Kichuguu si Mlima CAG: Chuki Dhidi ya Magufuli imewatoa ufahamu sasa?

Watu wanaendekeza siasa mno kuhusu suala la CAG. Rais halazimiki kumteua CAG yule yule kila baada ya miaka mitano. Katiba na Sheria viko wazi kwa yeyote kuona. Kwa vile marais waliopita walimteua mtu yule yule kwa vipindi zaidi ya kimoja haina maana Rais ajaye analazima kurudia kumteua.

Kilichowazi ni kuwa pindi akishateuliwa na kuapishwa CAG hawezi kuondolewa kirahisi hadi muda wake wa miaka mitano upite au yatokee yale yaliyoanishwa kwenye Katiba kuweza kumuondoa. Ina maana Rais hawezi kuamka na kumtumbua au kumuondoa ofisini kiholela - ndio maana Ndugai pamoja na majaribu yote hakuweza kumuondoa.

Sasa kipindi cha miaka mitano kikiisha CAG anaweza (eligible) kuteuliwa tena; lakini hawezi kulazimisha kuteuliwa tena kwa vile tu alikuwa CAG miaka mitano iliyopita. Huku ni kutokusoma na kuelewa kwa usahihi Katiba na sheria.
Swali ambalo linaweza kuulizwa na labda la muhimu kisheria ni hili: Kwa vile CAG inadaiwa hajafikisha miaka 60 ya kustaafu kwa lazima na kwa vile hajateuliwa kushika tena nafasi hiyo je bado anaendelea kuwa mtumishi wa umma au la? Kama ni ndiyo basi ni wazi atapangiwa kazi nyingine hadi atakapofikisha miaka 60 ya kustaafu (Ubalozi??). Lakini kama siyo, ni wazi atalipwa mastahili yake yote kwa muda wote aliokuwa CAG na kurudi uraiani.
Tusitengeneze mlima toka kichuguu.

Mwanakijiji ni wewe ninaekufahamu umeandika huu ujumbe au umeibiwa simu?
 
Hivi mnadhani Rais anaamka tu na kusema fulani kuwa fulani na fulani atakuwa fulani? Ni ngumu sana kumkamata Rais kwenye mitego midogo kama hii. Siri za Ikulu ni nyingi hujuibkumetokea nini.
Wewe mtu hujui maana ya katiba na muongozo wa kanuni za taasisi ya umma. Umeandika hovyo hovyo mawazo ya kijinga ili yule mtu akuone. Mumeshaujua udhaifu wake imebaki kazi kwenu kujito ufahamu na kuweka akili pembeni. Kabla hujaandika madudu humu uwe unajiridhisha kwanza!

Sasa nakueleza. Magufuli kwa kuteua CAN mpya kavunja katiba ya nchi mchana kweupeee. Na hata tafsiri sahihi ya maneno yaliyopo kwenye kanuni zinazoongoza ofisi ya CAG hajaielewa achilia mbali kama tutajielekeza kwenye kanuni na kuitupa katiba kama yeye alivyofanya.
 
Watu wanaendekeza siasa mno kuhusu suala la CAG. Rais halazimiki kumteua CAG yule yule kila baada ya miaka mitano. Katiba na Sheria viko wazi kwa yeyote kuona. Kwa vile marais waliopita walimteua mtu yule yule kwa vipindi zaidi ya kimoja haina maana Rais ajaye analazima kurudia kumteua.

Kilichowazi ni kuwa pindi akishateuliwa na kuapishwa CAG hawezi kuondolewa kirahisi hadi muda wake wa miaka mitano upite au yatokee yale yaliyoanishwa kwenye Katiba kuweza kumuondoa. Ina maana Rais hawezi kuamka na kumtumbua au kumuondoa ofisini kiholela - ndio maana Ndugai pamoja na majaribu yote hakuweza kumuondoa.

