Kifahamu kilimo cha maua

Kifahamu kilimo cha maua

Maelezo mazuri asante! Issue ni je soko liko wapi? Wengi wamekichukia kilimo kwa sababu hizo! Anaambiwa zao fulani zuri, lina pesa & demand kubwa analima! End of the day hajui solo liko wapi anaishia kukata mtaji wake!

This is soooo true UKWELI MTUPU HUU maana kumekuwepo na kuingia katika kilimo kwa kufuata mkumbo ama kulima kwa mazoea...hii imeshapitwa na wakati kama inawezekana kwanza tafuta masoko then pia kama unaweza ingia katika mkataba na hiyo kampuni then ndio uingie shamabani...
 
Zile kampuni za mbegu zinasumbua sana hasa kama huja meet vigezo vyao.

Hii Margold unavuna maua pekee na si mbegu na unayakausha then unayasaga kwenye mashine
Nimependa sana uzi wako nami nataka unipe mbinu za kulima haya maua ya maligold pls au nipe dondoo kidogo na mbegu nazipata wapi na udongo gani unaofaa na hali ya hewa gani inayofaa kulima kilimo hichi mm niko dar
 
Hayo mau Mara nyingi hayachagui mahali huku Kilimanjaro tena nje ya mji katika wilaya ya same vijijini hapo mengi kumbe nipo na zao zuri hasa kwa ufugaji wa kuku sijui woi naanza kuyapanda kwa faida ya kuku wangu
 
Mkuu ungemalizia Uzi kwa kutaja bei ya kuuzia hayo maua na utaje kwa mfano ukiwa Arusha sehemu flani au kampuni Fulani wananunua na kadhalika...
 
Kuna mahala nilipita nilikuta yamelimwa mahali sikujua matumizi yake ngoja nitamtafuta huyo mtu anipe dondoo mbili tatu
 
Airport yetu kuanzia safari ni usumbufu utaulizwa maswali Mia umeyatoa wapi? Unapeleka wapi? Kwanini Unapeleka? Una kibali? Kodi umelipa? Una cheti cha uraia?....
 
Nimekaa Arusha miaka mingi kikazi na eneo la Arumeru kina ma Lab hall makubwa ambayo ni mashamba makubwa ya maua.Cha ajabu maua Karibu yote yanasafirishwa kupitia kiwanja cha ndege cha Kenya Jomo Kenyatta wakati tuna kiwanja kizuri tu pale Kilimanjaro cha KIA

Tatizo ni nini KIA haitumiki kusafirisha maua kwenda Ulaya kutoka mashamba ya Arusha?

Au kuna watu wana maslahi na usafirishaji hayo maua huko Kenya?

Mkuu, acha kuuliza maswali kama wale wanaosema Dreamliner yetu sasa ndio italeta watalii nchini badala ya kutumia mashirika mengine ya ndege. Au unataka watu wa maua walazimishwe kuyapandisha maua yao kwenye Dreamliner yaje Dar?

KIA, mashirika makubwa yanayotua pale ni KLM na Ethiopian Airways. Sasa kama hayo maua yanapelekwa nchi ambako pale Nairobi JKIA ndipo kuna direct flight kwenda nchi hizo, huoni ni hesabu ndogo sana kuamua yapitie Nairobi?

Chkulia kwa mfano, hayo maua yanaenda Germany. Ukipeleka KIA itabidi uyaweke ndani ya KLM kisha yaende Amsterdam kupitia Dar, kisha kutoka Amsterdam yahamishiwe kwenda kwenye ndege nyingine ili yaende Germany. Sasa sio rahisi zaidi kuyapeleka Nairobi ili yawekwe kwenye ndege ya Lufthansa inayoenda moja kwa moja Germany kutoka Nairobi?

Nikupe mfano mwingine. Mimi ni Mtanzania nipo Arusha. Ninaposafiri kwenda Geneva, France au Germany kutoka Arusha naenda kupandia ndege Nairobi, Swiss Air, Air France/Kenya Airways au Lufthansa. Siwezi kusafiri hadi Dar ndio nipande ndege ya kwenda Geneva, Paris au Frankfurt. Kama huko ni kukosa uzalendo basi wakae na uzalendo wao! Kwanza humu barabarani magari ya serikali yanakimbia ovyo yasije yakatuua bure!

