demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Leo sikuwa na ratiba ya kutazama mechi ya Taifa Stars dhidi ya Benin. Ila baada ya kusikia watu wakiwa na hamu na shauku ya kumuona Kibu Denis, nikaona nayo ni fursa ya kuweza kumtazama.
Lengo pia ni kutazama ni kipi ambacho Taifa kama Taifa tumekiona kwa Kibu Denis hata tukafikia hatua ya Kugawa Uraia kwake. Ni kheri tungempa uraia Steven Sey (Namungo FC)
Baada ya kufanyika mabadiliko na Mwl Kim Poulsen nikaja kugundua kuwa tumepoteza nafasi ya Uraia kwa mtu asiye na cha ajabu sana katika uchezaji wake wa Mpira.
Hata ukijaribu kuchambua uchezaji wake na takwimu zake kiujumla huoni tofauti kati yake yeye na Ditram Nchimbi.
Nilicho kuja gundua kingine ni kuwa mshawasha uliopo machoni pa watanzani kuhusu Kibu Denis unatokana na uhalisia kuwa watanzania wengi hawajawahi kushuhudia jitu lenye miraba saba likiichezea timu yao ya Taifa, hivyo wakadhani wamejiokotea Lukaku Wao.
Kiuhalisia uwepo wa Kibu Denis kwenye Timu ya Taifa ya Tanzania kunapunguza hamasa na ladha ya Ushindi. Maana mara nyingi anaonekana akikosa basic skills kama vile Kupokea Mipira, Anticipation, Ball Control, Tactical Decisions.
Nadhani kama tusinge muingiza Kibu Denis kwenye mechi ya leo basi Taifa Stars tungepata Ushindi.
Sioni Taifa Stars ikipata matokeo ya Ushindi endapo Kibu Denis anahusika kwenye mechi.