Kifahamu kilimo cha maua

Aisee taarifa yenye kufikirisha watendaji hiyo kwa Kusafiri wa anga.
 
Haya mwerevu mwenye akili hivi huo uwanja ulioutaja hapo juu Health law International Airport ndiyo uko nchi gani?
 
Ngoja nikuongezee kidogo, Kenya vilevile ina ndege zake zinaenda moja kwa moja abroad!!
Kwahiyo Kuna u muhimu wa kuwa na Shirika la ndege la nchi husika kuwa strong ili kusaidia hata biashara kama hizi.
 
Kabisa na huo ni ukweli
 
Haya mwerevu mwenye akili hivi huo uwanja ulioutaja hapo juu Health law International Airport ndiyo uko nchi gani?
UK London!! Unajua ulikuja na maneno ya kukaa Arusha miaka 10, sio hoja. Mtu anaweza kaa siku moja, akaomba historia ya hiyo biashara akaambiwa kuwa tangu zamani, iko hivyo. Usihofu ili ni jamvi la kuelimishana, kufundishana, kuonyana na nk.
 
Kwahiyo Kuna u muhimu wa kuwa na Shirika la ndege la nchi husika kuwa strong ili kusaidia hata biashara kama hizi.
Ndio haisaidii biashara hizi tu, itasaidia hata wafanya biashara wengine. Tena hata kuwa na Meli ya mizigo ndio suala muhimu sana kwa nchi, maana itakuza za uchumi.
 
Punguzeni charges za landing kwa kichwa utaona watalii watashuka pale
 
Serikali iboreshe mazingira ya biashara ipunguze tozo na kuondoa ushuru usio wa lazima ndio ndege zitakuja hapo hakuna bla blah....
 
Ni kwa sababu yanauzwa kupitia european middle men
Mkuu, hapana hilo sula la middle men nalikataa, kwa sababu hizi:-
Suala la biashara yoyote, licha ya kwamba si mtaalamu sana, kabla ya kumfikia mlaji ina watu watatu. Mkulima, mfanyabiashara wa kati,mkubwa na mlaji. Sasa huyo wa kati ndio wengi wetu tunamuita middle men, lakini kwa ukweli sio. Yeye anakuwa na nguvu ya ushawishi na hela kidogo sana, hela nyingine ataipata kwa mfanyabiashara mkubwa, ambaye yeye atapeleka kwa mlaji moja kwa moja.
 
Ipo research iliyofanywa kuhusu biashara ya maua hapo Arusha...na walisema hayo ya middle men.
Kila mwaka hao middle men wanaingia Arusha kufuatilia kilimo cha maua.

By the way upo msuguano wa muda mrefu kati ya mashamba haya ya maua na ofisi ya Rais/Makamu wa Rais Mazingira.

Madawa yanayotumika katika kilimo hiki ni hatarishi kwa mazingira ...learn more on POPs
 
Serikali iboreshe mazingira ya biashara ipunguze tozo na kuondoa ushuru usio wa lazima ndio ndege zitakuja hapo hakuna bla blah....
Hebu kuwa specific...ni kodi zipi hizo?
 
HIlo ndilo ambalo Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) chini ya Bwana Hamza Johari wanakutana sasa kujadili

Wadau wa usafiri wa anga watakutana kwa siku mbili mjini hapa kujadili mambo mbalimbali, ikiwemo namna ya kuufanya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kuwa njia panda ya usafiri wa anga.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amesema leo Jumatatu kuwa, mada tisa zitajadiliwa miongoni mwa hizo zikiwa ni kupungua kwa shehena ya mizigo katika sekta hiyo, udhibiti wa matumizi ya ndege zisizo na rubani na ukaguzi wa viwango vya kimataifa.

TCAA kwa kushirikiana na wadau wa usafiri wa anga wameandaa kongamano la siku mbili kuanzia kesho kujadili namna ya kuiinua na kuiboresha sekta hiyo.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ‘Kupeleka juu sekta ya usafiri wa anga’ litafanyika mjini hapa na litazinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

"Kongamano hili litatusaidia kujua wapi tunakosea na kuibua mpango mkakati wa namna ya kusahihisha makosa hayo. Ili nchi iweze kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati ni lazima kila sekta ifanye mambo muhimu," amesema Johari.

Amesema wadau wa sekta watazungumza na wao watajitathmini kila mmoja kwa nafasi yake na baadaye watachukua hatua itakayowafikisha mahali wanapotarajia kufika.

"Kwa mujibu wa Shirika Usafiri wa Anga la Kimataifa (ICAO), katika ukaguzi na udhibiti wa viwanja vya ndege tumepiga hatua kutoka asilimia 37.8 mwaka 2013 hadi asilimia 64.4 mwaka huu na tunapaswa kuendelee juu zaidi," amesema Johari.
 
Ukipandisha ua rose kwenye bombardier likifika London limemong'onyoka na linanuka moshi
 

Umenena vyema kabisa KIA uwezo huo hawana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…