Sasa kipindi cha miaka mitano kikiisha CAG anaweza (eligible) kuteuliwa tena; lakini hawezi kulazimisha kuteuliwa tena kwa vile tu alikuwa CAG miaka mitano iliyopita. Huku ni kutokusoma na kuelewa kwa usahihi Katiba na sheria.
Swali ambalo linaweza kuulizwa na labda la muhimu kisheria ni hili: Kwa vile CAG inadaiwa hajafikisha miaka 60 ya kustaafu kwa lazima na kwa vile hajateuliwa kushika tena nafasi hiyo je bado anaendelea kuwa mtumishi wa umma au la? Kama ni ndiyo basi ni wazi atapangiwa kazi nyingine hadi atakapofikisha miaka 60 ya kustaafu (Ubalozi??). Lakini kama siyo, ni wazi atalipwa mastahili yake yote kwa muda wote aliokuwa CAG na kurudi uraiani.
Tusitengeneze mlima toka kichuguu.
Embu tuone katiba inasemaje kidogo
Screenshot_20191103-215012.jpeg
Screenshot_20191103-215027.jpeg
Screenshot_20191103-215041.jpeg
 
Nimekuelewa lakini hapa lengo ni kutengeneza mazingira ya "plunder with impunity"

Huyu Jiwe ana operate na oligarchy yake iliyo royal kwake. Tukubali tulikosea kumpa nchi atawale, tusubiri the worst to come from him hadi aje atoke ofcn.
Upo sahihi mkuu Ndugai na wabunge wa ccm walisema hawataki kufanya nae kazi kwa maagizo ya jiwe obvious hili lilitegemewa.
 
Huyo unayemtetea ndiye anaikamua JF mahakamani. Wewe endelea kumtetea inaezekana akaamuamuru DPP afute kesi.

Tanzania tuna CAG mwenye elimu ya kuunga unga.

Tz tuna CAG tuliye ambiwa hawezi kazi na akatumbuliwa.

Alafu mtu huyo huyo akamteua awe CAG... JE kama kazi ya TRA kashindwa atauweza U-CAG?

Only in tanzania.

Kwa mtindo huu Tanzania ya viwanda itaendelea kuwa wimbo wa jukwaani tu.

Pathetic!
Mkuu uzuri mleta mada wote tunamjua dishi lilishayumba siku nyingi hataki tena kuusimamia ukweli ila umempa za uso.
 
Watu wanaendekeza siasa mno kuhusu suala la CAG. Rais halazimiki kumteua CAG yule yule kila baada ya miaka mitano. Katiba na Sheria viko wazi kwa yeyote kuona. Kwa vile marais waliopita walimteua mtu yule yule kwa vipindi zaidi ya kimoja haina maana Rais ajaye analazima kurudia kumteua.

Kilichowazi ni kuwa pindi akishateuliwa na kuapishwa CAG hawezi kuondolewa kirahisi hadi muda wake wa miaka mitano upite au yatokee yale yaliyoanishwa kwenye Katiba kuweza kumuondoa. Ina maana Rais hawezi kuamka na kumtumbua au kumuondoa ofisini kiholela - ndio maana Ndugai pamoja na majaribu yote hakuweza kumuondoa.

Sasa kipindi cha miaka mitano kikiisha CAG anaweza (eligible) kuteuliwa tena; lakini hawezi kulazimisha kuteuliwa tena kwa vile tu alikuwa CAG miaka mitano iliyopita. Huku ni kutokusoma na kuelewa kwa usahihi Katiba na sheria.
Swali ambalo linaweza kuulizwa na labda la muhimu kisheria ni hili: Kwa vile CAG inadaiwa hajafikisha miaka 60 ya kustaafu kwa lazima na kwa vile hajateuliwa kushika tena nafasi hiyo je bado anaendelea kuwa mtumishi wa umma au la? Kama ni ndiyo basi ni wazi atapangiwa kazi nyingine hadi atakapofikisha miaka 60 ya kustaafu (Ubalozi??). Lakini kama siyo, ni wazi atalipwa mastahili yake yote kwa muda wote aliokuwa CAG na kurudi uraiani.
Tusitengeneze mlima toka kichuguu.
Hapa umeandika riwaya ya kufikirika maana hakuna hata kifungu kimoja cha sheria ulichoonesha kuegemea.

Unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi lakini kwa mambo yanayohusu sheria na katiba, nguvu ya hoja ni lazima iegemee kwenye vifungu vya katiba na sheria kuliko kuandika kama mpiga debe.
 
Wewe mtu hujui maana ya katiba na muongozo wa kanuni za taasisi ya umma. Umeandika hovyo hovyo mawazo ya kijinga ili yule mtu akuone. Mumeshaujua udhaifu wake imebaki kazi kwenu kujito ufahamu na kuweka akili pembeni. Kabla hujaandika madudu humu uwe unajiridhisha kwanza!

Sasa nakueleza. Magufuli kwa kuteua CAN mpya kavunja katiba ya nchi mchana kweupeee. Na hata tafsiri sahihi ya maneno yaliyopo kwenye kanuni zinazoongoza ofisi ya CAG hajaielewa achilia mbali kama tutajielekeza kwenye kanuni na kuitupa katiba kama yeye alivyofanya.
Mkuu badala ya kutoa povu ungeweka hivyo vifungu vya katiba vilivyokiukwa.. Vinginevyo na wewe umejambajamba tu hapa
 
Hilo naona nalo watu hawaliangalii na ndio maana Membe kuonyesha dalili za kuchukuwa fomu 2020 kesha onekana kama mhaini.
Kama ilivyo kwa CAG, hata Rais sio lazima wananchi wampe kipindi kingine cha miaka mitano. Hakuna mahali panalazimisha hivyo.
Kichuguu (Rais) hakiwezi kuwa mlima (wananchi).
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Aisee... Bavicha mna hoja za kipumbavu!
 
Usimjibu mpumbavu kadri ya upumbavu wake usije kuwa sawa na yeye... Mithali 26:4

Watahangaika sana na JPM lakini ukweli utabaki kuwa ukweli zile pesa walizokuwa wanakula watazitapika tu watake wasitake. Hapa kazi tu JPM
 
Naijali nchi yangu bashite wewe uko kwenye unfalme kula kumbuka kusaza Magufuli ni fisadi na wewe team endelea kuenjoy for now lakini mutaishia ukingoni tu
Hivi Lowasa nae akiishia ukingoni eti?
Si baadae mlitaka awe rais wenu?
 
2020 nami nagombea urais kupitia ccm iwe mvua iwe jua
Nalog off
 
Then, ataenda kuendelea na shughuli zake nyingine za binafsi.
Mwanakijiji unaelewa unachochangia. Umri wa kustaafu ni miaka 60. CAG hajafikisha. Hapo amestaafu au amestaafishwa?

. Umri wa CAG kustaafu ni miaka 60
. Akistaafu haruhusiwi kuwa mtumishi wa umma
. Kama umri wa kustaafu haujafika, ina maana hajastaafu. Ataendelea kuwa mwajiriwa wa serikali kwa nafasi ipi bila ya kuwa mtumishi wa umma?
. Hiyo ndiyo sababu ya wakati wote tulipokuwa na uongozi wenye hekima, hakuna CAG aliyeondolewa kwenye nafasi yake kabla ya kufikisha umri wa miaka 60.
. Uongozi siyo sheria na kanuni pekee yake bali ni pamoja na busara ya kuamua ufanye nini ili kuepusha migongano.
 
JPM hawezi kuwa worse kuliko Che-nkapa au JK. Haitawezekana, hizo ndio chuki ambazo hazizingatii maendeleo yanayoletwa katika kipindi hiki cha awamu ya 5.
Hivi kikubwa alichofanya Magufuli kumzidi Mkapa na Kikwete ni nini? Kwa maendeleo ya jumla ya kila sekta, the current regime has done incomparably much less.
 
Mkapa alishiriki kuwauzia shares SA za makampuni yetu ya NBC, Air Tanzania, Tanesco etc kwa bei ya peremende, na wao wakayaua kwa kifo cha mende. JK aliruhusu waporaji wa rasilimali na kuiba twiga wetu na kufilisi taifa na kutembeza bakuli huko Ulaya. JPM karudisha nidhamu serikalini na kuweka kipau mbele kufufua mashirika yaliyouzwa na kutokutegemea bakuli huko ulaya. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Back
Top Bottom