Kibaha: Watu wawili waliotoka jela kwa msamaha wauawa

Wanasema Samia kafanya kazi NGO za nje, ana exposure ya kutosha. Juzi pia kawakoga wazee wa D'Salaam kwamba kasoma nje, na kapanda sana mabasi na wazungu.

Ni wapi huko aliona wanatoa msamaha jumla jumla jela nzima unaachia ma armed robbers, serial killers and child rapists??

Tatizo tunaenda nje hatuigi mambo ya kuendesha nchi, tunaiga jinsi ya kufunga ribbons za zawadi ya benzi kwa Rais mwenye magari mia moja.
 
Kama zingetumika sheria za uarabuni kosa moja la wizi linaenda na kidole, la pili kiganja.......n.k
Hizo naona ni hadithi tu,mbona sijaona au kusikia kwenye vyombo vya habari Sheria hiyo inatekelezwa na nchi yoyote.
 
Jeshi letu la Polisi linapaswa kuteketeza Vijiwe vyote vya Uvutaji na uuzaji wa Bangi ambavyo kimsingi mdio mazalia ya uhalifu wa kila aina.

kufanyike msako maalum seriously tutateketeza kabisa uhalifu mitaani.

Mamlaka zinazo toa mapendekezo ya Misamaha kwa wafungwa iwe makini sana ktk kupendekeza majina ya wanao paswa kupewa msamaha wa Rais. uadilifu na umakini ni muhimu sana wakati wa zoezi.

Mara nyingi tatizo la wezi sugu, vidokozi na wakabaji katika mtaa fulani ni tatizo linaloletwa na Uongozi uliopo madarakani hapo mtaani, hebu tujiulize maswali ya Msingi kabla ya kuamua kuwaua hawa vibaka je hapo mtaani kuna

1, Ulinzi shirikishi? jambo hili ni muhimu kwani vijana wengi mtaani wanajuana tabia na ni kwa majina hivyo ni vigumu sana kwa mgeni kuingia na asijulikane nini anataka kufanya, Mfano nina ndugu watoto wa kike wanasoma na wamepanga uchochoroni ndanindani hapo Manzese wanaweza kurudi saa 3 au 4 usiku lakini wana uhakika wa kufika salama nyumbani kwani wakati wote vijana wapo mtaani

2, Viongozi wamesimamia na kuhamasisha vipi usalama wa raia wake? mfano hapo Kibaha palipotokea tukio hili tumtume Mshana Jr afike kwa mtendaji na Mwenyekiti wa kijiji aulizie ni lini Mtaa/Kijiji kilifanya kikao na wanainchi kuhusu usalama na ulinzi shirikishi? mara nyingi mahali panapotokea mob justice za namna hii sababu kubwa ni wanainchi kuchoka na uongozi ambao hauchukui hatua

3, Wazazi nao huchangia sana kwa malezi mabaya na kufumbia macho utovu wa nidhamu kwa watoto wao, hii huchangiwa na harakati nyingi na nzito kwa wazazi ambazo hupelekea wazazi kutokupata muda wa kukaa na kuongea na familia zao kuhusu malezi bora

4, Uchumi mbovu unaotuzunguka hupelekea watoto wasio na usimamizi mzuri kuingia kwenye magenge ya utovu wa nidhamu, je jamiii tumejiandaa vipi kuwajenga vijana wetu katika elimu ya kujitegemea?

5,Polisi wetu hawashirikishwi na uongozi wa mtaa kuweza kutambua viashiria vya tendo ovu, tujiulize uongozi wa mtaa ni lini waliweza kukaa na wanainchi na kuongelea tatizo la usalama kabla ya mauaji kama haya? labda hili nalo tumwombe Msana Jr atuletee majibu ili tuzidi kuchambua
 
Watu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.

Watu hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 na walipata msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa amesema leo Mei 10, 2021 kuwa watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.

"Hawa watu wametambuliwa ni Ramadhani Mohamed maarufu kwa jina la Seven au Ali (28) mkazi wa kwa Mathiasi na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) mkazi wa mtaa Jamaika, wote walikuwa wamerudi uraiani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais," amesema Nyigesa.

Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameshauri wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Chanzo: Mwananchi
Waliwasamehe mapema mno hawa si walifungwa 2020. Nadhani pia serikali irudi iangalie kama hawa walikidhi vigezo vya msamaha au kuna mtu alinufaika na kupendekeza haya majina.by the way bora wangekosa huo msamaha wangeendelea kuwa hai.
 
Wawe wanafanya hvyo na kwa mafisadi sasa, maana hawa nao wanarudisha maendeleo nyuma
 
Recidivism - the tendency of a convicted criminal to reoffend.
... According to the National Institute of Justice (Marekani), almost 44 percent of the recently released return before the end of their first year out. About 68 percent of 405,000 prisoners released in 30 states in 2005 were arrested for a new crime within three years of their release from prison, and 77 percent were arrested within five years, and by year nine that number reaches 83 percent.

... tafiti hizo ...
 
Wanasema Samia kafanya kazi NGO za nje, ana exposure ya kutosha. Juzi pia kawakoga wazee wa D'Salaam kwamba kasoma nje, na kapanda sana mabasi na wazungu.

Ni wapi huko aliona wanatoa msamaha jumla jumla jela nzima unaachia ma armed robbers, serial killers and child rapists??

