Kibu Denis alipopewa uraia kwa njia ya mlango wa nyuma ilikuwa sawa ila ni kosa kwa Singida Black Stars kufanya kwa wachezaji wake

Mpigania uhuru wa pili

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
3,380
Reaction score
6,376
Kuna watu wanaleta ushabiki wa Simba na Yanga kwenye swala nyeti la uraia, wakati Simba inamsajili Kibu ilimsajili kama mchezaji wa Kitanzania kwani alishachezea Geita na Mbeya City kama Mtanzania. Wakati huo alikuwa amechaguliwa timu ya Taifa hivyo mpaka anapewa uraia Simba haina sehemu yoyote ya kulaumiwa.
 
Ushabiki wa Simba na yanga unazalisha matahira wengi sana
 
Hii fungulia mbwa ina athari kubwa tu huko mbeleni.

Hao wachezaji wenyewe hawana hata potential yoyote kwa nchi hii na hawatokaa waitwe hata timu ya taifa.
 
 
Simba ndo walivyo. Wakifanya wao wanalazimisha ionekane wana haki zote ila akifanya mwingine wanakuwa wa kwanza kupiga kelele za malalamiko
 
Acha uongo kibu Denis kapewa uraia akiwa mbeya city
 
Kibu anapewa uraia wakati wa uamisho wake kwenda simba kutoka mbeya city ulikwama kwa ishu za urai mpaka waziri mkuu aliingili kati

Ila wewe sikushangai kama uliibishia video ya wazi ikionyesha mashabiki wa simba wakivunja viti sembuse hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…