Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa kichwa kipya cha treni ya meme chenye namba va usajili E6800-01 kilichoundwa na kampuni ya 'Hyundai Rotem Company' (HRC) kimewasili nchini Tanzania kutoka chini Korea Kusini.
TRC iliagiza vichwa vipya 17 vya meme kutoka 'Hyundai Rotem Company' (HRC) ya nchini Korea Kusini yenye namba ya usajili E6800-01 hadi E6800-17 kwa ajili ya reli ya kiwango cha kimataifa - SGR. Mfumo wa uendeshaji unaotumika katika kichwa ni nishati ya meme wenye msongo wa kilovoti 25 a kitakuwa na nguvu ya kilowati 5,000 sawa na nguvu ya 6,800 kwa kipimo cha 'Horse Power'. Kichwa kitakuwa na uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa (160km/h), kuvuta na kulisha meme kwenye mabehewa yasiyozidi 14 ya abiria kwa wakati mmoja.
TRC inatarajia kufanya majaribio ya kichwa cha treni kitakachotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa kati ya Dares Salaam na Morogoro na baadaye Dares Salaam hadi Dodoma, baada va kukamilisha ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa madereva mapema mwezi Disemba 2023.
Mwezi Disemba 2023 TRC inatarajia kupokea vichwa vingine vitatu (3), mpango wa uletaji vitendea kazi utakuwa ukitekelezwa kwa awamu pindi undwaji wa vitendea kazi unapokamilika. TRC imeshapokea mabehewa 35 kwa ajili ya uendeshaji wa huduma katika reli ya kiwango cha kimataifa.
Kufikia Septemba 2023 mradi wa SGR Dares Salaam - Morogoro umefikia 98.6%, Morogoro - Makutupora umefikia 95.41%, Makutupora - Tabora umefikia 12.32%, Tabora- Isaka umefikia 5.02% na Mwanza - Isaka umefikia 41.95%, Mkandarasi kampuni ya CCECC yuko eneo la mradi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa SGR awamu ya pili Tabora - Kigoma.
View attachment 2801271