KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

Kama wanaweza kupokea vijana wawafundishe nafikiri tuwapeleke na sisi tuwe na hazina ktk jeshi letu.
Hawa wa kwetu ni kuvunja matofali kwa kichwa ndio ukuaji wa technology
 
m ntakuwa nachukua mazoezi ya kuendesha pikipik kwa stlye za hatari.ukirud we m naajiriwa kama helper.mbona watakuwa waadilifu.no kuuza
wanyama,no kuweka pesa nnje,no kufisadi.kila mtu atakuwa muoga.chezea kuvumuzishwa kabla sir god mwenyewe ajaamua
mmmmmm
 
Mara ya mwisho hawa jamaa kusikika kwenye vyombo vya habari ni pale walipoenda Dubai kama watalii kutoka nchi mbalimbali na kumuua Ofisa wa ngazi ya juu wa Hamas Mahmoud Al-Mabhouh kwenye chumba cha Hoteli aliyofikia. Kamera za Usalama za Uwanja wa ndege ziliwaonyesha toka wanawasili Dubai. Kamera za Hotelini zliwaonyesha tangu wakiwasili hotelini hapo mpaka wauwaji walipokuwa wakiingia kwenye chumba cha bwana Mabhouh na kutoka baada ya kumaliza kazi wakiwa wameshika tennis rackets wakipozi kama vile wanaenda kucheza tennis.

Na mikakati na sera hizo ndizo zimewawezesha kuishi hapo na kufanya maendeleo kama taifa. Bila hivyo wasingekuwepo. Kumbuka walipotangaza taifa lao tu hapo hapo nchi za kiarabu zikajiunga na kuwavamia. Jiulize, ndiyo tu wametangaza kuanzisha taifa wakavamiwa na majeshi ya nchi zaidi ya tano kutaka kuwaondoa lkn wakashinda. Mnakumbuka vita ya siku7 na pia Yom Kipur war. Ni series of war after war. Na mnafahamu kuwa kuna nchi na makundi mengi tu lengo lao ni kuwafuta kabisa wayahudi wasiwepo duniani. Kwahiyo jinsi wanavyo behave na maisha wanayoishi ni sbb ya maadui wao na ndiyo njia pekee wanaweza kuishi na kuendelea kuwepo kama taifa.
 
ndicho nilitegemea mkuu maana story bado inahitaji kuendelezwa
Kweli, nilipanga kuandika zaidi kuna mengi sana ya kushare na wana JF wenzangu kuhusu hawa watu. Nilibanwa kidogo na shule. Nikiweka ntaku tag kwa heshma yako busegwe
 
Kweli, nilipanga kuandika zaidi kuna mengi sana ya kushare na wana JF wenzangu kuhusu hawa watu. Nilibanwa kidogo na shule. Nikiweka ntaku tag kwa heshma yako busegwe
Nashukuru kwa ushirikiano wako mkuu naisubilia kwa hamu kubwa
 
"Mparestina atafute nchi yake tu"
SASA KAMA KUNA KITENGO CHA KIJASUSI KAMA HICHI SASA MBONA WAPALESTINA HAWAISHI WANAENDELEA KUONGEZEKA NA KIWAUA WAISRAELI KILA SIKU HAUONI KUWA KUNA KI2 HAPO HEBU TUENDELEE KUONGELEA MAENDELEO YA KIINTELIJENSIA YA NCHI YE2 PENDWA TANZANIA TUACHANE NA MA-CONSPIRACY.
 
KIDON ni kitengo ndani ya Mossad chenye jukumu la kufanya mauaji dhidi ya wale wenye kuhatarisha usalama wa Israel. KIDON ndio wanaosifika na kuogopwa zaidi duniani katika kufanya assasinations kwa ufanisi na ufasaha wa hali juu


Neno Kidon ni la kiyunani lenye maana ya ncha ya upanga, hili lina akisi jinsi kitengo hiko kilivyo mahiri na hatari katika kufanya mauaji.



