Kichuguu si Mlima CAG: Chuki Dhidi ya Magufuli imewatoa ufahamu sasa?

Umeongea Kwa Mahaba na unazi bila kuanishia hivyo vifungu vya Sheria
Pathetic at its best
 
Tatizo kubwa hapa ni HADHI na UADILIFU wa mteuliwa.
Mteuliwa hana hadhi mbele ya taaluma ya uhasibu na ukaguzi. Sio mtu huru kwenye maamuzi yake kama miiko ya ikaguzi inavyodai.
Uadilifu kwa watu waliofanya nae kazi unatia shaka sana.
Hiyo nafasi inataka mtu haswaa.
Kwa mara yanza nchi itapokea taarifa zinazoelemea upande 1 wa mihimili.
 
Achana na huyo ahmak
Huyo CAG kachaguliwa na chadema? Bilabkutaja chadema hamuoni raha. Huyo aliyepita kachaguliwa na raisi wa CCM na huyu ni hiyo hiyo CCM sasa chadema inaingiaje?
 
Wewe si Jana ulidai jamaa kavunja katiba kumtoa CAG?? , kuweni na msimamo bas mnatuchanganya
 
Rais hawezi kutushawishi kuwa anachukua rushwa kwa kuuacha kumuongezea muda mtu aliyeibua ufisadi wa Ths 2.4 Bilioni na kutuletea mtu ambaye alitudhihirishia mwenyewe kuwa ni dhaifu katika kusimamia TRA.

Kwa vile Magufuri ni msahaulifu, naweka clip yake mwenyewe akimuongelea Charles Kicheere wakati akimvua cheo cha CG-TRA;
 

Attachments

  • VID-20191104-WA0001.mp4
    713.5 KB
Haya, tumekusikia!
 
Hii awamu ikipita wanafiki utawashangaa watakavoikandia. Watakuja namsemo mpya wa kuitukuza awamu ya SITA usipime! Wasomi wakiwa wanafiki nchi iko mashakani.
Haitakuwa leo wala 2025 hatoki, uchaguzi unaokuja watu wake sasa wanakimbia ofisi. CAG hakutakiwa tangu mwanzo kwa sababu msema kweli, katka kipindi hiki msema kweli hastahili kuishi.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Aisee... Bavicha mna hoja za kipumbavu!
Mbona mkisikia MtuPori kuondolewa kichaa kinapanda? Ataondoka tuu, kwanza mwenyewe kasema kasukumiziwa
 
Wewe si Jana ulidai jamaa kavunja katiba kumtoa CAG?? , kuweni na msimamo bas mnatuchanganya
Wapi nilidai jamaa kavunja katiba kumtoa CAG?

Mimi nimekuwa nikiwaeleza watu kwamba hakuna katiba ilipovunjwa katika hili.

Kwa nini unanilisha maneno?

Ni kwa sababu ya ujinga au ushenzi?

Unaweza kuweka nukuu nilipodai jamaa kavunja katiba kumtoa CAG?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 

Mzee Mwanakijiji mbona unajibu hoja nyepesi. Tunaomba ufafanuzi wako kwa maswali toka kwenye hii post..

Anza na Katiba (sheria mama) inasemaje kuhusu CAG kuachia ofisi kabla ya umri.

Mjadala mzuri,
 
Huyu jamaa ana sifa zote za kuwa rais wa Tanzania.
1. Mweledi
2. Muadilifu
3. Mnyenyekevu
4. Mchapa kazi
5. Jasiri
6. Mthubutu
7. Hayumbishwi
8. Elimu yake haina shaka yoyote
Huyu ndiye Mussa Assad
Kama ni mwanachama wa CCM Tumuombe naye achukue fomu kama atakavyo chukua Membe 2020 ili kuleta ushindani ndani ya chama hicho kinacho buruzwa buruzwa utadhani mzoga wakati kina watu (baadhi) timamu na wanajitambua.
 
Umenena sawa, hata 2020 CCM inaweza kuteua mtu mwingine ashike kijiti cha Uraisi!
 
