Kifahamu kikundi cha udukuzi mtandaoni kiitwacho Anonymous Hackers mwanzo mwisho

Kifahamu kikundi cha udukuzi mtandaoni kiitwacho Anonymous Hackers mwanzo mwisho

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
SALUTE
FB_IMG_15749495666303628.jpg

Inafahamika kua Tanzania ni moja kati ya nchi zenye amani na uhuru duniani, hii inatufanya

Kujitamba na kutembea kifua mbele ya mataifa mengi hasa ya Afrika kua tuna amani na furaha
zaidi katika nchi yetu. Lakini kitu kimoja kikubwa ambacho tunakosea watanzania ni kuwa
tunachanganya kukaa kimya na Amani. Tuna amani na uhuru sawa but deep down watanzania
tumechagua kukaa kimya na kujifanya vipofu katika mambo ambayo tunaona hayafai, ukimya huo ndio unatufanya tuonekana amani ipo ya kutosha.

Kwangu siwezi kusema kua ni Kukaa kimya bali ni uoga na unafiki wetu wenyewe, tumechagua kua vipofu wakati macho tunayo, tumechagua kua mabubu lakini midomo na uwezo wa kuongea tunao, sijui ndivyo tulivyochagua au ndivyo tulivyofanywa tuwe hivi toka miaka ya nyuma. Kwa nchi za wengine watu wake hua hawakubali kukaa kimya, watatoka nje hata kama nikutumia nguvu watatumia ili mawazo na hisia zao ziwafikie walengwa.....lakini kuna wengine hawana uwezo au ujasiri wa kwenda barabarani kuwasilisha hoja zao ila wameamua kutumia

Keyboard ya computer kama silaha kuu ya kupambana na kuonyesha madudu/maovu ya
serikali au taasisi mbalimbali....

Kama huwezi kimbia tembea, kama huwezi tembea tambaaa ilimradi usiache kusonga mbele. So kwakua wengine hawana uwezo wa kupambana watu wameamua kutumia kibodi kama silaha.

Kupitia hili makundi mbalimbali ya wanaofanya mashambulizi ya kimtandao (Wadukuzi)
yamekua yakijitokeza karibia duniani kote, achana na wapuliza filimbi (Whistleblowers) kama
wakina Edward Snowden, Mark Felt, Daniel Ellsberg, Kathryn Bolkovac nk hapa nazungumzia

Makundi ya wadukuzi kama lulzSec, Black hat hackers, Anonymous Hackers, Lizard squad, Legion
of doom,nk. but hapa tutazungumzia kikundi maarufu zaidi cha udukuzi duniani kinachojiita
Anonymous Hackers.

Kwanza kabisa ili kukifahamu hiki kikundi chimbuko lake inabidi turudi nyuma miaka kama 400 iliyopita ili tupate mtiririko mzuri wa historia.

Siku ya April 13 mwaka 1570 katika eneo la stonegate jijini York England katika familia ya bwana Edward Fawkes na bibi Edith Fawkes alizaliwa mtoto wa kiume wakamwita Guy Fawkes. Wazazi wa Guy walikua ni waumini wazuri tu wa kanisa la England ambalo sasa unaweza liita kanisa la Anglikana, familia ya upande wa mama yake Guy walikua ni Recusant Catholics (hawa ni wakatoliki waliokataa kuwa waanglikana huko england,wales au ireland). Pia binamu ya aliyeitwa Richard Cowling alikua ni padri wa shirika la Jesuit.

Akiwa na miaka 8 baba yake alifariki kisha mama yake akaolewa na mwanaume aliyeitwa Denis Baynbridgge ambae alikua ni mkatoliki, hivyo kupitia huyu baba yake mpya Guy Fawkes alibatizwa na kua Mkatoliki. Mwaka 1591 Guy aliuza kiwanja chake cha urithi kisha akasafiri kwenda
kupigana vita ya Eight Years War ambayo ilikua inapiganwa na wakatoliki huko Hispania.

Mwaka 1604 Guy alikua anajihusisha na kikundi kidogo cha wakatoliki wa uingeleza kupambana na wazushi/Protestant kilikua kinaongozwa na bwana Robert Catesby lengo lao kuu lilikua ni
kumuua Kiongozi wa Protestant King James mfalme wa uingeleza yule aliyetafsiri biblia huko uingereza na kuweka kila
sehemu yenye jina jacob akaweka jina lake James. Yeye na wenzake walipanga mpango
unaojulikana kama Gunpowder Plot....Walienda kupanga vyumba karibu na kasiri kisha
wakaenda kupandikiza madebe 36 yenye unga wa risasi katika jumba la mfalme.Lakini huo
mpango uligundulika mapema na Guy Fawkes alikamatwa .