Kidon ilianzishwa miaka ya 70 kutoka katika kitengo cha Caesaren kilichokuwa chini ya Mossad kufuatia kuuawa kwa waisrael 11 waliokuwa washiriki katika mashindano ya Olympic mjini Munich Ujerumani mwaka 1972. Mauaji hayo yalifanywa na wapiganaji wa kipalestina, japo waisrael wengi walikufa wakati polisi wa Ujerumani walivyojaribu kuwaokoa mateka. Na mara moja baada ya kuundwa wakapewa kazi ya kuua kila aliyehusikia na mauaji hayo ya waisreal kazi iliyofanyika kwa mafanikio makubwa japokuwa kuna wahanga nao walikufa

Mbali ya kuwa kitengo hiki kuwa chini ya Mossad lakini kutokana na usiri wake mkubwa hakina ofisi ndani ya makao makuu ya Mossad mjini Tel Aviv. hata ma-agent wake ni vigumu kutia mguu makao makuu, hii ni kwa mujibu wa afisa wa zamani wa intelijensia katika kitengo cha Mossad kinachoratibu shughuli za Kidon bwana Mishka Ben-David katika kitabu chake "Duet in Beirut". Anaendelea kusema kuwa hata majina wanayotumia ni majina ya kufikirika na si majina rasmi, na wakiwa shughulini hutumia jina la 3 la mhusika na mara nyingine hadi utambulisho wa 4 na wa 5. kutoka na usiri na ufanisi wa hali ya juu, kitengo hiki kimepachikwa jina la Mossad ndani ya Mossad

Recruitment katika kitengo hichi ni kutoka katika special forces wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya
Israel Defence Force (IDF) na hupatiwa mafunzo ya hatari kwa mda wa miaka 2. hawa jamaa wanasifika kwa kutoacha alama yeyote katika assasinations zao na wamekuwa wakifanikiwa kwa miaka mingi

Wauaji hutumia pasi na nyaraka feki za mataifa mbalimbali za kusafiria zilizofojiwa kwa ustadi wa hali ya juu na wataalamu wao au hutumia pasi halisi za mataifa mbalimbali ambazo picha hubadilishwa kiutaalamu ili kufanana na mhusika. Pia wanauwezo mkubwa sana wa kujipenyeza na kuingia nchi yeyote na kufanikisha mauaji.

Katika mauaji wanayoyafanya pale mashariki ya kati, mtindo maarufu ni ule ya wauaji wakishambulia huku wakiwa wanatumia usafiri wa pikipiki. Mtindo huu ndio umetumika kuwaua maprofesa na wanasayansi wa nyuklia wanne wa Irani mpaka sasa. Katika mtindo huu, kawaida timu ya wauaji inakuwa na watu wanne

1.TRACER-huyu anamfatilia mlengwa anayetakiwa kuuawa

2.TRANSPOTER-huyu anaiongoza timu ya wauaji kwa mlengwa huyo anayetakiwa kuuawa

3.HELPER-huyu anaendesha pikipiki, anakuwa amembeba muuaji

4.KILLER-huyu ndio muuaji hasa, anafyatua risasi au kurusha magetic bomb kwa target(hili bomu linaweza kumuua mlengwa tu huku wengine wakijeruhiwa)

Unaambiwa huyu shooter anauwezo wa shoot accurately katika speed yeyote bila kupepesuka hata kidogo yani hakuna hata kutingishika akilenga mwendo kasi wowote ule bila kukosa au kurusha bomu likanasa katika sehemu ya gari anayotaka linase sehemu ambapo mara nyingi huwa ni upande wa gari aliokaa mlengwa na kitendo hiki huwa cha haraka sana kiasi wahusika huwa ngumu kutambua kama kuna kitu kimewekwa au kurushwa kwenye gari. Mtindo huu ndio 'Trade Mark' ya mauaji ya KIDON

haya ni machache katika yale machache,mengi kuhusu kitengo hiki. Kwa machache zaidi vitabu hivi ni vizuri; GIDEON'S SPIES: The inside story of Israel legendary secret service by Gordon Thomas na SPIES AGAINST ARMEGEDDON: Inside Israel's secret wars by Dan Raviv and Yossi Melman .
Vitabu viko hapo chini nime attach

Karibuni mwenye elimu zaidi kuhusu KIDON

 
Kwa nguvu waliyonayo was isirael ilitakiwa mpk as kusiwepo ht mparestina ht mmoja lkn nusra ya mungu ndio inawaweka mpk leo
 
Back
Top Bottom