Jamani haya mambo hapa kwetu si ya kushangaza, kweli, inawezekana ni ufuska wa wanaume na pia inawezekana ni uwasha-washa wa hako katoto na pia kuna uwezekano mkubwa wa mazingira anayokulia hapo nyumbani.
Sasa hivi, limekuwa jambo la kawaida kabisa kukuta mama ana watoto nyumbani nae hashikiki, anaingiza akitoa wanaume nyumbani bila ya hesabu. Jee, mtoto anaekulia mazingira hayo, naye aweje? Hakuna cha kumzuwia, ni ngono kwa kwenda mbele.
Mambo mengi hupelekea watoto kuelekea kwenye ufuska, ikiwepo dhiki, umaskini, ukosefu wa maadili kwa wazazi na kwa wachache sana, kufatana na makundi yasiyo na maadili mema.
Zamani mtoto akikosa, mtu mzima yeyote, hata si mzazi wake ni mpita njia tu, alikuwa akiweza kumkanya na hata kumtandika. Thubutu, dunia ya sasa, ukijaribu kumkanya mtoto wa watu anaweza kukuchamba asikubakishe. Maadili kwisha.
Tuwaombee watoto zetu na wa-wenzetu, yasiwakute mabalaa ya dunia. Tuwaombee wawe watoto wenye kheri. Na sisi wazazi ndio tuwe wa kwanza kuwaonesha mifano bora.