Ndugu zangu mabibi na mabwana hakuna kichwa cha habari ambacho kingefaa ziaid ya hicho nilichochagua. Naomba usinihukumu kabla ya kusoma habari yote.
Hakuna aliyewahi kuikosoa serikali ya awamu ya tano na bunge hili la sasa akabaki salama. CAG amejiingiza kwenye msitu wenye giza nene ambao hatoweza kutoka salama.
Kama ni mfuatiliaji wa masuala mbalimbali hapa nchini utagundua kuwa kibarua cha CAG tayari kimeota mbawa.
Kauli za Ndugai siyo za bure kuna mpango na mkakati ambao umeshasukukwa kumuondoa, maana CAG amesema bunge ni dhaifu kwa kushindwa kusimamia serikali hii inayofanya mambo mengi bila idhini ya bunge.
Kununua ndege, Ujenzi wa kiwanja Chato, Ununuaji wa korosho nk bila bunge kujadili na kupitisha bajeti. Kwa maana nyingine CAG kusema bunge ni dhaifu amekosoa utendaji wa serikali pia.
Nawahakikishia CAG atotumbuliwa mapema January hii au mwanzoni mwa February.
Mh Ndugai asidanganye watanzania kuwa bunge lake lipo imara kuisimamia serikali, ebu awaambie wananchi ni lini bunge limewahi kujadili ununuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja Chato, ununuzi wa korosho kwa pesa za umma?
Serikali ya awamu ya tano ikikusudia kufanya lolote bunge la Ndugai linasema ndiyooooo, ni aibu sana kuwa na bunge butuuuu kama hili