Kichwani kwa Bondia Mwakinyo kupo sawa sawa? Amuombe Radhi upesi sana ' Legend ' Rashid Matumla kabla hajatuudhi zaidi

Kwahiyo bwana GENTAMYCINE umeanza kubishana na mabondia au unataka wakuondoe hivyo vimeno viwili ulivyobakiza mdomoni

Huyu Dogo ' Mwakinyo ' amenikera sana Mkuu na nilianza ' Kukachukia ' ghafla pale ambapo Siku moja alipokuwa akifanya Kipindi na Clouds tv ambapo muda mwingi alikuwa ' anajimwambafai ' huku akijiona ameshayapitia Denge Maisha ( ameukata ) na muda mwingi alikuwa akijulambalamba Mdomo huku akirembua Macho yake na nikajua kuwa kumbe alikuwa anawakilisha tabia ya Wanaume wa Tanga ambayo Watoto wa Mjini tunaifahamu kwa sana tu ila hapa Kimaadili nawatunzia Siri yao hiyo. Na nikikuchukia hata ufanyeje siwezi Kukukubali tena! Sipendi Mtu mwenye Dharau na asiyeheshimu Watu huku akiwa hapendi Kukosolewa.
 
Matumla ashachukua mkanda wa WBU na UBO wa dunia na mikanda kadhaa ya afrika
Matumla ni icon kwenye boxing tz
Sasa hyu mwakinyo kama wakina mobeto wanamfanya kuwa jeuri na kujiona star
Kwa kutotaka ushauri atapotea mapema

Ova

Apotee mara ngapi Mkuu?
 
Mbona unaanza maneno mengi na herufi kubwa katikati ya sentensi? au ni aina mpya ya uandishi mkuu.
 
Multiple IDs @ work

Bila bila itakuwa alikosea Kuandika na alidhani ananijibu Mimi GENTAMYCINE na kumbe alikuwa anamjibu Mwingine na Mimi nimemjibu baada ya Kuona amenitaja pale katika ile ' Post ' yake. Sina haja ya kuwa na ID nyingi hapa ila kama una uhakika na ID zingine kuwa ni zangu basi nakuomba wataarifu Uongozi wa JamiiForums ili uziunganishe zote na ibaki tu hii ' Brand ID ' yangu ya GENTAMYCINE.
 
Na wakishamaliza kuziunganisha unapigwa life ban ambayo kwako ni kama kunyimwa visa ya kuingia nchi takatifu
 
Mwambieni Huyo Mwakinyo Aombe Pambano La Marudiano Na Yule Mfilipo ( Ambaye Hayupo Hata Kwenye Ramani ) Na Pambano Lisifanyike Hapa Nchini. Uone Kama Hajarudi Hapa Pua Imehamia Shingoni.
 
Mjinga wewe.. mtu kajaza taifa huoni kama kafanya maajabu...


Huyo matumla siku ile ya mechi Mimi mwenyewe nilianza kumuona Hana analolijua zaidi ya wivu...


Yaani unashangaa mtu kujaza Diamond Jubilee ila hushangai mwakinyo kujaza taifa...



Hili taifa limejaa Ng'ombe zisizokuwa na akili .. Mijitu imejaa wivu.


Pvmbavu
 
Sawa ni bora wakacheki na fuse kama ziko sawa upstair.

Zingekuwa haziko sawa ningekuwa ni " Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer " kama hivi nilivyo?
 
Kwaiyo mwakinyo anaminyoo au kiribatumbo?
 
Nimepata bahati ya kusikiliza hayo mahojiano yake, nilichojifunza kwenye hayo mahojiano ni kuwa huyu dogo anadanganywa na watu waliomzunguka au anajidanganya mwenyewe kuwa yeye ni mkubwa kuliko snake boy, yani mpaka anai condition azam akicheza pambano lake snake boy asiitwe, mara snake boy kaja kuganga njaa, yani huyu kasahau mwaka jana tu alikosa nauli ya kwenda Uingereza kwenye lile pambano lililompa umaarufu mpaka leo anajulikana, waliokaribu nae wamuambie asijisahau hivyo, bado ana umri mdogo sana na ana safari ndefu ya kwenda, snake boy angekuwa kipindi hiki ambacho kuna evolution ya technology and social media pengine angekuwa maarufu mara elfu moja ya umaarufu alionao huyu dogo, ni mshauri tu kuwa kwa umri wake bado ana safari ndefu sana ya kutembea na hivyo anahitaji sapoti na ushauri wa wadau wote, anaowapenda na ata asiowapenda.
 
Naunga mkono hoja mkuu. Mwakinyo amelewa sifa lakini huwezo hana sana, kwakifupi ni overrated!

Anaanza vipi kumdharau Legend wa ngumi Tanzania kama Rashid Matumla.

Kwa faida ya wasiojua, Rashid Matumla alifanya mchezo wa ngumi ukawa na hamasa hasa huku maeneo ya kwetu uswahili. Rashid alianza kuitwa Snake Boy mpaka baadae Snake Man.

Vijana wa Keko walikuwa inspired sana na Rashid, kuanzia Keko Magurumbasi, Keko Mwanga, Keko Machungwa, Keko Toroli klabu za ngumi zikawa zinafunguliwa. Hali iliyopelekea mchezo huo kusambaa zaidi Jijini Dar Es Salaam. Huku pia ukiibua wapiga ngumi wakabaji.

Impact ya Matumla kwenye masumbwi ilipelekea baadhi ya taasisi kama JKT na Polisi kuajiri askari ambao ni wacheza ngumi. Mfano mzuri ni mdogo wake Matumla ambaye ni askari kanzu anaetembea na difenda za doria. Pia kuna Koba Kimanga na wengineo wengi.

Sasa leo hii anatokea bwa mdogo mmoja analeta dharau kwa "The Living Legend Matumla" sisi wwngine tunakuwa hatumuelewi.

Mlio karibu na Mwakinyo mwambieni apambane walau afikie rekodi ya Francis Cheka achilia mbali Rashid Matumla.
 
Binafsi nimezaliwa tanga nakukulia tanga, nimesoma mkwakwani primary na nasekondary nimesoma mkwakwani pia, nimebahatika kuwaona mabondia wengi kutokea tanga tangu miaka ya 90 mpka sasa.
Huyo mtoto mwakinyo tangu mwanzo hakua nahaiba ya ubondia kabisa. Crew yake anayozunguka nayo nimbovu nahiwez kumjenga kua boxer mzuri. Huwez kua bondia toka tanga afu ukawa mshamba kias hiki
 
Dogo mwakinyo omba radhi haraka sana!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…