Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 327
- 537
Mh!Anachoma..... hio ni njia ya zamani sana ili kuua bacteria
Basi ndio maana hakijapona mpaka leo siku 12, bacteria hawauwawi kwa kuchoma bali kwa dawa za kupaka au za kumeza.
Ukikichoma ina maana unaweka jeraha jipya na hata uchafu unaingia. Hata kinapokauka haishauriwi kulibandua lile gamba mapema kabla halijaanza kujiachia lenyewe.
Kama mbinu hiyo ya kuchoma ndiyo anayoitumia (kukichoma) kwa kweli safari itakuwa ndefu sana. Hakuna haja ya kukichoma ni usafi tu ndiyo ilihitajika basi, lakini kwa sasa inabidi akisafishe na kupaka hiyo dawa aliyopewa na kukifunika kwa pamba safi wala asisumbuke kuchoma.