November 5, 1605, aliteswa sana ndio akataja majina ya wenzake. Fawkes alihukumiwa kunyongwa katika jengo la bunge lakini aliruka kutoka juu akavunja shingo na kufa. Ukawa mwisho wake! Kila mwaka November 5 hua ni siku ya kusherehekea siku ya huyu Guy huko kwa malkia kwa kuchoma baruti na kuva vinyago vyenye sura ya Guy Fawkes.

Bado tupo kwenye mada inayohusu Chimbuko la Anonymous Hackers usisahau..nimetaja hayo
makanisa na vita ili tuelewane vizuri huko mbele..

Mwaka 1982 mwandishi Alan Moore aliandika Novel inaitwa V for Vandetta amabayo ilikua inamuhusu muhisika anayeitwa V ambae alikua na sura ya tabasamu musatachi mpana ambao umepanda kwa juu mwishoni na ndevu nyembamba zilizoshuka chini. Kiuhalisia huo ndio ulikua mwonekana wa Guy fawkes, lengo lake huyo V ilikua ni kufanya mapinduzi kwa kuungusha mfumo wa Fascist. Mwaka 2005 Warner bros. walitoa muvi kuhusu novel hii ya V for Vandetta.

Mwanzo wa Kundi la Anonymous Hackers October 1, 2003 Christopher Poole akiwa na miaka 15 alizindua site yake aliyoiita 4Chain.net, site hii ilikua ni imageboard forum ambapo watu walikua wanapost picha na kufanya
mazungumzo humo kama hapa JF . Poole alitengeneza site ili kushindana na Imageboard nyingine iliyokua Japan inayoitwa 2Chain iliyotengenezwa na Futaba Channel. Poole alichukua
Source code za futaba channel kisha akazitafsiri kutoka lugha ya kijapani kwenda kingereza na
kutengeneza 4chain kisha akaanza kuwaalika watu kutembelea site yake.

Sasa ilikua hivi huko kwenye 4chain.net kuna watembeleaji walikua wanapost comments bila
adminstrator kufahamu taarifa za mtoa comment hivyo watembeleaji wa namna hiyo kwa chini
kulikua na jina Anonymous kumaanisha taarifa za muhisika hazijulikani. Mwaka 2004 sasa
adminstrator wa 4chain.net bwana Poole alileta protocal ya "Forced_Annon" ambapo post zote
kwenye site hiyo zilikua zina hiyo status ya anonymous. Mara nyingi watumiaji wa huu mtandao
wa 4chain walikua wanavamia mitandao mingine wakiwa na Avatar moja ya anonymous na
kuifanya ishindwe kutoa huduma (Cyber Attack).

Mfano mwaka 2006 members wengi wa 4chain walivamia mtandao wa kijamii unaoitwa Hobbo wakafanya watumiaji kushindwa kuupata
hewani huu mtandao..Yaani kwa mfano sisi member wa JF tuvamie mtandao wa kanyatalk
tukiwa na utambulisho wa aina moja na kufanya mtandao huo watumiaji wake wasiweze kuupata hewani.
FB_IMG_15749494826018109.jpg

Guy Fawkes

Itaendelea.....
Yours
Vers

NB.
Heshimuni mamlaka na serikali zilizopo madarakani. Ukikosoa kosoa kwa heshima na Ustaarabu... Sio kisa ni haki yako kuongea basi uongee na yasiyo faa katika sehemu na muda usiofaa
 
Protest_ACTA_2012-02-11_-_Toulouse_-_05_-_Anonymous_guy_with_a_scarf.jpg

Tom Cruise sidhani kama ni jina geni kwa watu wengi humu, muigizaji wa muvi za mission imposible, huyu jamaa ana mchango mkubwa katika kuenea kwa kundi la Anonymous hackers....Tom cruise ni muumini wa imani inayoitwa Church of Scientology waamini wa kanisa hili wanaamini katika tafiti za mambo ya dini na sayansi. Kulikua na blog ambayo ilikua inajihusisha kutoa umbea au zile za chini ya kapeti za mastaa kama yale magazeti ya shigongo ulioitwa Gawker, ulikua maarufu sana na unatembelewa na wengi..

Basi January 15 mwaka 2008 huu mtandao ulipost video ya mwigizaji Tom Cruise akilisifu hili kanisa/imani yake alikua anasema kua "We (Scientology church) are the authorities on getting
people off drugs, we are the authorities on mind, we can rehabilitate criminals..We can bring peace and unit Communities" ndani ya muda mfupi video ilikua imetembelewa na watu wengi huko YouTube napo na mitandao mingine video iliwekwa watu wakawa wanaongea vibaya kuhusu hilo kanisa na video hiyo ya Tom Cruise. Viongozi wa hilo kanisa wakawahimiza Youtube na mitandao mingine ya video kuondoa hiyo video mara moja ila Gawker waligoma.