Mkuu Mwana Kijiji

Nimesoma katiba, nikairudia tena kwa utulivu. Nimeona CAG anaweza kutoka madarakani kwa njia MBILI tu.

Mosi ; Kustaafu

Pili ; Kuondolewa ikiwa atashindwa kutimiza wajibu. (Hapa kumewekwa taratibu zake Ibara 144,(2-3).
Na moja ya taratibu hizo hii ya mkataba sijaiona.

Hii kanuni ya Renewable contract inaingia wapi kwenye hizo hapo juu?
 
Mbona mengine mnasemaga anamuenzi Julius, Tena sie tunaendekeza siasa? Alim demote mwenyewe just for curiosity watu wasihoji?! Mbona Kama kocha anatatizo na sio wachezaji au haya haya tuhusu basi tunawashauri man u tu
Prof Mussa Assad atakumbukwa na vizazi vijavyo kama Mtanzania pekee kwenye awamu ya 5 aliyebakia amesimama dhidi ya ya utawala dhalimu, usioheshimu misingi ya Katiba, utawala wa sheria na utawala bora.

Jina lake litaandikwa kwenye kitabu cha mashujaa kwa wino wa dhahabu kwa kuwa alikataa kutepeta dhidi ya utawala wa kidikteta wa Magufuri. Amekataa katakata kulamba soli ya viatu vya Magufuri kama wanavyolamba wengine mfano Jaji Mkuu, Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, DPP na AG.

Profesa Mussa Assad umewatendea haki Watanzania na umeonyesha thamani ya elimu yako kwa kuibua upotevu mkubwa wa fedha za walipa kodi wa nchi yetu zipatazo Tsh 2.4 Trilion kwa kipindi cha miaka 4 kutoka utawala unaojifanya anachukua rushwa.

Yanayoendelea tunayaona kwa kupitia mteule anayekuja kuchukua nafasi yako. Hata kipofu anajua Charles Kicheere amekuja kubariki mazingira ya "plunder with impunity" kwa kipindi Magufuri atakapokuwa madarakani.

Kupumzika Prof Mussa Assad, kazi yako ilikuwa ni ya kutukuka, tutakukumbuka hata Muumba akiwa amechukua roho yako.
 
Kasome vizuri au muulize prof. Shivji
 
Uteuzi wa CAG mpya haukufuata sheria, Sheria inataka Kama CAG hatopewa mkataba mwingine wa miaka mitano basi sababu za kutofanya hivyo ziwe ni sababu za kwa mujibu wa ibara ya 144 inayozungumzia sababu na utaratibu wa kumuondoa CAG, kinyume cha hapo sheria imefafanua kuwa sharti CAG apewe mkataba mpya, Naweka sheria subsection 3 hapa inasema hivi:


Kwa hiyo ni dhahiri ukisoma katiba. na sheria inayofafanua vipengele hivyo vya katiba kwa pamoja Uteuzi wa CAG mpya haukufuata sheria.

Jambo hili hata profesa Shivji kaliona na kalizungumzia hapa chini:

 
Reactions: prs
Kama ndio hivyo na Jiwe sio lazima amalize kipindi cha pili cha miaka mitano, sababu anazojustify yeye na wafuasi wake kumtoa CAG ndio hizo zitajustify kumtoa yeye naye asiendelee kipindi cha pili.
 
Reactions: prs
Sawa ila asingemchagua kilaza wa kwenda kufanyia majaribio kodi zetu. Tumeshachoka kuona vijana wanasoma na kupata shahada ila ajira hakuna, na wapiga domo wasio na elimu ndio wanapewa kazi serikalini.
Unawadharau wapiga domo wakati lissu anaishi kwa kupiga domo
 

Kasome tena sheria, Prof Shivji ametaja hadi kufungu kilichokiukwa sasa wewe unaongeaje hivo bila kwanza kusoma katiba. Watanzania bwana ushabiki kwenye kila kitu sijui ni kwanini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…