Kichuguu si Mlima CAG: Chuki Dhidi ya Magufuli imewatoa ufahamu sasa?

Kichuguu si Mlima CAG: Chuki Dhidi ya Magufuli imewatoa ufahamu sasa?

Watu hawana ajira kila siku mnalalamikia wazee wapumzike.

Leo kapumzishwa kipenzi chenu, mmesahau kilio cha ajira kwa vijana.

Sasa mlitaka hadi atembelee mkongojo kwa sababu mnampenda?!

Wapo wanaostaafu kwa hiyari, msikalili miaka 60.

Binafsi napendekeza ange mstaafisha Mkuchika, Kamwelwe na akipendezwa zaidi naye astaafu, awapishi na wengine.
 
Wewe mtu hujui maana ya katiba na muongozo wa kanuni za taasisi ya umma. Umeandika hovyo hovyo mawazo ya kijinga ili yule mtu akuone. Mumeshaujua udhaifu wake imebaki kazi kwenu kujito ufahamu na kuweka akili pembeni. Kabla hujaandika madudu humu uwe unajiridhisha kwanza!

Sasa nakueleza. Magufuli kwa kuteua CAN mpya kavunja katiba ya nchi mchana kweupeee. Na hata tafsiri sahihi ya maneno yaliyopo kwenye kanuni zinazoongoza ofisi ya CAG hajaielewa achilia mbali kama tutajielekeza kwenye kanuni na kuitupa katiba kama yeye alivyofanya.
Havunji Katiba kwa vile unasema kavunja. Labda ufafanue ni wapi amevunja Katiba?
 
Mimi swali langu ni hili mmk. Ikiwa kichere alitumbuliwa kwa kejeli kuwa hajui kazi yake huko tra. Leo hii kumuweka kuwa cag inamaana ameshajua kazi yake?
Tuache tumalizie weekend, haya maswali magumu magumu hayafai na weekend hii
 
Usijitoe ufahamu! Unalijua hili kwa mapana na marefu
Unajuaje kuwa nalijua. Membe akitaka kugombea achukue fomu tu, mbona CCM ina demokrasia yao. Mbona nani yule alikuwaga CCM naye alichukua fomu ya kugombea Urais dhidi ya Kikwete au mmesahau?
 
Watu hawana ajira kila siku mnalalamikia wazee wapumzike.

Leo kapumzishwa kipenzi chenu, mmesahau kilio cha ajira kwa vijana.

Sasa mlitaka hadi atembelee mkongojo kwa sababu mnampenda?!

Wapo wanaostaafu kwa hiyari, msikalili miaka 60.

Binafsi napendekeza ange mstaafisha Mkuchika, Kamwelwe na akipendezwa zaidi naye astaafu, awapishi na wengine.
Hawa si ni wabunge?
 
Kwanini Magufuli anaejinasibu kuwa msema kweli anamfuta kazi Prof Assad anasifika kwa uzalendo na kupenda kusema ukweli mtupu!?

Lazima tufikiri!
 
Sasa nakueleza. Magufuli kwa kuteua CAN mpya kavunja katiba ya nchi mchana kweupeee. Na hata tafsiri sahihi ya maneno yaliyopo kwenye kanuni zinazoongoza ofisi ya CAG hajaielewa achilia mbali kama tutajielekeza kwenye kanuni na kuitupa katiba kama yeye alivyofanya.
Tuwekee hapa hizo kanuni zinazoongoza ofisi ya CAG tujisomee...!!!
 
Professionals hawaandiki titles za kimtaani kama hivyo! Acha kuleta siasa, hata wewe unajua sababu za kutokuongoezewa kwake muda
 
Havunji Katiba kwa vile unasema kavunja. Labda ufafanue ni wapi amevunja Katiba?
Mkuu, siia nikueleweshe: Kanuni zinatamka wazi kuwa CAG anaweza kupewa awamu ya pili ya uongozi. Hili limetamkwa wazi kwenye kanuni ili kuilinda katiba. Waliotunga hizi kanuni walikuwa na lengo kuwa katiba isivunjwe.

Katiba unataka wazi kuwa CAG atastaafu akifikisha miaka 60 Hiyo ndiyo sheria mama na ukienda kinyume zni unavunja katiba Ni sawa na katiba inavyosema kuwa mtu atagombea urais wa JMT iwapo atatimiza miaka 40 kisha CCM ije na kanuni zake za mgombea awe na miaka 35 na kisha tufuate kanuni za CCM kwa vile tu ni chama tawala
 
You are absolutely right, Katika hili JPM hakukosea kisheria hakukosea hata kidogo kumchagua mtu mwingine kuwa CAG.
 