Kitendo cha kuhimiza mtandao wa youtube kuondoa hiyo video ndio kiliwachukiza Anonymous waliona kama ni kitendo cha kuwazuwia watu wasizungumze au kuonyesha maovu yaliyopo kwenye taasisi au mashirika hivyo wakaanza kushambulia online websites za kanisa hilo, walizizima kabisa website kwa muda Walitumia DDoS attack. DDoS attack ni kifupi cha Distributed Denial of Sevice Attack ambapo mdukuzi bua anatumia zaidi ya IP Addres kufanya website husika kua bize muda mwingimoja ambazo zinafanana Kampeni zikaanza facebook na
youutube kwenda nje ya viunga vya kanisa hilo popote lilipo kuanzia miji ya Edinburg, Manchester, York, Brimingham.. Annonymous walikusanyika nje ya kanisa la Church of scientology wakiwa wamevalia Vinyago vyenye sura ya Guy Fawkes ambayo ilichorwa kwenye novel ya V for Vandetta. TUkumbuke kua Guy Fawkes alikua anapambana na makanisa ya namna hii hivyo kwa kumuenzi anonymous hacker walitumia mask ya ya sura yake iliyochorwa kwenye novel ya V for Vandetta

So kuanzia kwenye tukio hilo Annonymous wakaanza kufanya DDoS attack au udukuzi katika serikali, mashirika ya kiserikali, taasisi za kifedha nk. Mpaka sasa Anonymous Hackers limekua ni kikundi cha udukuzi kilochoenea pote duniani na kila mtu anaweza kujiunga.

Je utajiunga vipi nawe uwe sehemu ya mabadiriko katika dunia?

Kwanza fahamu kikundi hiki hakina makao makuu na hawatambuani wote labda hua wanakutana kimya kimya kama member wa JF kwa njia wanazojua wao, hawana vitambulisho kitu kitakacho kufahamisha kua wewe ni member ni kuvaa ile mask yenye sura ya Guy Fawkes inayofahamika kama Anonymous hackers mask. So kama unahitaji kujiunga wewe agiza online hiyo mask kisha chagua kitu unachotaka kufanya sehemu ulipo kwenye upande wa udukuzi elimu inayohitajika uwe unajua Computer Programing. Popote ulipo unaweza kua member ila huwezi kukuta kwamba wanauongozi au mikutano.

Hilo ndio kundi la Anonymous hacker, wao wanasema wamegoma kukaa kimya.. Je wewe binafsi uko tayari kusema yale unayohitaji kusema unapoona mambo hayaendi kwenye serikali yako? ni wachache sana nchi hii wanaweza fanya hivo. Ila You have all rights not to remain Silent if you supposed to speak. Kama yahitajika kuongea ongea kama hutaweza ongea unguruma, usipoweza kuunguruma piga kelele ilimradi tu usibaki kimya.. we all need freedom of speech. Amani bila ya uhuru wa kuongea ni Udikteta while we are proclaiming ourselves to have Democracy and liberty! Martin Luther anasema siku tutakapoamua kuwa kimya katika mambo ya muhimu ndio tutakua tumeamua kufikisha tamati maisha yetu. Nobody can kill or arrest your ideas, only you!
Jesus walimkataza asiongee kua yeye ni mwana wa Mungu ila hakukaa kimya hadi siku yake anakufa aliendelea kusema.
FB_IMG_15749498947184420.jpg


Anonymous Hackers
-We are Legion, Expect US
The End..
Vers
el maestro
 
Tayari kiongozi hua silali na kiporo..
Iko hivi je kuna mtu aliyewezamfunga Samaki mdomo.?
Huwezizuia watu kuongea ukiwazuia ndani wataongea nje, ukiwazuia kuongea mawe yataongea. Wengi wamepotea wengine wameumizwa kwa risasi, bambikwa kesi, filisiwa, nk.Je tumefanikiwa kuwafunga mdomo?
 
No don't do this.. nazungumzia serikali zote za Africa
True thus ufukara umetamalaki miaka 60 tangu uhuru Africa,check mataifa yanayoruhusu watu wao kuongea yalivo mbali kiuchumi.Biblia inasema taifa lolote pasipo mashauri lzm litaanguka.Maana ya neno mashauri ni kuzungumza
 
Iko hivi je kuna mtu aliyewezamfunga Samaki mdomo.?
Huwezizuia watu kuongea ukiwazuia ndani wataongea nje,ukiwazuia kuongea mawe yataongea.Wengi wamepotea wengine wameumizwa kwa risasi,bambikwa kesi,filisiwa,nk.Je tumefanikiwa kuwafunga mdomo?
Sidhani mkuu...
Ila kimya kingi kina kishindo wanasema
 
Back
Top Bottom