Kibajaji kimeniponza...

Kibajaji kimeniponza...

Mkunde Original

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2013
Posts
807
Reaction score
647
Jana natoka zangu ofisini jioni hii niko kwenye foleni, dereva kibajaji kaja na abiria wake 3 wanaume kawapakia kwa nyuma.

Akanipigia honi na kunionyesha ishara ya kuomba aingie kwa mbele kwani alikuwa anachepuka kando ya njia na hapo kamuona trafiki so anataka kurudi nia kuu asikamatwe au asipigwe bao.

Mie bana dereva sina roho mbaya nikaita fair play maana kesho naweza kutanua mie nikamuomba kumchomekea atanipisha, hivyo nikampisha magari yaliposogea akaingia njia kuu. Baada ya bajaji kuingia njia kuu akajipenyeza upande wa kushoto yule kaingia mtaani akasepa.

Mie nikaendelea na foleni langu njia kuu maana husband alishanionya kuchepuka barabarani sio tuu nitasababisha ajali bali pia navunja sheria hivo nilitulia.
Sijakaa sawa nawaona voda fasta hawa hapa wakanigongea kioo wakiashiria nifungue kioo nikafungua wakasema mama ongoza gari kituo cha polisi, nikashangaa nimefanya yepi? wakasema umemsaidia yule dreva wa bajaji kutoroka na sie tumeweka foleni ili kuwablock wameiba hela kwenye bureu de change moja ya mhindi heee mie hata sikuwaelewa vizuri nikabaki nawashangaa mara kikaja king'ora na maaskari mama ongoza njia .

Yalitokea kibao huko kituo cha polisi thank God baba mkwe yuko a bit top huko juu ndo nikatoka baada ya mawasiliano kadhaa kufanyika yaani nilichoka kabisa na tukio lililonikuta khaaaa!

Je ningekuwa sina ninayemjua huko juu si ungekuta niko segerea.... naenda kwenye debe daaaah hadi sasa nawaza sipati jibu.

Hakiamama ukikutana na mimi barabarani usiniombe kunichomekea wala sikupishi aiseee.., be aware mtu usiyemjua anaweza kukuletea matatizo.
 
Mkasa wako waonesha ni namna gani unavyowaogopa askari polisi wakati huo huo ni namna gani hawa jamaa walivyo waonevu...

Nimerudia kusoma mara kadhaa lakini sijaona mahali popote ulipovunja sheria sio tu za barabarani bali za nchi...

Nimejaribu kufikiria kile kifungu cha sheria kinachowatia hatiani wale wote wafanikishao kuwatorosha wahalifu, lakini sioni uhusika wako...

Mwisho pole kwa usumbufu ulioupata...
 
Mkuu watu8 na mimi nimerudia kusoma sijaona popote ambapo Mkunde Original alifanya kosa lililostahili apelekwe kituoni
Hakuna sehem yoyote alisikia tangazo kuwa kuna majambazi yanafukuzwa na polisi so waendesha magari wasiwapishe
Yeye aliwapisha waendesha bajaji hao kama raia mwema sasa huko kuja kuambiwa amewaruhusu eti kupita majambazi sioni hao polisi walikuwa na uhakika gani kama mkunde original alikuwa anawajua kuwa ni majambazi
 
Last edited by a moderator:
Pole kwa yaliyokukuta
Asante, kwa kutusaidia na sisi wengine, tumepata fundisho juu ya tatizo lako
 
mimi hao polisi wasingekuwa na uwezo wa kunifanya chochote, zaidi ya yote hata huko kuongoza gari kwenda kituoni nisingeenda, ningewasha gari hadi home kama wananifuata wangekuja wakinifuata na king'ora chao wanikamatie home halafu waniambie kosa lao ni lipi. chochote ambacho wangenifanya either kunifungulia mashitaka /ambayo hapo naona kama hayapo, ningekuja kuifungulia serikali kesi ya madai hadi ningejenga gorofa. shenzitaipu polisi.
 
watu8 kamaliza hapo juu acha uoga! Mimi nina watu wako juu sana kwenye hilo jeshi lao la polisi lakini ishu zangu huwa nazimaliza kwa kukomaa nao. Ukitaka kuwaweza unatakiwa kuwa mbishi sometimes.
 