Professionals hawaandiki titles za kimtaani kama hivyo! Acha kuleta siasa, hata wewe unajua sababu za kutokuongoezewa kwake muda
Hapana sijui; sababu za kutokuongezewa muda zimetolewa kwenye taarifa kwa vyombo vya habari. Kuna jingine?
 
Mkuu, siia nikueleweshe: Kanuni zinatamka wazi kuwa CAG anaweza kupewa awamu ya pili ya uongozi. Hili limetamkwa wazi kwenye kanuni ili kuilinda katiba. Waliotunga hizi kanuni walikuwa na lengo kuwa katiba isivunjwe. Katiba unataka wazi kuwa CAG atastaafu akifikisha miaka 6a. Hiyo ndiyo sheria mama na ukienda kinyume ni unavunja katiba Ni sawa na katiba inavyosema kuwa mtu atagombea urais wa JMT iwapo atatimiza miaka 40 kisha CCM ije na kanuni zake za mgombea awe na miaka 35 na kisha tufuate kanuni za CCM kwa vile tu ni chama tawala

Hapana sidhani kama umeelewa; soma juu ya Majaji ulinganisha na CAG. Utaona kuwa kama Katiba ingetaka CAG akishateuliewa adumu hadi miaka 60 ingesema hivyo. Haijasema. Kimsingi ni kuwa kwa mfano CAG anateuliwa akiwa na miaka 45; na akaendelea kuteuliwa kwa vipindi vingine vitatu vya miaka mitano mitano; ina maana kuwa akifika miaka 60 hatoweza kuteuliwa tena (atakuwa amefikia muda wa kustaafu.) Na kuwa kama CAG anateuliwa kipindi cha kwanza akiwa na miaka 56 hii ina maana akifikisha miaka 60 itabidi astaafu kwa lazima hata kama hajamaliza muhula wake wa kwanza.

Sasa, CAG anateuliwa kwa miaka mitano tu ambayo ni guaranteed; miaka mingine mitano ni suala la mamlaka yake ya uteuzi (Rais) kuona kama wanataka aendelee au la. Kwa hiyo kwa mfano Magufuli angemteua sasa hivi tena wakati amebakisha miaka 2 kufikisha miaka 60 ina maana itabidi amteue mtu mwingine in two years. Lakini akimteua mtu ambaye yuko mbali na miaka 60 sasa (Kicherre) ina maana kati ya teuzi ambazo hatokuwa anahangaika nazo in the next five years itakuwa ni ya CAG. Akishamteua hawezi kumuondoa kirahisi hadi atimize miaka yake 5.
 
Hawa si ni wabunge?
Wabunge hawazeeki?!

Wabaki na ubunge wao, wizara wapewe vijana nao wakapate uzoefu.

kila siku tunalalamikia uadilifu na inexperienced staff, wapewe vijana tuwa groom ndiyo tutaenda sawa.

Tuache kutetea wazee kila siku, tusiwatupe bali tuende nao watupe uzoefu, ili wakiondoka tuweze kujiongoza.

Asad katumika, inatosha sasa apewe mwingine ndio tunataka hivyo, nchi hii yetu sote hivyo tuijenge sote pamoja.

Na kwa wale wanaoweza kustaafu kwa hiyari tuwaombe wafanye hivyo, ingesaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo, ukitoka mwingine anasogea mwisho mwingine anaingia.

AJIRA SIO NDOA!
 
Mwanakijiji hujasoma sehemu inayosema mtu aliyewahi kuwa CAG HARUSIWI KUFANYA KAZI NYINGINE YA UMMA??

Huyu Mussa Assad kabla ya kuteuliwa na mkwere kuwa CAG alikuwa mhadhiri pale UDSM. Akiwa kama CAG alikuwa on secondment hivyo anaweza akitaka kurudi na kuendelea kufundisha kama wanavyofanya wenzie wakina Ndullu, Likwelile na Mwamba.

Marupurupu anayostahili ni yale tu ambayo atapewa kuhusiana na kipindi cha miaka mitano aliyokuwa CAG; tofauti na vile anavyotaka kutuaminisha [ kutulisha matango pori] Pascal Mayalla kuwa atalipwa marupurupu ya CAG mpaka atakapofikisha miaka 60!!!
 
Back
Top Bottom