Kichwani kwa Bondia Mwakinyo kupo sawa sawa? Amuombe Radhi upesi sana ' Legend ' Rashid Matumla kabla hajatuudhi zaidi

Kama kumrekebisha angeenda kwenye uongozi wa Mwakinyo Jr kama Legendary na kutoa nasaha zake, sio kuwa NEGATIVE kwenye Media kubwa kama Azam.

Matumla ana WIVU ilo liko wazi na namshauli kwenye maswala mazito ya Kitaifa next time awe POSITIVE sio kutomboka tomboka hovyo hovyo, Nilikuwa namheshimu ila sasa naomuona wa ajabu.
 
Labda hamjamuelewa.
Anacholalamika yeye. Ni matumla kumsema vibaya kocha wake mwakinyo.
 
Bondia Hassan Mwakinyo anahitaji kupewa semina namna ya kuongea na vyombo vya habari sio kila neno la kutamka tu kwenye media ilhali bado anasafar ndefu kwenye career yale ya ngumi.

Leo Hassan Mwakinyo ameongea maneno makali ya kuudhi na kumdhihak bondia mkongwe nchin Rashid Matulma snake boy mwakinyo amesema kuwa " Rashid ndiye aliyefanya watanzania wengi waamin kuwa alipigwa katika lile pambano lake kutona na aina ya uchambuzi aliokuwa akifanya siku hiyo ya pambano,pia hawezi kumueshim tena matumla mpaka amuombe radhi kocha wake yeye vilevile Mwakinyo amedai kuwa Rashid hajui kitu kwenye ngum na hawamtaki tena kwenye kwenye tasnia hiyo ya kupigana"
Sasa kauli kama hizi inakuwa sio nzur kuziongea mbele ya media yeye anatakiwa achukulie ushaur wa watu kama changamoto kwake kuendelea mbele kwan sio yeye wa kwnza kusemwa.
Anachosahau Mwakinyo ni kuwa lile pambano lilioneshwa live na kila mtanzania aliangalia ndo maana wanatoa maoni yao na wala sio kwa sababu ya uchambuzi wa Rashidi.
 
Mimi ni mshabiki tu mwakinyooo amefanya makosa namna ya kumjibu mwenzake ,lakini ukiangalia haya majibu ni kuwa hawa wanamichezo wetu hawajaandaliwa namna ya kuongea kwenye media,huyu bondia atafutiwe wataalamu wa kumpa ushauri baadae atabadilika,waige kwa watu wa mpira wa miguu kwa kweli wanajitahidi kuongea vizuri.
 
Mkuu, nimeongea kistaarabu sana ila umenishambulia kwa maneno magumu magumu!!!Nimekukosea nini kaka??Ungeandika Alicho achieve Rashid Matumla ingesaidia sana kizazi kipya wangefahamu vinginevyo wanaweza wakadhani Mwakinyo ndio mwanzo mwisho!!Nimekupa ushauri mzuri ila umenishambulia kwa maneno magumu!!Asante nimeyapokea nimeyameza kishingo upande
 
Mtoa Mada nilimshauri aweke Rekodi za Matumla kanishambulia sana kwa maneno magumu magumu nimesikitika sana
 
Hivi kwani arsene wenger hawezi kukosoa mbinu za jose Mourinho??

Japo Mourinho anaweza kua na vikombe vikubwa kumzidi wenger??
Hoja sio kukosolewa, hoja ni kusema Matumla hajafanya kitu, sasa hapo ndipo rekodi zinapohitajika mkuu!!Kwa Mfano wako ingekuwa kama Wenger angesema Mimi ni kocha bora na mwenye mafanikio kuliko Mourinho hapo ndipo wadau wangetaka Rekodi ziwekwe mezani ili Rekodi zizungumze
 
Matumla hakuongea vibaya bali ni tafsri ya huyo mtoto na jopo la watu wake alichosema ni kuwa anadhani Mwakinyo aina ya upiganaji wake nikama umeshasomeka na wapinzani wake na hajafanya mabadiliko kama anataka aende mbalizaidi ya hapo inabidi atizame namna ya kubadili mbinu au kocha na akasema kabisa kuwa si kuwa kocha yule ni mbaya ila mapambano huko mbele yatakuwa makali kuliko hilo nayanahitaji kocha mwenye uwezo zaidi kwani ni kawaida tu kwenye ndondi kubadili kocha hata kama kocha ni nduguyo kiuchambuzi siuoni tatizo, kusingizia matumla kwa mapokeo ya watanzania ni kumuonea kunawatu walianza kuponda na kutaka apigwe hata kabla ya pambano nao walitumwa na matumla ajifunze pia kwa wachezaji wa mpira hupondwa wazi hata kama wanaumia huwa wanatumia hiyo kama changamoto
 
Wewe ndio hujaelewa kabisa
 
Mkuu ni kawaida kwa watanzania hivyo usishangae SIKU ISHA MASHAUZI akimdharau BI.KIDUDE.
 
Floyd Myweither aliachana na baba yake seuse Kinyogori
 
Mimi naitaf naitafuta hiyo interview ili nipate cha kuongea coz wabongo ni watu wakuongeza kachukbari
 
Kwenye uandishi kwa hapo ulipotumia fungua semi na funga semi, maana yake ulikuwa una mnukuu Mwakinyo.

Hivyo ulitakiwa kutumia maneno yaleyale ya Mwakinyo, ambayo naamini yako katika nafsi ya Kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…