Kichuya:Niliua off-side,ni mechi ya Mbeya City

Kwanza mtoa post huna takwimu sahihi juu ya kichuya ni wapi kaifunga yanga mechi nne mfululizo?
Weka takwimu kaka
Kichuya ni mume wwenu tu
Aliwafunga mechi zote msimu uliopita,akapiga penati kule Zenji,akapiga penati ngao ya jamii,akapiga bao kali mechi ya juzi

Tena ni mara 5
 
kuna watu hata mpira hamjawahi kucheza wala hamfatilii ila mnatoa maoni kishabiki.

kichuya ni mchezaji upo ndani unaonaje kama umeua off side, bila ushabiki ule mpira ni off side maana tangu anaupokea alikuwa ameotea wala hakuonesha kurudi nyuma kwanza kuua offside bali kaupokea(akiwa mbele zaidi ya wote) na kwenda ku score
hakuna sehemu kaua iyo offside
 
Watu hawajui maana ya off-side, Wekiona mchezaji yupo peke yake wanadhani yupo off-side. Kama mabeki hucheza off-side trick hivyo hivyo washambuliaji huvunja off-side trick.
ukiwa peke yako tena mbele kuliko wachezaji wote hiyo ni offside. unaweza kuwa peke yako ile nyuma ya timu pinzani iyo si off side.

je kichuya alikuwa peke yake mbele ya wachezaji wote ama hapana?. kichuya alikuwa peke yake mbele ya wachezaji wa timu pinzani hivyo alikuwa off-side.

kutwambia kaua off-side ni uongo, maana kapokea mpira tayari akiwa amezidi, alitakiwa arudi nyuma (nyuma ya beki wa mwisho) ndo apokee mpira aende golini (hapo angekuwa kaua off-side) ila hakufanya ivo.
 
Yanga kateni rufaa,ishakuwa goli ivyooo,waliofungwa wapo kimyaaa
 
Kama tulishafungwa mpaka goli la kutumia mkono...unadhani kuna goli gani jingine la ajabu zaidi ya hilo
 
Off-side ni moja kati ya sheria tata sana, Mara nyingi inaendana na jinsi mwamuzi alivyo-sharp na anavyojisikia.

Goli walilofungwa Mbeya City na Kichuya, Simba walifungwa mwaka huu kwenye fainali ya kombe la shirikisho, Dodoma katika ushindi wa Simba wa 2-1. Hatukusikia wataalam wa kung'amua offside wakilizungumzia, wachamabuzi walikaa kimya. lkn hili la Kichuya jana ndio inaonekana habari ya mjini.

Lkn pia tujiulize, nani aliona Kichuya alikuwa wapi wakati pasi ndio inaanza kupigwa? Kuamua eti ni offside wakati mtu ndio anafunga pekee inakuwa sio sawa. Tangu lini winga aliyekuwa kulia anajikuta ausubiri mpira katikati kama centre foward huku akiacha eneo lake bila mtu? Maana yake alitokea eneo lake, akaona concentration ya walinzi wa Mbeya City iko kwa Okwi na Bocco akaomba iwekwe kati yeye akatokea na kumiliki mpira kisha kuuweka kambani. Hata walinzi wa Mbeya City wamechelewa kunyoosha mikono hadi walioona hakuna namna ya kumfikia Kichuya ndio wakaomba huruma za mwamuzi
 
Siku mkifungwa goli kama hilo tusiwasikie mkilialia! Mwosha huoshwa pia!
Siku hizi mnazidi kumchukia kichuya eeh!
Ukisikia Kichuyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, ndani kidadeki!
 
Huyu jamaa ni mnafiki na mzushi mkubwa si wa kumuamini
 
Ndala FC wanapata shida kwa mambo ambayo ni rahisi kung'amua
 
Bro humu ni jamii forum kuna aina nyingi sana za watu wenye kariba mbalimbali, hapa Bongo hakuna daraja sijagusa, muulize Edwine Hagai au Said Maulid. Jiulize wakati mpira unatoka mguuni kwa Mkude Kichuya alikuwa position gani? Kwa umbali aliokuwa Mkude na Kichuya ulitegemea Kichuya aanze kukimbia baada ya kumfikia wakati kuna seconds zinatumika mpira ukiwa angani? Haya matukio huenda simultaneously pale mchezaji anapo release mpira na position aliyopo anayepokea mpira. Aliyecheza mpira huweka emotion pembeni na kuruhusu weledi ufanye kazi yake.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
mkuu suala la off-side mpaka leo linasumbua hata ulaya sio sisi tu, ko suala la kugusa madaraja yote halifanyi kuwa sahihi kuitafsiri ile off-side.

off side ni kweli hutafsiriwa toka pigo la mwisho la mtoa pasi (mkude) kwenda kwa mpokeaji (kichuya). tayari alikuwa yuko mbele

kwanza niseme azam hawakuwa na camera ya pembeni kuonesha vizuri ndo maana imeleta utata.maelezo ya kichuya anakwambia aliua off-side (kwa maana ya kutoka nafasi ya kuotea kurudi nyuma) kitu ambacho si kweli. hakuna sehemu amerudi, tangu anapokea (angalia video) alikuwa ana move kwenda mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…