Tatizo tunaenda nje hatuigi mambo ya kuendesha nchi, tunaiga jinsi ya kufunga ribbons za zawadi ya benzi!
Ajakosea mbona. Anachofanya ni kupunguza wafungwa magerezan kwa kuwabadirishia adhabu( toka gerezan kwenda kaburini)
 
Kuna jamaa alikaa jela miaka mitano kwa kesi ya wizi wa kutumia bunduki. Baada ya hio miaka alitoka lakini kesi ikawa haijaisha, ikabaki ile ya bunduki.

Basi jamaa akawa anaenda kusikiliza kesi yake kule mahakama ya mwanzo Ilemela na mimi nikawa namuona pale (nilikuwa sitaki hata mazoea nae).

Jamaa msala wa kwanza ulikuwa umeisha kiaina maana hakuna aliekuwa anafuatilia, msala wa pili ikawa bunduki, nao ulikuwa unaelekea kuisha.

Cha ajabu huyu mwamba alirudi tena mzigoni, akaanza tena kuiba!

Wana nzengo walimkamata mchana kweupe wakapiga sana, alipoulizwa ni wa wapi akasema Igoma (alikamatiwa kisesa), hapo wakaona wampe nafasi awajulishe nduguze kwamba anakufa!

Na ikawa hivyo walimuua mchana kweupe.

Nadhan hawa vijana wanaotoka jela wanapaswa kuwekwa special quarantine kwa ajili ya life skills mpya na kuwekwa sawa kisaikolojia.

Matukio ya kutoka jela na kuuwawa yamekuwa mengi mno.
Tatizo wakitoka kule wao wanaona kama wamefuzu diploma ya wizi badala ya kujirekebisha.
Acha wauliwe
 
Wanasema Samia kafanya kazi NGO za nje, ana exposure ya kutosha. Juzi pia kawakoga wazee wa D'Salaam kwamba kasoma nje, na kapanda sana mabasi na wazungu.

Ni wapi huko aliona wanatoa msamaha jumla jumla jela nzima unaachia ma armed robbers, serial killers and child rapists??

Tatizo tunaenda nje hatuigi mambo ya kuendesha nchi, tunaiga jinsi ya kufunga ribbons za zawadi ya benzi kwa Rais mwenye magari mia moja.
Aliyeachia child rapists ni Samia?

Msamaha una kanuni zake, umebakisha mwaka wewe msamaha haukuhusu itakua serial killer na armed robber?
 
Kuna jamaa alikaa jela miaka mitano kwa kesi ya wizi wa kutumia bunduki. Baada ya hio miaka alitoka lakini kesi ikawa haijaisha, ikabaki ile ya bunduki.

Basi jamaa akawa anaenda kusikiliza kesi yake kule mahakama ya mwanzo Ilemela na mimi nikawa namuona pale (nilikuwa sitaki hata mazoea nae).

Jamaa msala wa kwanza ulikuwa umeisha kiaina maana hakuna aliekuwa anafuatilia, msala wa pili ikawa bunduki, nao ulikuwa unaelekea kuisha.

Cha ajabu huyu mwamba alirudi tena mzigoni, akaanza tena kuiba!

Wana nzengo walimkamata mchana kweupe wakapiga sana, alipoulizwa ni wa wapi akasema Igoma (alikamatiwa kisesa), hapo wakaona wampe nafasi awajulishe nduguze kwamba anakufa!

Na ikawa hivyo walimuua mchana kweupe.

Nadhan hawa vijana wanaotoka jela wanapaswa kuwekwa special quarantine kwa ajili ya life skills mpya na kuwekwa sawa kisaikolojia.

Matukio ya kutoka jela na kuuwawa yamekuwa mengi mno.
igoma wanaishi watu wengi hatarishi sijui kwa sababu kunakaliwa sana na wakurya
 
Watu wawili waliotoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameuawa baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali huko kwa Mathiasi mjini, Kibaha mkoani Pwani.

Watu hao walifungwa kwa makosa ya wizi katika kesi ya jinai namba 273/2020 na 260/2020 na walipata msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza mjini Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Wankyo Nyigesa amesema leo Mei 10, 2021 kuwa watu hao wameuawa Mei 8 alfajiri kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo na wananchi wenye hasira waliowatuhumu kuhusika kwenye tukio la wizi.

"Hawa watu wametambuliwa ni Ramadhani Mohamed maarufu kwa jina la Seven au Ali (28) mkazi wa kwa Mathiasi na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) mkazi wa mtaa Jamaika, wote walikuwa wamerudi uraiani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais," amesema Nyigesa.

Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameshauri wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Chanzo: Mwananchi

Polisi wanachangia tabia za wizi mtaani na vitendo vya wananchi kujichukulia madaraka mkononi. Hawana msaada kabisa wanapojulishwa vitendo vya wizi mtaani na hivyo kufanya vijana waendelee kuiba maana wanaona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa. Hii ndio sababu wananchi wanapowakamata wanaona wamalize kabisa
 
Ajakosea mbona. Anachofanya ni kupunguza wafungwa magerezan kwa kuwabadirishia adhabu( toka gerezan kwenda kaburini)
Si wote aliowasamehe wamekamatwa tena waliporudia kosa. Kuna wengine watatoka death row wataenda wataua tena na hawatakamatwa. Haya yanatokea nje ya nchi, hapa ni kwa vile press yetu na record keeping institutions ni mbovu, hakuna anaefuatilia vitu kama hivi.

Kwa wenzetu huwezi kufungulia jela nzima eti msamaha wa Rais. The Magufulis and the Samia Suluhus of the third world hawana exposure masikini ya Mungu, ya jinsi ya ku run a rule-based society.
 
Kwan si kuna vigezo vya msamaha kwa wafungwa? Sio kuwa yeyote tu anaweza tolewa
 
Back
Top Bottom