Kichuguu si Mlima CAG: Chuki Dhidi ya Magufuli imewatoa ufahamu sasa?

Soma post #182 halafu ifafanue ili wakina Tomaso tuelewe
 
Kwani kazi ya TRA na CAG ni sawa?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Zinafana kwa kiasi fulan kwani zinahusu mahesabu ya fedha. Swali langu ni je?? Ikiwa taasis ndogo ya tra kwenye section ndogo hakuwa na ufanisi je? Huko kwenye hesabu za serikali ambako yeye ndio top atakuwa fanisi? Je rais anaweza kutuambia kuwa yeye rais ndio hakuwa sahihi alipomdemote toka tra hadi kwenda kuwa Ras njombe?

Je haoni yale maneno yake ya kashfa na kejeli alosema siku anamtumbua ameyajajisi tena? Yaan kajirudishia
 
In light of this new information, like Prof. Shivji, I stand corrected.

Magufuli violated the constitution by not adhering to the proper impeachment tribunal process that is constitutionally prescribed.
 

Huyo Prof. Shivji ameshaomba radhi kwamba hakusoma ss.3 na amethibitisha kuwa katiba imekiukwa kaangalie tweeter
 
Suala la ufanisi ni tata sana, kwa sababu mtu anaweza ku evolve.

Pia, rais anapata taarifa nyeti nyingi sana ambazo hatuzijui.

Zaidi, kwenye uteuzi hatakiwi kutoa sababu wala ku justify maamuzi.

Tena, kazi za serikali ya Tanzania, mtu unaweza kushushwa cheo ili kupimwa kama utatetereka au una akili isiyotetereka, ukionekana hujatetereka unapandishwa cheo.

Serikali haina adabu.

Tatizo ninaloliona hapa ni kwenye kumuondoa Assad.

Inaonekana CAG kuondolewa, hata baada ya mkataba wa miaka mitano kuisha, kuna impeachment tribunal inatakiwa kumuondoa.

So far tunaona hakukuwa na tribunal hiyo, Magufuli kaamua mwenyewe tu.
 
Mzee Mwanakijiji, je! Hujui kwamba CAG haruhusiwi kuteuliwa katika kazi nyingine yoyote ya Umma baada ya kuacha/kukoma kuwa CAG?
 
Kasome tena sheria, Prof Shivji ametaja hadi kufungu kilichokiukwa sasa wewe unaongeaje hivo bila kwanza kusoma katiba. Watanzania bwana ushabiki kwenye kila kitu sijui ni kwanini.
Tumeshajadili kote huko awali.

Magufuli amevunja katiba kwa kutofuata mchakato wa kumtoa CAG.

Hata baada ya kumaliza mkataba wa miaka mitano, kumuondoa CAG kunataka mchakato wa impeachment tribunal.
 
Enzi zile ukiwa na akili timamu ungejadili sababu za injustice termination lakini kwa kuwa Akili zako ulimwazima jiwe unajadili mipasho tu
 
Magufuli amejionyesha kuwa ni fisadi papa yaani kwa hili la Assad ataficha wapi uso wake Dotto James a ajiandae kufungwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji pesa madudu ni mengi mengi ha ha jamaa jizi kweli

Kama Magufuli ni fisadi, basi maana ya fisadi inatakiwa itafsiriwe upya kwenye kamusi. Asaad alijiharibia mwenyewe kutamka mambo ambayo hakuyafanyia audit. Angefanya audit na akagundua bunge ni dhaifu na akatoa report ya maandishi kuwa bunge ni dhaifu halafu baadaye popote ulimwenguni akawatangazia watu kuwa bunge ni dhaifu hakuna ambaye angemhoji. Kwa kuwa alishafanya uchunguzi na akaainisha hayo kwenye taarifa ya ukaguzi. Sasa kusema jambo ambalo hujalifanyia ukaguzi wakati wewe ni auditor ni kufanya mambo kisiasa. Najua kuna mwanasiasa mmoja anamdanganya kuwa yeye ni mkubwa kuliko rais wa JMT. Naye Asaad akadanganyika kiasi cha kudiriki kumpelekea ripoti zake hata kabla ya kuziwakilisha kwa spika. Sasa tuone huyu mwanasiasa atamsaidia vipi mtaalamu Asaad. Bahati mbaya hata hawezi kumkaribisha awe kiongozi kwenye chama chake cha kisiasa kwa sababu uongozi wa chama cha kisiasa ni uongozi wa taasisi ya umma ambao Asaad haruhusiwi kisheria!!!
 
Kwa hiyo Jiwe nae hasimuone Membe kama msaliti, miaka yake 5 ikiisha siyo lazima ccm wampitishe tena, kila mwanachama mwenye sifa anayo haki kuomba kuteuliwa. Au mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu unauma siyo?
 
Kwa hiyo Jiwe nae hasimuone Membe kama msaliti, miaka yake 5 ikiisha siyo lazima ccm wampitishe tena, kila mwanachama mwenye sifa anayo haki kuomba kuteuliwa. Au mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu unauma siyo?
Mbona unataka kubishana na wewe mwenyewe. Membe kama mwana CCM anajua Katiba na taratibu za CCM, aingie kwenye kinyang'anyiro.. sidhani kama lina issue.
 

Shida iko kwa huo muhimili mahakama. Nionavo mimi our learned president has being wrongly adviced thus reach erroneus conclusion!
 
Mbona unataka kubishana na wewe mwenyewe. Membe kama mwana CCM anajua Katiba na taratibu za CCM, aingie kwenye kinyang'anyiro.. sidhani kama lina issue.
@Mzee Mwanakijiji unachagua maswali ya kujibu yaliyo nje ya mada yako. Mambo ya Membe hayana mantiki kwenye mada.

Tafadhali rejea maswali yetu. Kama huyaoni nikurushie post namba.
 
Wewe MMMKJ umekuwa mtu mnafiki sana katika utawala huu
Sikutegemea mwandishi na mchambuzi nguli kama Mmkj anaweza akaja na hoja dhaifu anazoshindwa kuzitetea kama hii aliyoiwasilisha.

Mmkj hakufanya hata reference ya Katiba tu kujua namna CAG anaweza kuondolewa kabla ya kustaafu.
 
Umekuwa lawyer mtafisiri sheria siku hizi?Tumeoma pahala opinion za manguli wa sheria kama Prof. Shivji.
Labda utupe ufafanuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…