View attachment 1867792
Sijui huyu Bi. Mkubwa wetu anajisikiaje akiona vitu kama hivi mtandaoni! Leo anaitwa dikteta wa kike.
Maana kwa mujibu wake yeye mwenyewe, huwa anajivinjari humu mitandaoni ili kujua yaliyomo vichwani mwa wananchi.
Tulio wahalisia wa mambo na tulio na uzoefu wa kufuatilia siasa za kitaifa na kimataifa, kwa kutumia uzoefu wetu huo, tulijua tu kuwa haitochukua muda kwa zile sifa alizokuwa anapewa kugeuka kuwa lawama.
Yaani alikuwa hadi anapewa sifa za uongo [mfano ni kuongea Kiingereza kizuri kilichonyooka. Ukweli ni kwamba Kiingereza chake si kizuri na hakijanyooka. Hana tu lafudhi nzito].
Kuna sehemu niliona watu wakimuita eti ni ‘genius’ kwa vile tu alikuwa anaongea kiupole bila kufokea na alivyosema watu wasibambikiwe kesi!
Hizo ndo standard za baadhi ya Watanzania [emoji1787].
No wonder tupo kwenye hali tuliyonayo.