Kiboko ya Wachawi aonekana DR Congo, awatambishia Watanzania kuwa anakula maisha. Asema amemisi zile laki tano za kiingilio

Kiboko ya Wachawi aonekana DR Congo, awatambishia Watanzania kuwa anakula maisha. Asema amemisi zile laki tano za kiingilio

Hivi karibuni kuna clip zinasambaa zikimuonyesha aliyekua akijiita Nabii Kiboko ya Wachawi akijigamba kuwapiga waumini wake alipokua Tanzania. Ameonyesha pia mjengo wake unaoendelea na ujenzi huku akisema ame-miss zile laki tano za watanzania za viingilio. Anazungumza maneno ya kejeli kama kuwaita waumini wendawazimu na kusema maneno kama "mtajua hamjui."

Wale mnaodandia makanisa kutafuta miujiza, mjifunze kitu hapa. Hizi ni fedheha kwa waliokua waumini wa Kiboko ya wachawi.
 
Kuna watu naamini kuna watu bado watakuwa wanamtetea😂
 
Mimi hizi mambo hata siamini ni dada yangu alikuja kutoka arusha kafikia kwangu akiwa na majanga yake akesema anaenda kwa nabii kiboko ya wachawi huko buza, ndo atasaidika nilimkataza akaniambia mimi saivi ni mtoto wa shetani na atanisema kote kwenye ukoo na maombi juu nikaombewa nakwambia tv ilikuwa ni mwamposa mda wote nk:
Kesha logwa uyo hao wengi wanabii wanakua wachawi kuvuta watu kifikra kupitia Tv unajua tu hv vitu brainwashed through tv ndo yote haya. Km yule mgawa keki ni ku brain wash watu yale yale ya tb joshua
 
Yule mshenzi alimpiga dada yangu laki 5 hivi hivi daaah inauma sana
Nilijaribu kuelimisha watu kwa hawa matapeli, lakini ni vigumu kuwatoa waTZ toka mikononi mwa hawa Matapeli.
Ukiachana na matapeli WaTz. wako waNigeria, wakongo, warundi n.k.
Tuendelee kuwaombea duaa wenzetu waliokumbana na majaribu haya. Nguvu ya serikali peke yake haitoshi, kwa vile suala la imani ni suala huru.
 
Huyu jamaa sheria isimuache. Jeshi la polisi huyu kahujumu uchumi, atafutwe na interpol

Ushauri afungwe gereza za bongo
Afungwe kwa kosa gani? Mukimfunga huyu na mkamwacha mwamposa dunia itawashangaa, maana wote ni matapeli,na utapeli wao una baraka za serikali, wajinga hawaishi,ni kama tu ngombe,kila siku tunakula nyama kwa sababu ngombe za kuchinja hazijawahi kupungua machinjioni.
 
Mimi simfahamu kiboko ya wanga, lakini napenda kufahamu, "Serikali haina dini", Sasa inafahamuje kama imani fulani ni fake au ipi Sio fake? Au sadaka ipi ikitolewa kwenye dhehebu fulani, ipi ni halali na ipi ni utapeli? Kama mtu kaenda kwenye dhehebu lolote na kutoa sadaka kwa hiyari, hajalaziishwa, kwanini serikali iingilie? Kama yeye anapambana na wachawi nao wachawi Wanatakiwa wapambane na wao kwenye ulimwengu wa roho, sio watetewe na serikali 🤔
500,000 ndio kilikuwa kiingilio cha kumuona. Ukifanya hivi maana yake unafanya biashara (unatakiwa ulipe kodi). Umekiuka sherti la kuifanya usajili wa jumuiya yako kama ya kidini. Hilo ni moja tu, yapo mengi
 
Back
Top Bottom