Last edited by a moderator:
Jana natoka zangu ofisini jioni hii niko kwenye foleni, dereva kibajaji kaja na abiria wake 3 wanaume kawapakia kwa nyuma. Akanipigia honi na kunionyesha ishara ya kuomba aingie kwa mbele kwani alikuwa anachepuka kando ya njia na hapo kamuona trafiki so anataka kurudi nia kuu asikamatwe au asipigwe bao. Mie bana dereva sina roho mbaya nikaita fair play maana kesho naweza kutanua mie nikamuomba kumchomekea atanipisha, hivyo nikampisha magari yaliposogea akaingia njia kuu. Baada ya bajaji kuingia njia kuu akajipenyeza upande wa kushoto yule kaingia mtaani akasepa. Mie nikaendelea na foleni langu njia kuu maana husband alishanionya kuchepuka barabarani sio tuu nitasababisha ajali bali pia navunja sheria hivo nilitulia.
Sijakaa sawa nawaona voda fasta hawa hapa wakanigongea kioo wakiashiria nifungue kioo nikafungua wakasema mama ongoza gari kituo cha polisi, nikashangaa nimefanya yepi? wakasema umemsaidia yule dreva wa bajaji kutoroka na sie tumeweka foleni ili kuwablock wameiba hela kwenye bureu de change moja ya mhindi heee mie hata sikuwaelewa vizuri nikabaki nawashangaa mara kikaja king'ora na maaskari mama ongoza njia .........
Yalitokea kibao huko kituo cha polisi thank God baba mkwe yuko a bit top huko juu ndo nikatoka baada ya mawasiliano kadhaa kufanyika yaani nilichoka kabisa na tukio lililonikuta khaaaa!!!!!
Je ningekuwa sina ninayemjua huko juu si ungekuta niko segerea.... naenda kwenye debe daaaah hadi sasa nawaza sipati jibu.
Hakiamama ukikutana na mimi barabarani usiniombe kunichomekea wala sikupishi aiseee.., be aware mtu usiyemjua anaweza kukuletea matatizo.
Jioni njema wote.

mmhh.. Mkunde Original! mimi Excel napinga kabisa hoja!

hii ni habari picha..

haukuwa barabarani wala nini! umetuletea tu ujumbe kwamba tuache nanii!

ceteris paribus nimekuelewa!
 
Last edited by a moderator:
Unyee debe kwani kosa lako liko wapi? ulishindwa kuwaambia kwamba wewe umempisha tu hilo la kuwakamata ni jukumu lao
 
Ahsante kwa kutujurisha kuwa Una ndugu mkubwa kwenye vyombo vikubwa vya dola hapa Nchini....
 
Mkuu watu8 na mimi nimerudia kusoma sijaona popote ambapo Mkunde Original alifanya kosa lililostahili apelekwe kituoni
Hakuna sehem yoyote alisikia tangazo kuwa kuna majambazi yanafukuzwa na polisi so waendesha magari wasiwapishe
Yeye aliwapisha waendesha bajaji hao kama raia mwema sasa huko kuja kuambiwa amewaruhusu eti kupita majambazi sioni hao polisi walikuwa na uhakika gani kama mkunde original alikuwa anawajua kuwa ni majambazi

Hata mimi nimeshaa pia! Coz kusaidia kutoroka mhalifu ni Criminal case inayohitaji Actus reus na Mens rea!
Kumruhusu mtu kupita/kukatiza sio Actus reus kwa sababu sheria za barabarani zinaruhusu hilo! Na wala hakuna Mens rea kwasababu hakuwa na nia ya kutorosha mhalifu! Nawala sio negligence kwa sababu Mkunde hakuwa na duty of care hapo!
...
Hapa wangempeleka huko wangempotezea muda tu, but wangemuachia!
 
Last edited by a moderator:
mimi hao polisi wasingekuwa na uwezo wa kunifanya chochote, zaidi ya yote hata huko kuongoza gari kwenda kituoni nisingeenda, ningewasha gari hadi home kama wananifuata wangekuja wakinifuata na king'ora chao wanikamatie home halafu waniambie kosa lao ni lipi. chochote ambacho wangenifanya either kunifungulia mashitaka /ambayo hapo naona kama hayapo, ningekuja kuifungulia serikali kesi ya madai hadi ningejenga gorofa. shenzitaipu polisi.

Pamoja kwenye hiloo.
 
Back
Top Bottom