Hawa jamaa ni noma sana. Ndio waliotumika kuua wale wote waliohusika na utekaji nyara na kuuawa kwa wanamichezo wa Israel kwenye mashindano ya Olympic ya Munich, Germany mwaka 1972. Movie ya "Munich" inahusu suala hilo. Pia Kitabu cha Lillehammer Affair kinasimulia jinsi Kidon kwa kushirikiana na vitengo vingine vya MOSSAD walivyomsaka na kisha kumuua kimakosa Ahmed Bouchiki huko Lillehammer, Norway wakidhani ni mastermind wa Olympic Massacre Ali Hassan Salameh.
Mara ya mwisho hawa jamaa kusikika kwenye vyombo vya habari ni pale walipoenda Dubai kama watalii kutoka nchi mbalimbali na kumuua Ofisa wa ngazi ya juu wa Hamas Mahmoud Al-Mabhouh kwenye chumba cha Hoteli aliyofikia. Kamera za Usalama za Uwanja wa ndege ziliwaonyesha toka wanawasili Dubai. Kamera za Hotelini zliwaonyesha tangu wakiwasili hotelini hapo mpaka wauwaji walipokuwa wakiingia kwenye chumba cha bwana Mabhouh na kutoka baada ya kumaliza kazi wakiwa wameshika tennis rackets wakipozi kama vile wanaenda kucheza tennis.
Ulitokea mtafaruku mkubwa wa kidiplomasia kwani majasusi hao wa Israel walisafiri kwa kutumia passport za nchi mbalimbali kama Australia, Belgium, Italy,Sweden n.k. Israel kama kawaida yao wakawa ambiguous (hawakukubali wala hawakukanusha).