Kibongo bongo madirisha ni lazima yawe na grills

Hata ulaya wanaweka grill , ukiacha commercial buildings
Ulaya ni nchi zilizo upande wa mashariki, huko ni eneo lenye nchi nyingi zenye uchumi mdogo. Hayo maeneo yana viwango vikubwa sana vya uhalifu ambavyo kitakwimu vinakaribiana sana na nchi zetu za ulimwengu wa tatu. Pia mataifa mengine ni yale yaliyo kusini mwa ulaya kama Hispania, Ureno, Italia na Uturuki pia haya yana viwango vikubwa vya uhalifu huwa wanaweka sana manondo nondo dirishani.

Nchi zilizo upande wa kaskazini na magharibi mwa ulaya (Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Sweden, Norway, Finland, Denmark, Iceland, Ubeligiji, Uswisi na Ufaransa) ni kitu cha ajabu kuweka nondo dirishani. Upande huu viwango vya uhalifu vipo chini sana na watu wengi wana shughuli za kuingiza kipato ukilinganisha na wenzao wa pande za kusini na mashariki mwa ulaya.
 
Kuna siri nyingi kwenye maisha

Jaribu kuokota kitu kwenye ule uwanja wake usio na fence wenye maua, Utaleta mrejesho hapa

Maisha ni siri sana

Usione vyaelea
Hehe hehe shehe hio hatari sasa haujui MTU anajiamini vp na wala Hamna hata kamulinzi
 
Unatakiwa kuwa na system mbili,
1. System inayo kupa taarifa, alarm yenye sauti kama ya kukuamsha .. Hii system inatakiwa itambue kitu chochote kinacho gusa gate, grill za madirisha, fence etc na itoe taarifa bila mwizi kujua.

2. Unatakiwa uwe na CCTV camera.


Kuna jamaa ana system hata ukiwa mwizi ukikaribia gate tuu, gate linafunguka na kuna kasauti kanakukaribisha.. baada ya dk 5 gate linajifunga na yeye anapata taarifa kwa alarm kwennye simu yake.

Sasa kuna jamaa gate lilipo funguka akaingia , akachelewa gate likajifunga.. jamaa akafungulia mbwa tena remotely, alijikojolea hadi akagonga mlango wenyeji wampe maji.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ila kusema ukweli wafungaji wengi wa cctv camera hawana akili ya kuongeza intelligence ya hizi system.

98% ya cctv camera hazija wahi kamata mwizi japo 60% ya wenye cctv camera wamewahi ibiwa wakiwa na hizo camera
 
Ni kweli hakuna hata DNA database ya wahalifu. Picha za cctv camera kwa aliyefunika uso haziwezi kuwa ushahidi wa kutosha.
 
Ndugu yangu TV zinaibiwa kila siku Bongo tena kila sehemu sio Masaki sio Tandale.
Nilikaa Philipines nako wana grill kwa sababu ya wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…