Kibatala ana ushaidi kuwa aliyetekwa ni Humphrey Polepole au ameamua kutimiza wajibu tu?

Kibatala ana ushaidi kuwa aliyetekwa ni Humphrey Polepole au ameamua kutimiza wajibu tu?

Sawa, call it kijinga...lakini mimi siamini unachoamini wewe, narudia tena WASITHUBUTU HATA KUJARIBU KUMUUA POLEPOLE... mwisho wa kunukuu.

Sasa ita tena kwamba ni maneno matupu.
Kuamini si hoja.

Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Kuna mtu aliruka ghorofani juu sana hapo Morogoro Road, chini aliweka Simtank la maji.

Aliamini atapona kwa kuangukia lile Simtank.

Alikufa.

Ile imani yake kwamba Simtank la maji litamsaidia, haikumsaidia kitu.

Huyo Polepole mwenyewe aliamini Mungu wa mbinguni atamlinda.

Lakini katekwa kijinga tu.

Huelewi nini?
 
Mzunguko wooote huo wa nini kutafuta ushahidi? Kitu ni tit for tat reaalistic mambo yanaisha. Sheria kitu gani wakati unaona na inaeleweka vema ni fulani
Anayefanya hayo sio mwanaharakati ni mwanasheria hivyo lazima atoe jazba, hisia na anatakiwa awe mtulivu afanye vitu kisheria
 
Hivi polisi wamefika kwenye crime scene? Sijasikia popote hili suala .

Au siku hizi Tz tukio kama hilo likitokea Polisi hawaendi eneo husika. Nani anatakiwa kuthibitisha ile damu ni ya polepole kati ya polisi na upande wa familia? Seriously polisi wanajificha kwenye kichaka cha “Hatuna taarifa kama HP alikuwa Tz” Sawa, Zile damu ni za nani? ni kithibitisho cha kwanza cha kufahamu ni binadamu gani alipigwa katika ile nyumba akaacha zile damu.

Aiseee nchi imekuwaje!? Mbona kila kitu kinaenda kinyume nyume.
 
Back
Top Bottom