Mkunde Original
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 807
- 647
- Thread starter
-
- #41
Mkuu watu8 na mimi nimerudia kusoma sijaona popote ambapo Mkunde Original alifanya kosa lililostahili apelekwe kituoni
Hakuna sehem yoyote alisikia tangazo kuwa kuna majambazi yanafukuzwa na polisi so waendesha magari wasiwapishe
Yeye aliwapisha waendesha bajaji hao kama raia mwema sasa huko kuja kuambiwa amewaruhusu eti kupita majambazi sioni hao polisi walikuwa na uhakika gani kama mkunde original alikuwa anawajua kuwa ni majambazi
Mkasa wako waonesha ni namna gani unavyowaogopa askari polisi wakati huo huo ni namna gani hawa jamaa walivyo waonevu...
Nimerudia kusoma mara kadhaa lakini sijaona mahali popote ulipovunja sheria sio tu za barabarani bali za nchi...
Nimejaribu kufikiria kile kifungu cha sheria kinachowatia hatiani wale wote wafanikishao kuwatorosha wahalifu, lakini sioni uhusika wako...
Mwisho pole kwa usumbufu ulioupata...
Niweke interest Mimi sio mwizi/Jambazi. Ila ingetokea ndio nikaweza kuiba Bureau De Change...nikafanikiwa, siwezi tumia usafiri wa Bajaj Never!! Ndio maana nasema sioni uhalisia wa story yako.polisi wetu si unawajua ustaarabu ziro, wanaweza hata kukubambikizia kesi aaah mie na polisi akuu, tena hapo kwenye kufungua kesi itabidi nisome sheria nizijue
Sioni uhallisia wa hii habari yako...!! Over
Mkasa wako waonesha ni namna gani unavyowaogopa askari polisi wakati huo huo ni namna gani hawa jamaa walivyo waonevu...
Nimerudia kusoma mara kadhaa lakini sijaona mahali popote ulipovunja sheria sio tu za barabarani bali za nchi...
Nimejaribu kufikiria kile kifungu cha sheria kinachowatia hatiani wale wote wafanikishao kuwatorosha wahalifu, lakini sioni uhusika wako...
Mwisho pole kwa usumbufu ulioupata...
Hata mimi nimeshaa pia! Coz kusaidia kutoroka mhalifu ni Criminal case inayohitaji Actus reus na Mens rea!
Kumruhusu mtu kupita/kukatiza sio Actus reus kwa sababu sheria za barabarani zinaruhusu hilo! Na wala hakuna Mens rea kwasababu hakuwa na nia ya kutorosha mhalifu! Nawala sio negligence kwa sababu Mkunde hakuwa na duty of care hapo!
...
Hapa wangempeleka huko wangempotezea muda tu, but wangemuachia!
Ooooh my Gosh!! huwa nasikiaga tuu kuwa kuna habari ikisomwa na watu wengi basi kila mtu atapata tafsiri yake, it happens here!!. I didn't mean what you think ila umenifanya nifikirie upande huo pia na nimejikuta nacheka heheheeeee
Jana natoka zangu ofisini jioni hii niko kwenye foleni, dereva kibajaji kaja na abiria wake 3 wanaume kawapakia kwa nyuma.
Akanipigia honi na kunionyesha ishara ya kuomba aingie kwa mbele kwani alikuwa anachepuka kando ya njia na hapo kamuona trafiki so anataka kurudi nia kuu asikamatwe au asipigwe bao.
Mie bana dereva sina roho mbaya nikaita fair play maana kesho naweza kutanua mie nikamuomba kumchomekea atanipisha, hivyo nikampisha magari yaliposogea akaingia njia kuu. Baada ya bajaji kuingia njia kuu akajipenyeza upande wa kushoto yule kaingia mtaani akasepa.
Mie nikaendelea na foleni langu njia kuu maana husband alishanionya kuchepuka barabarani sio tuu nitasababisha ajali bali pia navunja sheria hivo nilitulia.
Sijakaa sawa nawaona voda fasta hawa hapa wakanigongea kioo wakiashiria nifungue kioo nikafungua wakasema mama ongoza gari kituo cha polisi, nikashangaa nimefanya yepi? wakasema umemsaidia yule dreva wa bajaji kutoroka na sie tumeweka foleni ili kuwablock wameiba hela kwenye bureu de change moja ya mhindi heee mie hata sikuwaelewa vizuri nikabaki nawashangaa mara kikaja king'ora na maaskari mama ongoza njia .
Yalitokea kibao huko kituo cha polisi thank God baba mkwe yuko a bit top huko juu ndo nikatoka baada ya mawasiliano kadhaa kufanyika yaani nilichoka kabisa na tukio lililonikuta khaaaa!
Je ningekuwa sina ninayemjua huko juu si ungekuta niko segerea.... naenda kwenye debe daaaah hadi sasa nawaza sipati jibu.
Hakiamama ukikutana na mimi barabarani usiniombe kunichomekea wala sikupishi aiseee.., be aware mtu usiyemjua anaweza kukuletea matatizo.
Nshawah kumgonga mtu makusudi kwa kunichomekea bila ruhusa yangu.
Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
Watu wa michepuko wanapitaga sana njia za wapita miguu na hawaogopagi faini.Bora sisi waenda kwa miguu!:msela:
Yaani ilikuwa kama muvi vile ila ndo ivo thanks God nilirudi home salama