Kichanga aliyepotea Kagera kwa siku 7 apatikana Dodoma

Kichanga aliyepotea Kagera kwa siku 7 apatikana Dodoma

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mtoto wa mwezi mmoja, Benitha Beneti ambaye alikuwa ameibwa nyumbani kwao Mtaa wa Migera, Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amepatikana akiwa hai mjini Dodoma baada ya kupotea takribani wiki moja.

Mtoto huyo aliibwa Desemba 01, 2022 akiwa amelala kitandani ndani ya nyumba baada ya mama, Johanitha Augustino kuwasindikiza wageni waliokuja kumpa hongera ya kujifungua.

Mama wa mtoto huyo, Johanitha Augustino akiongea na waandishi wa habari amelishukuru jeshi hilo kwa kusaidia upatikanaji wa mwanae na kusema kuwa Desema 8,2022 amepata taarifa ya kupatikana kwa mtoto wake kutoka kwa jeshi la hilo na kumtaka kwenda Dodoma kumfuata mtoto wake.

"Tulifika Dodoma saa 1:30 jioni mtoto alikuwa ameishachukuliwa vipimo na mie wakanichukua vipimo siku iliyofuata majira ya asubuhi wakanikabidhi mtoto na nikaonyeshwa mtuhumiwa, nikarudi Bukoba nikiwa na maaskari polisi" amesema Augustino

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani, Kagera William Mwampaghale akiongea na waandishi wa habari amesema jeshi hilo linawashikilia watu watano ambao hakutaja majina yao wala jinsia zao wanaohusika na wizi wa mtoto huyo.

"Mara baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo tulianza uchunguzi mara moja na msako mkali ulifanyika kuanzia Desemba 02,2022 hadi Desemba 08,2022 watuhumiwa hao walianza kukamatwa kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti mkoa wa Kagera na jijini Dodoma" amesema Mwampaghale

Ameeleza kuwa, mtoto huyo baada ya kuibwa alipelekwa kata ya Kamachumu Wilaya ya Muleba kwa mganga wa jadi ili afanyiwe dawa asimsumbue aliyemchukua.

Ameendelea kueleza kwamba, mara baada ya kutoka kwa mganga huyo watuhumiwa hao walitawanyika na mtuhumiwa aliyekuwa amemchukua mtoto alielekea Dar es salaam na wengine walijificha maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera wakihofia kukamatwa.

"Msako mkali uliendelea ambapo mtuhumiwa aliyekuwa amekimbilia Dar es salaam mara baada ya kugundua anafuatiliwa aliondoka na kwenda kujificha jijini Dodoma na ilipofika Desemba 08, 2022 majira ya saa12:00 jioni mtuhumiwa alikamatwa akiwa na mtoto huyo"Amesema Mwampaghale

Ameongeza kuwa, hali ya kiafya ya mtoto huyo ni nzuri na yupo chini ya uangalizi na watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kuhusika kwenye tukio hilo, na mama aliyekuwa na mtoto amedai alikuwa na msongo wa mawazo hivyo alimuiba ili amulee, watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya tatatibu za kiupelelezi kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

MWANANCHI
 
Miaka kama nane iliyopita hukohuko Kagera kuna mwanamke hakupata watoto kwenye ndoa yake ikafika kipindi akafanya ya kufanya kichanga kikachukuliwa Dar to Bukoba, kwakuwa muda wote alionekana ana mimba basi akatoka kama miezi kwamba ameenda kujifungua kweli akarudi na katoto ka kike akakalea mpaka kanakaribia kuanza chekechea ndo mama anakamatwa ndo watu kusanuka kumbe bi dada aliiba mtoto.

Ilivyokuwa wazazi halisi wa yule mtoto walishindwa kuendelea na kesi kutokana na hali waliyomkuta nayo binti yao unaambiwa alikuwa anamtunza kama malikia mpaka huruma ikawaingia na kuamua kuchukua binti yao bila kuchukua hatua yoyote
 
miaka kama nane iliyopita hukohuko kagera kuna mwanamke hakupata watoto kwenye ndoa yake ikafika kipindi akafanya ya kufanya kichanga kikachukuliwa dar to bukoba,kwakuwa mda wote alionekana ana mimba basi akatoka kama miezi kwamba ameenda kujifungua kweli akarudi na katoto ka kike akakalea mpaka kanakaribia kuanza chekechea ndo mama anakamatwa ndo watu kusanuka kumbe bi dada aliiba mtoto.
Ilivyokuwa wazazi halisi wa yule mtoto walishindwa kuendelea na kesi kutokana na hali waliyomkuta nayo binti yao unaambiwa alikuwa anamtunza kama malikia mpaka huruma ikawaingia na kuamua kuchukua binti yao bila kuchukua hatua yoyote
Daaaah, nimeumia sana
 
Back
Top Bottom