Tetesi: Kibarua cha CAG kuota nyasi

VIVIANET

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,129
Reaction score
2,918
Ndugu zangu mabibi na mabwana hakuna kichwa cha habari ambacho kingefaa ziaid ya hicho nilichochagua. Naomba usinihukumu kabla ya kusoma habari yote.

Hakuna aliyewahi kuikosoa serikali ya awamu ya tano na bunge hili la sasa akabaki salama. CAG amejiingiza kwenye msitu wenye giza nene ambao hatoweza kutoka salama.

Kama ni mfuatiliaji wa masuala mbalimbali hapa nchini utagundua kuwa kibarua cha CAG tayari kimeota mbawa.

Kauli za Ndugai siyo za bure kuna mpango na mkakati ambao umeshasukukwa kumuondoa, maana CAG amesema bunge ni dhaifu kwa kushindwa kusimamia serikali hii inayofanya mambo mengi bila idhini ya bunge.

Kununua ndege, Ujenzi wa kiwanja Chato, Ununuaji wa korosho nk bila bunge kujadili na kupitisha bajeti. Kwa maana nyingine CAG kusema bunge ni dhaifu amekosoa utendaji wa serikali pia.

Nawahakikishia CAG atotumbuliwa mapema January hii au mwanzoni mwa February.

Mh Ndugai asidanganye watanzania kuwa bunge lake lipo imara kuisimamia serikali, ebu awaambie wananchi ni lini bunge limewahi kujadili ununuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja Chato, ununuzi wa korosho kwa pesa za umma?

Serikali ya awamu ya tano ikikusudia kufanya lolote bunge la Ndugai linasema ndiyooooo, ni aibu sana kuwa na bunge butuuuu kama hili
 

Bunge la ndugai ndilo bunge dhaifu mno tangu tupate Uhuru. CAG yupo sahihi kabisa. Na hakujawahi kutokea spika dhaifu kama ndugai katika historia ya bunge la Tanzania.
 
Peleka Ujinga wako huko! Umekaa kiumbea Sana. Nenda kasome ujiridhishe Kama CAG anatumbuliwa Kama vihiyo wenzako huko CCM! Assad is there to stay until 2021! Pasukeni, jichomeni vidole kwenye vinyeo vyenu, Hakuna wa Kumtumbua Assad, so better swallow your bitter pills!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge la ndugai ndilo bunge dhaifu mno tangu tupate Uhuru. CAG yupo sahihi kabisa. Na hakujawahi kutokea spika dhaifu kama ndugai katika historia ya bunge la Tanzania.
Mwenye udhaifu aweza kupona,huyu hafai kabisa. Mboga zilizochacha waeza kuzila tena? Hata ukizipasha moto,utajifariji kwakuwa huna kiweo kingine lakini lazima uharishe sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umeweka akiba ya Uzi kabisa ili akiliwa kichwa uje kukumbushia uzi
 
Siyo rahisi Kama unavyofikria CAG anaweza tumbuliwa Soma katiba vizuri utajua ni njia ipi CAG anaweza tumbuliwa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No hicho nilichoandika ndicho kinaenda kutokea, kwa hiyo sidhani kama nitabadilisha. subiri muda siku chache zijazo utashangaa
Rais hana uwezo wa kumtoa CAG madarakani kwa mujibu wa sheria.

Ila kinachoweza kufanyika ni kumlazimisha kupitia mlango wa nyuma ili CAG ajiuzulu mwenyewe au wajifanye wanampa appointment na kumfanya Balozi somewhere ......... then anatumbuliwa kama alivyofanyiwa yule wa Canada!!

Awamu hii anything is possible ...!!
 
Ungeandika "huenda" labda
Maisha kila mahali na kutakucha tu so what
Kila mmoja anasimamia anachokiamini labda mnafiki tu

Sent from my SM using Tapatalk
 
Kama ni kweli basi atatoka kwa heshima kubwa na tutamkosa mtu ambaye ni mkweli na muadilifu.
Yeye binafsi hatopata hasara ili kama nchi, itakuwa imepoteza raslimali kubwa sana.
Waswahili wanamsemo 'Chema chajiuza, kibaya kinajitembeza'
 
Mlivyoambiwa ELIMU ELIMU ELIMU sijui kama mlielewa

Unaujua utaratibu wa kumfuta kazi CAG?
 
Sijaelewa neno "atotumbuliwa" lina maana gani kama ulivyolitumia kwenye bandiko hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…