Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Watu wanaendekeza siasa mno kuhusu suala la CAG. Rais halazimiki kumteua CAG yule yule kila baada ya miaka mitano. Katiba na Sheria viko wazi kwa yeyote kuona. Kwa vile marais waliopita walimteua mtu yule yule kwa vipindi zaidi ya kimoja haina maana Rais ajaye analazima kurudia kumteua.
Kilichowazi ni kuwa pindi akishateuliwa na kuapishwa CAG hawezi kuondolewa kirahisi hadi muda wake wa miaka mitano upite au yatokee yale yaliyoanishwa kwenye Katiba kuweza kumuondoa. Ina maana Rais hawezi kuamka na kumtumbua au kumuondoa ofisini kiholela - ndio maana Ndugai pamoja na majaribu yote hakuweza kumuondoa.
Sasa kipindi cha miaka mitano kikiisha CAG anaweza (eligible) kuteuliwa tena; lakini hawezi kulazimisha kuteuliwa tena kwa vile tu alikuwa CAG miaka mitano iliyopita. Huku ni kutokusoma na kuelewa kwa usahihi Katiba na sheria.
Swali ambalo linaweza kuulizwa na labda la muhimu kisheria ni hili:
Kwa vile CAG inadaiwa hajafikisha miaka 60 ya kustaafu kwa lazima na kwa vile hajateuliwa kushika tena nafasi hiyo je bado anaendelea kuwa mtumishi wa umma au la? Kama ni ndiyo basi ni wazi atapangiwa kazi nyingine hadi atakapofikisha miaka 60 ya kustaafu (Ubalozi??). Lakini kama siyo, ni wazi atalipwa mastahili yake yote kwa muda wote aliokuwa CAG na kurudi uraiani.
Tusitengeneze mlima toka kichuguu.