Kibajaji kimeniponza...

Kibajaji kimeniponza...

Mkuu watu8 na mimi nimerudia kusoma sijaona popote ambapo Mkunde Original alifanya kosa lililostahili apelekwe kituoni
Hakuna sehem yoyote alisikia tangazo kuwa kuna majambazi yanafukuzwa na polisi so waendesha magari wasiwapishe
Yeye aliwapisha waendesha bajaji hao kama raia mwema sasa huko kuja kuambiwa amewaruhusu eti kupita majambazi sioni hao polisi walikuwa na uhakika gani kama mkunde original alikuwa anawajua kuwa ni majambazi

Yaani ilikuwa kama muvi vile ila ndo ivo thanks God nilirudi home salama
 
Mkasa wako waonesha ni namna gani unavyowaogopa askari polisi wakati huo huo ni namna gani hawa jamaa walivyo waonevu...

Nimerudia kusoma mara kadhaa lakini sijaona mahali popote ulipovunja sheria sio tu za barabarani bali za nchi...

Nimejaribu kufikiria kile kifungu cha sheria kinachowatia hatiani wale wote wafanikishao kuwatorosha wahalifu, lakini sioni uhusika wako...

Mwisho pole kwa usumbufu ulioupata...

asante kwa kweli nilipata usumbufu mkubwa mnoo
 
polisi wetu si unawajua ustaarabu ziro, wanaweza hata kukubambikizia kesi aaah mie na polisi akuu, tena hapo kwenye kufungua kesi itabidi nisome sheria nizijue
Niweke interest Mimi sio mwizi/Jambazi. Ila ingetokea ndio nikaweza kuiba Bureau De Change...nikafanikiwa, siwezi tumia usafiri wa Bajaj Never!! Ndio maana nasema sioni uhalisia wa story yako.
 
Mie mwenyewe nimechoka aise, kumbe hizi fair play tunazozitoa barabarani sometimes unaweza kutorosha muhalifu, sikuwa najua hili

Pole Mkunde Original though naona polisi walikuwa na lao jambo


Mkasa wako waonesha ni namna gani unavyowaogopa askari polisi wakati huo huo ni namna gani hawa jamaa walivyo waonevu...

Nimerudia kusoma mara kadhaa lakini sijaona mahali popote ulipovunja sheria sio tu za barabarani bali za nchi...

Nimejaribu kufikiria kile kifungu cha sheria kinachowatia hatiani wale wote wafanikishao kuwatorosha wahalifu, lakini sioni uhusika wako...

Mwisho pole kwa usumbufu ulioupata...
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi nimeshaa pia! Coz kusaidia kutoroka mhalifu ni Criminal case inayohitaji Actus reus na Mens rea!
Kumruhusu mtu kupita/kukatiza sio Actus reus kwa sababu sheria za barabarani zinaruhusu hilo! Na wala hakuna Mens rea kwasababu hakuwa na nia ya kutorosha mhalifu! Nawala sio negligence kwa sababu Mkunde hakuwa na duty of care hapo!
...
Hapa wangempeleka huko wangempotezea muda tu, but wangemuachia!


Mkuu Mashaxizo unasoma LLB nini maana naona mzee actus reus na mens rea zinakushuka tuu
Karibu kwenye fani mkuu
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa mantiki ya wewe kukamatwa eti kwa kosa la kupisha Bajaji kwamba umesaidia wezi kutoroka....

Kwani mlipewa taarifa awali kuwa msipishe watu wapite?
 
Ooooh my Gosh!! huwa nasikiaga tuu kuwa kuna habari ikisomwa na watu wengi basi kila mtu atapata tafsiri yake, it happens here!!. I didn't mean what you think ila umenifanya nifikirie upande huo pia na nimejikuta nacheka heheheeeee

hahaa basi mie nilivosoma nikahisi labda umemaanisha hivo....
 
Jana natoka zangu ofisini jioni hii niko kwenye foleni, dereva kibajaji kaja na abiria wake 3 wanaume kawapakia kwa nyuma.

Akanipigia honi na kunionyesha ishara ya kuomba aingie kwa mbele kwani alikuwa anachepuka kando ya njia na hapo kamuona trafiki so anataka kurudi nia kuu asikamatwe au asipigwe bao.

Mie bana dereva sina roho mbaya nikaita fair play maana kesho naweza kutanua mie nikamuomba kumchomekea atanipisha, hivyo nikampisha magari yaliposogea akaingia njia kuu. Baada ya bajaji kuingia njia kuu akajipenyeza upande wa kushoto yule kaingia mtaani akasepa.

Mie nikaendelea na foleni langu njia kuu maana husband alishanionya kuchepuka barabarani sio tuu nitasababisha ajali bali pia navunja sheria hivo nilitulia.
Sijakaa sawa nawaona voda fasta hawa hapa wakanigongea kioo wakiashiria nifungue kioo nikafungua wakasema mama ongoza gari kituo cha polisi, nikashangaa nimefanya yepi? wakasema umemsaidia yule dreva wa bajaji kutoroka na sie tumeweka foleni ili kuwablock wameiba hela kwenye bureu de change moja ya mhindi heee mie hata sikuwaelewa vizuri nikabaki nawashangaa mara kikaja king'ora na maaskari mama ongoza njia .

Yalitokea kibao huko kituo cha polisi thank God baba mkwe yuko a bit top huko juu ndo nikatoka baada ya mawasiliano kadhaa kufanyika yaani nilichoka kabisa na tukio lililonikuta khaaaa!

Je ningekuwa sina ninayemjua huko juu si ungekuta niko segerea.... naenda kwenye debe daaaah hadi sasa nawaza sipati jibu.

Hakiamama ukikutana na mimi barabarani usiniombe kunichomekea wala sikupishi aiseee.., be aware mtu usiyemjua anaweza kukuletea matatizo.

ya mungu mengi
tenda wema nenda zako
lets assume usingempisha afu hao waporaji wana silaha za moto...unadungunyuliwa la kipanda uso afu still wanapita..:evil:
 
Nshawah kumgonga mtu makusudi kwa kunichomekea bila ruhusa yangu.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk

yani avata🙂r yako..jina lako...na comment zako....zinafanana kama machungwa..lol
 
Ukweli wa habari nauona na ikizingatia police wetu walivyo wababe na elimu zao za kusindikiza darasani sina budi kukupa pole kwa kadhia iliyokupata. Ila vp uliwauliza kama hiyo bajaji iliandikwa....SISI NI MAJAMBAZI TUNAWAKIMBIA POLICE??????????????? naamini hapo ungekuwa msitu wa pande japo swali linajieleza.
 
Uchunguzi usio rasmi unaonesha zaidi ya asilimia 60 ya askari waishio Dar ni wezi...walikushika wewe ili wezi wenzao (whether raia au askari wenzao) watoroke kiurahisi.. #myTHOUGHT

On the other hand Mkunde Original pamoja na kukana sana..mimi nahisi huu 'mchepuko wa bajaji' ni jambo lingine kabisaaa!!!
 
Last edited by a moderator:
Hivi hao wezi wapo kwenye kibajaji polisi walikosa hata bodaboda ya kuikimbiza au pikipiki yao ya kawaida kuikimbiza hiyo bajaji maana bajaji seed mwisho 80km/h it doesnt make sense hao polisi walikuwa na lao jambo...
 
Back
Top Bottom