Kiepe kimeisha, faida 10! Nakosea wapi?

Kiepe kimeisha, faida 10! Nakosea wapi?

Kumbe unachomoa halaf unauliza nn sasa
Sasa mkuu, kwan faida inakata kwa kutumia tu elf 5 ya kula kwa siku!!? Kwan hao wanoiona faida huwa wanaiona kabla hawajakata ya kula? Kula lazima aisee
 
Endelea kula mkuu ipo cku utatupa mrejesho mpya
 
Ukiwa mfanyabiashara lazima ujue hela ya biashara ni ya biashara tuu,.kama unatumia hela ya biashara kula,kuvaa,vocha,sijui usafiri n.k huwezi kuiona faida ya hiyo biashara,..lazima uwe serious kidogo na kitu unachokifanya.
sasa ndio biashara hio unayoitegemea kuendeshea maisha yako ...sio kwamba utumie mtaji bali kafaida unayopata ikusaidie sasa utafanyaje yan ukipata faida usile usivae ukiumwa usiende hospitali, usinunue mboga ya kupika, usinunue sabuni ya kuogea, yatakua maisha gani sasa hayo yani unajidhoofisha kisa biashara iende vizuri...healthy life is everything
 
afate huu ushauri,mimi pia yalinkuta mtaji wa laki 8 naondoka na jero faida kwa sikunikatumia njia iyo ikansaidia maana vijana wezi sana wanauza wanasema hawauzi,hata tray za mayai zinaisha wanakuambia hatujauza mayai yalienda wapi sijui,nikatimua nikaweka wingine kwa makubaliano hayo na tukafikia lengo na soda maji wakawa wananiuzia
safi
 
sasa ndio biashara hio unayoitegemea kuendeshea maisha yako ...sio kwamba utumie mtaji bali kafaida unayopata ikusaidie sasa utafanyaje yan ukipata faida usile usivae ukiumwa usiende hospitali, usinunue mboga ya kupika, usinunue sabuni ya kuogea, yatakua maisha gani sasa hayo yani unajidhoofisha kisa biashara iende vizuri...healthy life is everything
Sidhani yy kama amezungumzia kutumia faida,.kasema "anachomoa kwa ajili ya kula" n.k...sasa hela yaku run business ukiichomoa chomoa faida utaionaje???lazima faida itakuja tofauti na vile ulivyotegemea,.lazima iwepo plan ya kuendesha biashara na ifuatiliwe.
 
Mkuu, mtaji ni 1 Mil. Hyo ni aggregate ikijumuisha kodi ya frame na vitendea kazi ila nimeanza na viazi nusu gunia la 50, 000/- ili kucheck upepo. Tatizo ndo hapo sasa hicho kigunia kinachukua 6 days kuisha
Mwanzo mgumu sana, baadae wateja watazoea na biashara itachangamka na kupata hela nzuri tu, kuwa mvumilivu
 
Aise! Hii yako ni point ya kuizingatia sana. Kijana wangu kasukuma siku6 kumaliza kigunia cha ndoo 4 na kishtobe, mweh!
Nadhan ndo tatizo lilipo, mzunguko mdogo

Mzunguko ni mdogo kwasababu unauza chips mayai tu, chips kavu zinauzika sana kuliko kiepe. Inakubidi uongeze mishkaki, kuku, firigisi hii inakusaidia kuwa na aina mbalimbali.
 
Endelea kula mkuu ipo cku utatupa mrejesho mpya
Labda unipe ushauri boss, me natumia elfu 5 kwa chakula tu na si mambo mengine. Kama unashinda hapo 'golini' mpaka night, issue ya msos unasolve vp ingekuwa wewe?
Me nlivyokuelewa ni kwamba, nkae njaa ndo ntaiona faida
 
Sidhani yy kama amezungumzia kutumia faida,.kasema "anachomoa kwa ajili ya kula" n.k...sasa hela yaku run business ukiichomoa chomoa faida utaionaje???lazima faida itakuja tofauti na vile ulivyotegemea,.lazima iwepo plan ya kuendesha biashara na ifuatiliwe.

Natumia sehem ya faida (si mtaji) kula/msos na ndo baada ya kuendesha hiyo biashara kwa siku 6 najikuta sina faida mkonon zaidi ya mtaji. So me shauku yangu kubwa ni kufaham nakosea wapi mpaka nashindwa kupata zaid ya ile ya msos?
 
Labda unipe ushauri boss, me natumia elfu 5 kwa chakula tu na si mambo mengine. Kama unashinda hapo 'golini' mpaka night, issue ya msos unasolve vp ingekuwa wewe?
Me nlivyokuelewa ni kwamba, nkae njaa ndo ntaiona faida
Fanya hivi tafuta kiroba chenu cha unga hapo ikifika mida ya msosi mna jipikia ugari wenu mna piga msosi kwa kiroba cha kilo tano naimani kita wasukuma sana na bajeti baada yako ya siku baada ya kuwa 5000 ita anza soma 2000 tu..
 
Natumia sehem ya faida (si mtaji) kula/msos na ndo baada ya kuendesha hiyo biashara kwa siku 6 najikuta sina faida mkonon zaidi ya mtaji. So me shauku yangu kubwa ni kufaham nakosea wapi mpaka nashindwa kupata zaid ya ile ya msos?
Mkuu mimi nimekuelewa ,hiyo biashara sio kwamba haina faida ila faida unakula maana kama una kula kwa siku 5000 inamana kwa siku hizo 6 inamana ni 30000 alfu unakula ukijumlisha na hiyo 10000 inamana faida yako 40000 ,

sasa cha msingi cha kukushauri ili uwendelee kupata hela ya kula na yakuweka iongezeke ,kuza mtaji kwa kuongeza na vitu vingine mfano mishikaki kuku samaki na makorombwezo mengine faida itaongezeka maana unavyanzo vingi vya kupatia
 
Fanya hivi tafuta kiroba chenu cha unga hapo ikifika mida ya msosi mna jipikia ugari wenu mna piga msosi kwa kiroba cha kilo tano naimani kita wasukuma sana na bajeti baada yako ya siku baada ya kuwa 5000 ita anza soma 2000 tu..
Shukrani sana, nitaufanyia kazi ushauri huu pia
 
Mkuu mimi nimekuelewa ,hiyo biashara sio kwamba haina faida ila faida unakula maana kama una kula kwa siku 5000 inamana kwa siku hizo 6 inamana ni 30000 alfu unakula ukijumlisha na hiyo 10000 inamana faida yako 40000 ,

sasa cha msingi cha kukushauri ili uwendelee kupata hela ya kula na yakuweka iongezeke ,kuza mtaji kwa kuongeza na vitu vingine mfano mishikaki kuku samaki na makorombwezo mengine faida itaongezeka maana unavyanzo vingi vya kupatia
Asante sana mkuu kwa udadavuzi wako. Hakika nmepata la msingi
 
Biashara ya kiepe ina faida pamoja na changamoto zake mm kwenye goli rangu naenda chukua salio rangu tu kila jioni lakini kijana niliye muweka golini nae ame ajri mtu mwingine wa kumsaidia kazi wana lipanaje mm sijui cha muhimu kwenye hela yangu na yeye tuliyo kubaliana haitingishwi.. Komaa ndugu na mtangulize Mungu mbele hakuna biashara rahisi hata moja
 
  • Thanks
Reactions: Mj1

Aisee, poa poa boss wangu
 
Back
Top Bottom