa ajili ya life skills mpya na kuwekwa sawa kisaikolojia.
Matukio ya kutoka jela na kuuwawa yamekuwa mengi mno.
Hahahah nawe umeunga mkono juhudi za wananchi wenye hasira kaliMwizi na mchawi ni binadamu washenzi haina mfanowe[emoji848]
Safi sana wana kibaha
Eeh wazee wa liwezekanalo sasa...lisingoje baadae! Watu wamechafukwa nafsi na haya maisha!Kibaha huko hawataki mzaha,ukijichanganya wananzengo wanamaliza kazi.
Washatungua flat screen nini hapo magetoniKuondoa uhai wa mtu sio jambo jema ila wezi nina hasira nao
Kuna mitaa flani hapo kwa mathias wengi waliojenga ni wanajeshi,wazee wa suti nyeusi aisee pale hua hawacheleweshi.Eeh wazee wa liwezekanalo sasa...lisingoje baadae! Watu wamechafukwa nafsi na haya maisha!
Wanafiki, wakiwa kwenye media wanasema hivyo lakini wakifika kwenye matukio wakaona wezi wanapumua wanaelekeza lawama kwa wananchi kwanini wanafanya kazi nusunusu
Mkuu Shukrani za dhati kwa hili dokezo 'hint'. Sasa nitaenda maeneo hayo kuiba maksudi tu hili nichangamshe na kupasha martial art skills zangu ambazo kwa muda sasa zimepoa.Kuna mitaa flani hapo kwa mathias wengi waliojenga ni wanajeshi,wazee wa suti nyeusi aisee pale hua hawacheleweshi.
Mwizi akijichanganya ni imeisha hioooo.
kweli dawa yao niwananchi wenye hasira Kali basilulimudanda_jambo lipo kwenye damu
Wanauwezo mkubwa kukwepa makosa yao mbele yamahakama nandomana hukmbana na adhabu ndogo ,pia askari mchukua maelezo nae hua anaweza pigwa chenga yamwili kwenye maelezo...."A witch will always be a witch" hawajui namna nyingine ya kujipatia riziki mbali na uhalifu. Nadhani jela ndio mahali salama zaidi kwao
Hahah karibu mkuu,pale watu wanamiliki vyuma vya moto viwili viwili per house.Mkuu Shukrani za dhati kwa hili dokezo 'hint'. Sasa nitaenda maeneo hayo kuiba maksudi tu hili nichangamshe na kupasha martial art skills zangu ambazo kwa muda sasa zimepoa.
Sio mbaya huo ndio msamaha wa wananchiWatu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.