Kidonda kina siku 12 hakikauki na kupona, natumia dawa

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habari wakuu

Nina kidonda kwenye kidole kina siku 12, nilikipata baada ya kwenda kutibiwa Bawasiri clinic za Wakorea.

Unakiwekea dawa ya kuchoma moto ktk kidole mara Saba nichome kwa siku tano mfululizo Kila siku mara Saba.

Unaweka dawa ktk kidole hapo Kisha inachomwa inaungulia kidolea hadi iishe. Ilichomwa siku moja tu nikakataa kurudia Tena.

Sasa eneo hilo limeacha kidonda sasa naona hakiponi maana nilikuwa siweki dawa ya aina yoyote, mpaka kufika juzi nikaenda hospitali wakanipa dawa ya FLUCAMOX na tupe ya MUPIROCIN OINTMENT bp 2%

Leo siku ya tatu Sasa kidonda kama kinataka kukauka ila kinakua na usaha kidogo

Wakuu nauliza Kuna dawa ya kukausha kidonda?

IMG_20241110_200742.jpg
 
Habari wakuu

Nina kidonda kwenye kidole kina siku 12, nilikipata baada ya kwenda kutibiwa Bawasiri clinic za Wakorea.

Unakiwekea dawa ya kuchoma moto ktk kidole mara Saba nichome kwa siku tano mfululizo Kila siku mara Saba...
Mh, pole sana.

Sijaelewa maelezo yako kwamba ulipata baada ya matibabu ya bawasiri, halafu kuna nini unachoma sijui inaungilia?

Ili kidonda kipone ni lazima kiwe kisafi na uchafu usiingie ndani yake. Ni lazima kukisafisha na kukifunika kwa pamba safi na salama.

Wakati kinasafishwa kuna dawa za kumeza utapatiwa ili kusaidia kidonda kupona na kukaa vizuri. Kwa hiyo kama mwanzoni hakuna dawa za kumeza au hakikuwa kikisafishwa inawezekana ndiyo maana kimekaa muda wote huo bila kupona.

Kwa hiyo ni muhimu kwenda kituo cha afya/hospitali kusafishwa na kuendelea na dawa ulizopewa na daktari.

NB: Kuwa makini si kila kidonda kinasafishwa kwa spirit

Kila la kheri.
 
Habari wakuu

Nina kidonda kwenye kidole kina siku 12, nilikipata baada ya kwenda kutibiwa Bawasiri clinic za Wakorea.

Unakiwekea dawa ya kuchoma moto ktk kidole mara Saba nichome kwa siku tano mfululizo Kila siku mara Saba.

Unaweka dawa ktk kidole hapo Kisha inachomwa inaungulia kidolea hadi iishe. Ilichomwa siku moja tu nikakataa kurudia Tena.

Sasa eneo hilo limeacha kidonda sasa naona hakiponi maana nilikuwa siweki dawa ya aina yoyote, mpaka kufika juzi nikaenda hospitali wakanipa dawa ya FLUCAMOX na tupe ya MUPIROCIN OINTMENT bp 2%

Leo siku ya tatu Sasa kidonda kama kinataka kukauka ila kinakua na usaha kidogo

Wakuu nauliza Kuna dawa ya kukausha kidonda?

View attachment 3151499
Hivi kukichoma kidonda inakuwaje au inafanyikaje?

Sijaelewa hapo lakini kidonda kinahitaji kusafishwa tu na kupakwa dawa kama zipo za kupakwa na kukifunika kwa pamba au kitambaa kisafi basi kinapona na kukauka chenyewe.
 
Anachoma..... hio ni njia ya zamani sana ili kuua bacteria
 
Back
Top Bottom