Kwanza nasikia siku hizi kuna maswali ya kitotoa sana pale Dar airport baada ya Kangi Lugola kusema Watanzania wasiende nje kutembea au kufanya kazi.
 
Hivi Boing 777 inauwezo wa kutua hapo KIA?? Magufuli badala ya kupanua uwanja wa KIA ili kuendana na ushindani wa kibiashara.. Yeye kaenda kutengeneza uwanja Chato..... Wacha wakenya watupige za uso MK254

Cc barafu
KIA inapanuliwa pia
 
Hivi Boing 777 inauwezo wa kutua hapo KIA?? Magufuli badala ya kupanua uwanja wa KIA ili kuendana na ushindani wa kibiashara.. Yeye kaenda kutengeneza uwanja Chato..... Wacha wakenya watupige za uso

Hapo tusimwonee Magufuli. Ukisha sema International Airport ina maana ndege karibu zote zinaweza kutua, labda iwe ndege kubwa ya mizigo imesheheni kupita kiasi ndio itashindwa kuruka. Tena kutua ni rahisi zaidi, unaweza kutua Boeing 777 hata uwanja wa Shinyaka, na kuirusha kama haitakuwa na mzigo. Unakumbuka kuna wakati Airbus 340 ilitua uwanja mdogo wa Arusha walipokosea badala ya kutua KIA?

Kwa mtaji huu, hata Songwe ya Mbeya inaweza kutua Boeing 777 au hata Airbus 380. Mara nyingi ruway ya kilometa 2 inatosha kabisa. Hizo nyingine zinakuwa za ziada tu, pia kutoa nafasi kubwa zaidi ya usalama ndege inapofikia spidi ya kuruka na kupunguza kitu kinaitwa "point of no return" wakati wa ku-take off, yaani extra length iliyopo wakati ndege imefikia spidi ya kuruka.
 
Nimekaa Arusha miaka mingi kikazi na eneo la Arumeru kina ma Lab hall makubwa ambayo ni mashamba makubwa ya maua.

Cha ajabu maua Karibu yote yanasafirishwa kupitia kiwanja cha ndege cha Kenya Jomo Kenyatta wakati tuna kiwanja kizuri tu pale Kilimanjaro cha KIA

Tatizo ni nini KIA haitumiki kusafirisha maua kwenda Ulaya kutoka mashamba ya Arusha?

Niliwahi kusikia tuna wataalam wachache wa air yaani Air Technicians!! Ilitolewa na Waziri Prof Mbarawa!

Usafirishaji wa maua sio wa leo wala Jana lakini kwanini wataalam wameshindwa kutumia KIA kwani Kuna upungufu gani kiwanjani hapo!?!

Au kuna watu wana maslahi na usafirishaji hayo maua huko Kenya?
Sina uhakika sana, ila nijuacho ni kwamba mashamba mengi yanamilikiwa na wakenya na ndio wazalishaji wakubwa wa maua E. Africa kama sio Africa nzima.
Baada ya kuvunwa ni lazima yake processed n.a. kuwekwa nembo, so labda ni ngumu kuweka nembo ya made in Kenya wakati mzigo unalimwa, unafungiwa na kusafirishwa toka tz.
Pia imumbukwe issues za kodi, ajira(kwenye packaging nk) wanataka ziendelee kulipwa Kenya as part ya uzalendo kwa nchi yao.
 
Acha ujinga wewe, Jomo Kenyeta International Airport ni ya 100 kwa huduma za ndege duniani. Kila baada ya dk 15 ndege 4 kubwa zinashuka na 4 zinapaa kila siku. Oriva Tambo Johs wenyewe kila baada ya dk 15 ndege 10 zina land 10 zina take off. Uwanja unaongoza kwa shughuli duniani ni Health law International Airport. Kila baada ya dk 15 ndege 50 zinaland 50 zina took off. Sasa ndio unaweza kuufananisha na KIA au? Ikiwa hata DIA wenyewe hauifikii JKIA.
Nilirudi kwenye point yako ya kijinga, KIA ina ndege ya moja kwa moja kwenda Abroad pale, au unajua yale maua yanaenda kuuzwa Kisumu nini? Acheni chuki na wivu wa kitoto, eti ukiongea hivyo basi nani unategemea asikie eti aulize au akataze kupeleka JKIA utakufa maskini ndugu yangu, kama hata vitu vidogo hivyo vinakusumbua.
ameuliza akitaka kuelewesha sababu hasa ni nini? sidhani kama kulikuwa na sababu ya kutumia lugha kali kiasi hicho
 
