KIBOSHO: Askari wanaofanya operesheni ya kuua mbwa waua Binadamu,baada ya mbwa alielengwa kukwepa

Sio kila askari ni Polisi.huyo mleta habari amekurupuka mno.
Sijui kwa nini huwa watu wanakimbilia kuleta habari nusu nusu?
Wewe unaefahamu pia umekosoa nusu, kwanini haukukosoa na kuweka taarifa sahihi?
 
MBWA KAKWEPA RISASI IKAMPATA BINADAMU AKAFA[emoji848][emoji848][emoji848]

KIMO CHA MBWA NA BINADAMU SAWA KWELI? NINA MASHAKA NA ULENGAJI WA HUYO ASKARI
Au tuseme marehem alikua kainama? Au kajilaza chali?
 
Kuna miji kama huku niliko sijaona mbwa wakizurura sijui imetumika mbinu gani
 
Mbwa anawindwa na risasi ya moto?
 
Mbwa anakwepa risasi? Maajabu ya mwaka. Binadamu mwenyewe kuweza kukwepa ni maajabu tosha.
 
Amelipigwa Risasi akiwa anatembea kwa mguu akitokea kazini

Kifuani akiwa kasimama na mbwa kakwepa, Sasa mbwa naye sijui alikuwa kasimama maana kifua cha binadamu na kimo cha mbwa, mh kuna wa lakini Sana.
 
Tuombe wakija hapa wasiseme marehemu alikuwa akiigiza kutembea kwa mikono na miguu huku akibweka kama mbwa.
 
Kuna kitu hakipo sawa,alikusudiwa kufa mbwa na risasi ikafikia kwenye kifua Cha binadamu,

Basi Hilo jibwa lilikuwa kubwa na refu jamani
 

 
Hiyo ni ajali katika kazi, inaweza kuwa uzembe wa Askari au wa marehemu, taarifa haijakamilika vizuri
Huo ni uzembe tu! tusiume maneno!

1-mbwa wanapigwa risasi akiwa close range!

2-utumiaji wa risasi za moto una taratibu zake pamoja na kuzua shughuli zozote katika eneo Husika na luweka bendera nyekundu kabla za zoezi!
 
Huyo mbwa alikuwa mrefu sana au aliyeuwawa alikuwa mfupi au risasi huwa inasafiri kwa kupaa juu mpaka kutoka uelekeo wa kimo cha mbwa kufikia kifua cha binadamu.

Kwann haijampata miguuni?
 
Poleni sana ndugu
 
Kwa hiyo,

Unataka kunambia anaeruhusiwa kuwa na silaha uraiani ni Mwanajeshi?
Huyo sio Askari polis.ni bwana misitu ndo huwa wanafanya hizo operation ,na wanaruhusiwa kutumia bunduki ,na idara Yao Ina budget kabisa ya manunuzi ya risasi .

Hata wanyama Kama mamba n.k huwa ndo wanawapiga shaba endapo ni tishio kwa bndam.

Liombe radhi jesh Mara moja,kwa kulituhumu
 
Kwanini msiwaite ndugu zetu wahehe wakafanya yao?[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Kuna vitu vyashangaza sana ! hizo ni kazi za watu wa veterinary department .

Hao tanpol wanaenda kutumia live bullets kwa mbwa wakati kitengo cha vet wangeweza kuelimiate hao mbwa in a safest way !

Hao polisi hiyo si kazi yao pia nani kawatuma?
Kwani wewe nani kakwambia ni polisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…