Kibu Denis apewa zawadi huko Dubai baada ya kumkosha kocha mbrazili wa Simba

Kibu Denis apewa zawadi huko Dubai baada ya kumkosha kocha mbrazili wa Simba

utopolo og

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
575
Reaction score
1,575
Taarifa mpya na kubwa kutokea kambini mwa Simba huko Dubai ni kocha Robertinho kumpa zawadi Kibu Denis.

Sababu ya kumpa zawadi hiyo ni kuridhishwa na Kiwango kikubwa cha ufungaji kilichooneshwa na Kibu Denis akiwa mazoezini kiasi cha kumkosha kocha Robertinho Oliviera na kuamua kumchagua kuwa mchezaji bora wa mazoezi ya jana na hata kumpa zawadi.

Kocha huyo amesema huo ni utaratibu wake wa kutoa zawadi kwa mchezaji anayemvutia.

Tutaendelea kuwaletea kila kinachojili huku Dubai kwenye Kambi ya mnyama mkali[emoji1]

[emoji881]NguvuMoja
 
Kibu D mnyamaaa[emoji119][emoji119]

JamiiForums-1218828735.jpg
 
Hizi ndizo changamoto za kocha mpya sasa sijajua kama mashabiki wa Simba kama watamvumilia kocha,hapo unaweza ukakuta akaunda mfumo wake mwengine.
 
Shida ya Kibu inaanzia kwenye jina lake lipo kinyumenyume mana Kibu linaonyesha kama linatakiwa kuwa surname. Inasound kama linatakiwa kuwa Denis Kibu.

Pili kuna uzi juzijuzi nilisema Kibu ni mchezaji mzuri ambaye nadhani anapitia changamoto za kisaikolojia au kiroho. Haihitaji akili kubwa kuliona hilo.

Angalia Post # 5 katika Uzi huu
Pastor muombee hilo pepo limtoke akirudi aanze kushindana na kina Phiri na Mayelle kule juu kwenye mbio za kiatu cha dhahabu..
 
Huyo kocha anapenda wachezaji wenye nguvu na kimbiakimbia isiyo na faida!!, Kama anaamini Kibu D ni mchezaji mzuri basi angeacha begi lake pale uwanja wa ndege.
 
Back
Top Bottom