Sina uhakika sana, ila nijuacho ni kwamba mashamba mengi yanamilikiwa na wakenya na ndio wazalishaji wakubwa wa maua E. Africa kama sio Africa nzima.
Baada ya kuvunwa ni lazima yake processed n.a. kuwekwa nembo, so labda ni ngumu kuweka nembo ya made in Kenya wakati mzigo unalimwa, unafungiwa na kusafirishwa toka tz.
Pia imumbukwe issues za kodi, ajira(kwenye packaging nk) wanataka ziendelee kulipwa Kenya as part ya uzalendo kwa nchi yao.
Nadhani si wengi hao wakenya kwenye mashamba ya maua hapo Arusha ...nimetmbelea hayo mashamba kuna baadhi ya wawekezaji wazungu hapo
 
Hivi Boing 777 inauwezo wa kutua hapo KIA?? Magufuli badala ya kupanua uwanja wa KIA ili kuendana na ushindani wa kibiashara.. Yeye kaenda kutengeneza uwanja Chato..... Wacha wakenya watupige za uso MK254

Cc barafu

Klm boeing 777 inatua KIA daily , na wakati JOMO KENYATTA AIPORT iliungua Moto ndegezilizokuwa zitue nairobi zilielekezwa kutua KIA.kumbuka airforce one ya Bush na Clinton ilitua KIA

Kuna jamaa alikuwa na lori la friji alikuwa anasafirisha maua toka njombe mpaka KIA kwa ajili ya kupelekwa ulaya 2011 kurudi nyuma

labda hao wakulima wa arusha na moshi wamechukua sub contract ya kuzalisha maua kutoka kwa main supplier wa kenya ambao wamezidiwa na demand ya customer wao wa europe
 
Sina uhakika sana, ila nijuacho ni kwamba mashamba mengi yanamilikiwa na wakenya na ndio wazalishaji wakubwa wa maua E. Africa kama sio Africa nzima.
Baada ya kuvunwa ni lazima yake processed n.a. kuwekwa nembo, so labda ni ngumu kuweka nembo ya made in Kenya wakati mzigo unalimwa, unafungiwa na kusafirishwa toka tz.
Pia imumbukwe issues za kodi, ajira(kwenye packaging nk) wanataka ziendelee kulipwa Kenya as part ya uzalendo kwa nchi yao.
Hapana nakusahihisha.
Makampuni yanayozalisha maua mikoa ya kaskazini Arusha na Kilimanjaro ni ya wazungu. Na hata makampuni yaliyopo kenya yanayozalisha maua pia ni ya wazungu.
Mimi ni mwenyeji wa kule na nayafahamu sana fika mashamba hadi asili ya wazungu wanakotokea.
Pointi ni kwanini wanapitia Nairobi kenya badala ya kusafirisha kwa kutumia uwanja wa KIA.
Kuna mtu kaelezea nadharia nzuri kuwa uwanja wa nairobi unazo direct flight nyingi kuliko KIA.
Na ametolea mfano pia sio maua tuu bali watu wengi wa mikoa ya kaskazini wanatumia Uwanja wa Nairobi kupata safari za moja kwa moja.
 
KIA hakuna direct flights na pia hakuna cargo planes!

Ova
 
Sina uhakika sana, ila nijuacho ni kwamba mashamba mengi yanamilikiwa na wakenya na ndio wazalishaji wakubwa wa maua E. Africa kama sio Africa nzima.
Baada ya kuvunwa ni lazima yake processed n.a. kuwekwa nembo, so labda ni ngumu kuweka nembo ya made in Kenya wakati mzigo unalimwa, unafungiwa na kusafirishwa toka tz.
Pia imumbukwe issues za kodi, ajira(kwenye packaging nk) wanataka ziendelee kulipwa Kenya as part ya uzalendo kwa nchi yao.

Sio kweli mashamba ni ya wazungu na maua ni perishables lazima yafike sokoni haraka so kwa sababu kenya kuna direct flight za Europe na mashirika kama KQ yana freighter za cargo so kwanza mzigo unafika haraka na kwa bei nafuu. Ukitaka kwenda nje kupitia Kenya even the fare is cheaper.
 
Back
Top Bottom