Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,473
Mbona unakwenda off point? Kama huna cha kuchangia ni bora usome michango ya wengine.Tabia ya Mwakinyo ya kutotaka kukosolewa ameiiga kutoka hicho chama ambacho nacho hakitaki kukosolewa wala kupingwa.
Maoni yangu ni kwamba huyu kijana bado ana safari ndefu na yeye au washauri wake wanapaswa kumueleza hivyo.
Ana miaka 25 na akitumia vizuri muda wake anaweza kufika mbali sana ila kama atakuwa na 'attit..ude' kuwa yeye ndiye bora na hasikii ushauri wa waliomzidi kwa umri na uzoefu basi safari yake inaweza kuishia njiani kabla hajafika mbali.
Ushauri wangu ni kuwa kwanza atafute 'stable house' inayofahamika kimataifa na pili apate meneja wa meneja wa kimataifa na afuate ushauri wao.