KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

KIDON, unawajua hawa? The deadliest killing machine

Yes.......unazijua unifundishe........

Jinsia yenu ni wazuri zaidi linapokuja suala la ujasusi. Kazana japokuwa sijui nani atakuhire!! Maana ujasusi ni report based task. Ujasusi ni unit,ujasusi si ujambazi wala umafia,ujasusi ni special task always granted.
 
mkuu mngony asante sana kwa kuitafsiri habari hii ya kidon na kuiweka ktk lugha yetu adhimu ya kiswahili.hata sisi tusiolewa kizungu tumeelewa.
 
Last edited by a moderator:
Ndahani,
i too,real need that book,allow me to PM you my email address.
 
Last edited by a moderator:
mkuu mngony asante sana kwa kuitafsiri habari hii ya kidon na kuiweka ktk lugha yetu adhimu ya kiswahili.hata sisi tusiolewa kizungu tumeelewa.

Nashkuru wakunyumba, tunajifunza funza hivo hivo kidogo kidogo kadoda11
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nilichojifunza kwenye moja ya vitabu ulivyoambatanisha hapo ni kwamba mabalozi wa Israel wengi/wote na maafisa wote/wengi wa balozi zao wanakuwa na kazi maalumu za mashirika yao ya kijasusi na hii imekuwa moja kati ya nguzo muhimu za historia ya mafanikio ya MOSSAD. Swali ninalo jiuliza mpaka sasa ni je, nchi yetu inatumia utaratibu wa aina hii katika kutuma mabalozi katika nchi mbalimbali? Kwa maoni yangu ni kwamba itakuwa rahisi sana kulinda na kutetea maslahi ya Tanzania na watanzania kama kila afisa ubalozi wetu atakuwa katumwa kwa mfumo huu. mfano, haitawezekana kabisa kwa kampuni ya kigeni yenye nia ovu kupata fursa ya uwekezaji Tanzania kwa vile taarifa zao na malengo yao yatakuwa mezani kwetu muda mrefu kabla ya wao kutia miguu kwenye nchi yetu. Just thinking loudly.
 
Mkuu huu mfumo nchi nyingi sana unautumia.Kuanzia Marekani mbaka Tanzania

Ubalozi wa Tanzania unakuwaga na muambata wa kijeshi na yule wa kiusalama.Mara nyingi first au second secretary ndo anakuwaga afisa wa Idara ya Usalama wa taifa! Wako chini ya Directorate of External Operations

Pamoja mkuu
 
Na je ile dhana ya wafanyakazi wa ikulu lazima wote wawe wanausalama ni kweli? apakak
 
Last edited by a moderator:
Na je ile dhana ya wafanyakazi wa ikulu lazima wote wawe wanausalama ni kweli? apakak

Wale wafanyakazi permanent wote wa Ikulu lazima wawe Usalama or atleast wamepitia kozi flani ya usalama ya kutunza siri

Na pia hadi code word ya mfanyakazi wa Usalama mara nyingi anajiita mfanyakazi wa Ikulu au wa Ofisi ya Raisi. Waziri Mkuu Pinda ni mfano hai,anasema amefanyakazi Ikulu kumbe ni Usalama
 
komandoo wetu anaenda mafunzo kwa mda gani tena vileee?

sasa hao masela wanaenda tizi kwa miaka miwili tena sio tizi tu ni lile tizi la hatari, aargghhh potelea mbali bora niishie kuruta tu nistaafu :A S cry:
 
KIDON ni kitengo ndani ya Mossad chenye jukumu la kufanya assasination dhidi ya wale wenye kuhatarisha usalama wa Israel. KIDON ndio wanaosifika na kuogopwa sana duniani katika kufanya assasination kwa ufanisi na ufasaha wa hali juu

neno Kidon ni la kiyunani lenye maana ya ncha ya upanga, hili lina akisi jinsi kitengo hicho kilivyomahiri na hatari katika kufanya mauaji.

Kidon ilianzishwa miaka ya 70 kutoka katika kitengo cha Caesaren kilichokuwa chini ya Mossad kufuatia kuuawa kwa waisrael 11 waliokuwa washiriki katika mashindano ya Olympic mjini Munich Ujerumani mwaka 1972. mauaji hayo yalifanywa na wapiganaji wa kipalestina, japo waisrael wengi walikufa wakati polisi wa Ujerumani walivyojaribu kuwaokoa mateka. na mara moja baada ya kuundwa wakapewa kazi ya kuua kila aliyehusikia na mauaji hayo ya waisreal kazi iliyofanyika kwa mafanikio japokuwa kuna wahanga nao walikufa

