Kibatala wewe ni wakili mzuri na msomi lakini punguza majivuno na dharau dhidi ya mamlaka

UWT akili zenu hazina akili, hapo kosa ni nini sasa?
 
Mimi ni mwanaCCM ila sioni tatizo hapo kuhusu Kibatala. Tunahitaji mawakili kama Kibatala wa kutosha... hao unaowataja kama seniors ni waoga kinyama. Sugu kwenye kitabu chake alisema Prof Mgongofimbo alijitoa ghafla kwenye kesi aliyotaka kufungua kuhusu dili lake alilonyang'anywa na Ruge. Hata Shigongo naye alishalalamika kuhusu hilo. Hao seniors wengi hawana amshaamsha kama Kibatala.
 
Kitabala na Lissu wanaitendea haki tasinia ya sheria
 
ila nikikumbuka kesi ya marehemu Aneth Msuya basi tuu
 
Acha Kibatala afanye kazi yake.
Umesema amekushawishi nawe kusoma sheria,unaonaje ukaenda kuwa wakili wa serikali ili upambane na Kibatala kwenye kesi hiyo??

Lazima watu wafundwe tena kuhusu PGO hakuna porojo kwenye mambo ya msingi yanayohusu maisha ya watu.
Mleta mada usikose siku za kesi hapo Kisutu)))
 
Kesi ya mke wa Msuya ilikuwa ni ndogo?
Kuna watoto wadogo wanafungua kesi mahakama ya Afrika na wanaishinda serikali ila sijaona wakijitapa...

Kuna mawakili walienda kupambania mali za nchi huko duniani na walipambana na mawakili wa kueleweka ila sijawahi kuona mbwembwe zao...

Huyu ndugu yenu ana Ego iliyozidi.
 
Na wewe si ukafungue ya kwako, acha jamaa atambe sasababu ndiyo inampa maisha town hajawahi kuwa mjinga kama wana CCM wenzako.
 
Hakuna dharau wala kebehi hapo wewe ni mjinga tu hujui haki za raia na wajibu wa mwanasheria.

Kama tuna tatizo Tanzania basi tatizo hilo ni kwamba wanasheria wetu si wakali vya kutosha, hawana kebehi za kutosha, hawana dharau za kutosha.
kwel kabisa ukisikiliza mawakili wa nchi za watu wakati wakiwahoji mashaidi hasa us ndo utajua kuwa wanasheria wanatakiwa kuwa katili, wakali, wenye dharau, kebehi, kejeli, maneno ya shombo, wasicheke na kima, huwa najiuliza wale wanasheria wa kujitegemea wa us wakija huku kwetu, si wanasheria wa serikali watakuwa wanakimbia kesi.
 
Hzo kesi walizoenda kupambania huko duniani walishinda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…