Hongereni kuleta hivyo vichwa vipya vya Treni kama ulivyo kiri hapa.
Treni ya Umeme inahitaji Umeme wa Uhakika, ni vyema mkajipanga kwenye hilo hasa wakati huu ambapo kumekuwa na tatizo kubwa la Upungufu wa nishati hiyo.
Nikiri wazi, nilibahatika kupanda treni lenu wakati mkifanya majaribio kipande cha DSM - Morogoro.
Ni moja ya mradi mzuri sana, tumpe pongezi aliyetoa wazo la kuanzisha mradi huo.
Hofu yangu, na wengine wengi humu ni suala la Upungufu wa huo umeme wa kuendesha mitambo hiyo.
Vinginevyo mje na mpango mbadala wa kutumia Majenereta walau kuwa na uhakika wa nishati.
Ingawa najua litakuwa na cost implications.
Kila la kheri