Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Vyuma vikikaza sana watu huerevuka zaidi na kutafuta kila namna ya kutoka kimaisha ama la walau watoto waende chooni.
Kuna werevu mbaya usio na baraka za mamlaka, huu huitwa utapeli na kuna werevu mbaya lakini wenye baraka za mamlaka, huu nao ni utapeli kama utapeli mwingine tuu lakini umepakwa rangi za kuvutia sana. Mfano wake ni haya makanisa ya mitume na manabii.
Kuna walalahoi wamejionea namna mitume na manabii wanavyotajirika kupitia waumini wajinga sana.. Sasa nao wameamua kuja kivingine
Kuna dini iliyopewa jina la mpinga Kristo (Freemason/ wajenzi huru). Kwa ujinga uleule wa waumini wa mitune na manabii huku nako kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu hii imani ya The Masons/ Freemason!
Mwanzoni walikuwa wanabandika matangazo yao mitaani na kujitangaza mitandaoni, lakini sasa wamepanda Viwango. Wanaonesha na ibada zao kwa kuwatumia watu waliowahi kuwa maarufu na baadae kufilisika kabisa ili kuwavuta majinga wengine.
Hapa kwenye ibada wanaonekana watu wawili; Kasisi wa Freemason na muumini mpya (Lucas Mkenda) aka Mr. Nice. Hawa wako mbele ya sanamu la kishetani (satanism statue) na kasisi anaigiza kumuingiza Mr nice kwenye hiyo imani mpya
Kichekesho cha karne;
- Freemason ibada zao hutawaliwa na usiri mkubwa na hawarekodiwi na ukitokea wakirekodiwa ni kwa matumizi yao binafsi hawawezi kamwe kurusha mitandaoni
- Freemason hawavai kichovu kana hawa waigizaji hapa.. Kasisi kavua viatu hana socks Muumini naye kavua viatu ila yeye kavaa socks
- Mimbari ya Freemason ni kubwa na ya gharama kubwa na nadhifu sana.. Wanaoisogelea hawavui viatu
- Ibada zao sio za watu wawili na za dakika tano, huwa ni ibada maalum yenye watu maalum waliovalia suti kali nadhifu na za gharama
- Kuna vitambaa maalum vyenye nembo yao huvaliwa kuzunguka kiunoni
Wana formalities nyingi zilizopangiliwa vizuri na kwa utaratibu maalum na wa kipekee mno.
Hiki kituko cha Mr Nice na huyo tapeli wake juha kilichorekodiwa kwa simu na kurushwa tiktok huku kukiwa na nambari za simu ni udhalilishaji mkubwa wa imani zinazoheshimiwa na za kaliba za juu mno
Kama ugumu wa maisha ndio umemfanya Mr. Nice ashiriki huu upuuzi ina maana anaweza kufanyishwa kitu kingine kibaya zaidi na cha aibu kubwa mradi tu apate chochote!
Ni lazima atambue wakati ni ukuta huwezi kushindana nao! Aliinuliwa akaishi maisha yake bila haya maujinga yake! Ana nafasi ya kusimama tena kama kipaji chake kilikuwa halisi lakini sio kwa kutumia shortcuts kama hizi na kama alitaka kutengeneza kiki aliyemshauri kamuingiza cha jiji.