mbali ya kuwa kitengo hiki kuwa chini ya Mossad lakini kutokana na usiri wake mkubwa hakina ofisi ndani ya makao makuu ya Mossad mjini Tel Aviv. hata ma-agent wake ni vigumu kutia mguu makao makuu, hii ni kwa mujibu wa afisa wa zamani wa intelijensia katika kitengo cha Mossad kinachoratibu shughuli za Kidon bwana Mishka Ben-David katika kitabu chake "Duet in Beirut". anaendelea kusema kuwa hata majina wanayotumia ni majina ya kufikirika na si majina ya rasmi, na wakiwa shughulini hutumia jina la 3 la mhusika na mara nyingine hadi utambulisho wa 4 na wa 5. kutoka na usiri na ufanisi wa hali ya juu, kitengo hiki kimepachikwa jina la Mossad ndani ya Mossad

recruitment katika kitengo hichi ni kutoka katika special forces wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya Israel Defence Force (IDF) na hupatiwa mafunzo ya hatari kwa mda wa miaka 2. hawa jamaa wanasifika kwa kutoacha alama yeyote katika assasinations zao na wamekuwa wakifanikiwa kwa miaka mingi

assasinators hutumia pasi na nyaraka feki za mataifa mbalimbali za kusafiria zilizofojiwa kwa ustadi wa hali ya juu na wataalamu wao.pia hutumia pasi halisi za mataifa mbalimbali ambazo picha hubadilishwa kiutaalamu ili kufanana na mhusika.pia wanauwezo mkubwa sana wa ku-infiltrate nchi yeyote na kufanya assasinations.

katika assasination wanazozifanya mashariki ya kati, style maarufu ni ile ya wauaji wakishambulia huku wakiwa wamepanda pikipiki. style hii ndio imetumika kuwauwa maprofesa na wanasayansi wa nyuklia wa4 wa Irani mpaka sasa. kama kawaida timu ya wauaji inakuwa na watu wa4

1.TRACER-huyu anaitrace target

2.TRANSPOTER-huyu anaiongoza timu ya wauaji kwa target yao

3.HELPER-huyu anaendesha pikipiki, anakuwa amembeba muuaji

4.KILLER-huyu ndio muuaji hasa, anafyatua risasi au kurusha magetic bomb kwa target(hili bomu linaweza kumuua targert tu huku wengine wakijeruhiwa)

unaambiwa huyu shooter anauwezo wa shoot accurately katika speed yeyote bila kupepesuka hata kidogo yani hakuna hata kutingishika akilenga mwendo kasi wowote ule,au kurusha bomu likanasa katika sehemu ya gari anayotaka linase na asionekane

haya ni machache katika yale machache mengi kuhusu kitengo hichi. kwa machache zaidi vitabu hivi ni vizuri; GIDEON'S SPIES: The inside story of Israel legendary secret service by Gordon Thomas na SPIES AGAINST ARMEGEDDON: Inside Israel's secret wars by Dan Raviv and Yossi Melman hiki ninacho ntaki upload. nimejaribu network inasumbua

karibuni mwenye ujuzi zaidi kuhusu hiki kitengo

Ni ya ukweli sana,mzee inatishaaa.Thanks for your Information
 
Hii nimeonaga sehemu walihis ndo wamesepa na ile air malysia nkawasielew ndo
Kina nan hao
 
Kuna Movie iliyoongozwa na Steven Spielberg ambayo amecheza Eric Bana, Daniel Craig na wengineo inaitwa Munich ambayo inaelezea namna walivyoweza kulipiza kisasi kwa wanamichezo wa Olympic waliouawa kule Munich Ujerumani. Hii ilikuwa ni wakati wa Utawala wa Golder Meir kule Israel.
 
Mkuu huu mfumo nchi nyingi sana unautumia.Kuanzia Marekani mbaka Tanzania

Ubalozi wa Tanzania unakuwaga na muambata wa kijeshi na yule wa kiusalama.Mara nyingi first au second secretary ndo anakuwaga afisa wa Idara ya Usalama wa taifa! Wako chini ya Directorate of External Operations

Pamoja mkuu

Ahsante sana mkuu.
 
Wakuu hivi kuna vitabu au nyaraka zozote ambazo zinapatikana (kihalali) kuhusu matendo makubwa yaliyowahi kufanywa na idara yetu ya usalama kama ilivyo kwa MOSSAD (kwa vitabu vilivyo ambatanishwa na mleta hoja)? Kwa kiwango fulani naona kama upatikanaji wa baadhi ya taarifa au nyaraka ( kwa watu sahii) unaweza kuwa na mchango mkubwa sana wa kukuza uzalendo na utayari wa kuchangia kwa hali na mali kwenye ulinzi wa Taifa letu.
 
natamani waje tanganyika wafanye japo opareshen kama 10 tu za elimination nadhan nchi itapata heshima iliyopotea maana tanganyika yangu sasa ni kama shamba la bibi au kichwa cha mwenda wazimu
 
Back
Top Bottom