KIDON ni kitengo ndani ya Mossad chenye jukumu la kufanya assasination dhidi ya wale wenye kuhatarisha usalama wa Israel. KIDON ndio wanaosifika na kuogopwa sana duniani katika kufanya assasination kwa ufanisi na ufasaha wa hali juu
neno Kidon ni la kiyunani lenye maana ya ncha ya upanga, hili lina akisi jinsi kitengo hicho kilivyomahiri na hatari katika kufanya mauaji.
Kidon ilianzishwa miaka ya 70 kutoka katika kitengo cha Caesaren kilichokuwa chini ya Mossad kufuatia kuuawa kwa waisrael 11 waliokuwa washiriki katika mashindano ya Olympic mjini Munich Ujerumani mwaka 1972. mauaji hayo yalifanywa na wapiganaji wa kipalestina, japo waisrael wengi walikufa wakati polisi wa Ujerumani walivyojaribu kuwaokoa mateka. na mara moja baada ya kuundwa wakapewa kazi ya kuua kila aliyehusikia na mauaji hayo ya waisreal kazi iliyofanyika kwa mafanikio japokuwa kuna wahanga nao walikufa
mbali ya kuwa kitengo hiki kuwa chini ya Mossad lakini kutokana na usiri wake mkubwa hakina ofisi ndani ya makao makuu ya Mossad mjini Tel Aviv. hata ma-agent wake ni vigumu kutia mguu makao makuu, hii ni kwa mujibu wa afisa wa zamani wa intelijensia katika kitengo cha Mossad kinachoratibu shughuli za Kidon bwana Mishka Ben-David katika kitabu chake "Duet in Beirut". anaendelea kusema kuwa hata majina wanayotumia ni majina ya kufikirika na si majina ya rasmi, na wakiwa shughulini hutumia jina la 3 la mhusika na mara nyingine hadi utambulisho wa 4 na wa 5. kutoka na usiri na ufanisi wa hali ya juu, kitengo hiki kimepachikwa jina la Mossad ndani ya Mossad
recruitment katika kitengo hichi ni kutoka katika special forces wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya Israel Defence Force (IDF) na hupatiwa mafunzo ya hatari kwa mda wa miaka 2. hawa jamaa wanasifika kwa kutoacha alama yeyote katika assasinations zao na wamekuwa wakifanikiwa kwa miaka mingi
assasinators hutumia pasi na nyaraka feki za mataifa mbalimbali za kusafiria zilizofojiwa kwa ustadi wa hali ya juu na wataalamu wao.pia hutumia pasi halisi za mataifa mbalimbali ambazo picha hubadilishwa kiutaalamu ili kufanana na mhusika.pia wanauwezo mkubwa sana wa ku-infiltrate nchi yeyote na kufanya assasinations.
katika assasination wanazozifanya mashariki ya kati, style maarufu ni ile ya wauaji wakishambulia huku wakiwa wamepanda pikipiki. style hii ndio imetumika kuwauwa maprofesa na wanasayansi wa nyuklia wa4 wa Irani mpaka sasa. kama kawaida timu ya wauaji inakuwa na watu wa4
1.TRACER-huyu anaitrace target
2.TRANSPOTER-huyu anaiongoza timu ya wauaji kwa target yao
3.HELPER-huyu anaendesha pikipiki, anakuwa amembeba muuaji
4.KILLER-huyu ndio muuaji hasa, anafyatua risasi au kurusha magetic bomb kwa target(hili bomu linaweza kumuua targert tu huku wengine wakijeruhiwa)
unaambiwa huyu shooter anauwezo wa shoot accurately katika speed yeyote bila kupepesuka hata kidogo yani hakuna hata kutingishika akilenga mwendo kasi wowote ule,au kurusha bomu likanasa katika sehemu ya gari anayotaka linase na asionekane
haya ni machache katika yale machache mengi kuhusu kitengo hichi. kwa machache zaidi vitabu hivi ni vizuri; GIDEON'S SPIES: The inside story of Israel legendary secret service by Gordon Thomas na SPIES AGAINST ARMEGEDDON: Inside Israel's secret wars by Dan Raviv and Yossi Melman hiki ninacho ntaki upload. nimejaribu network inasumbua
karibuni mwenye ujuzi zaidi kuhusu hiki kitengo